Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiomba kati ya sijida mbili katika sala yake kwa dua hizi tano ambazo muislamu anazihitajia kwa uhitaji mkubwa, na zimekusanya heri za dunia na akhera, ikiwemo kuomba msamaha na stara ya madhambi na kufutwa kwake, na kumiminiwa rehema, na kusalimishwa na mambo yenye utata na matamanio na maradhi na magonjwa, na kumuomba Allah uongofu katika haki na kudumu katika hilo, na kupewa imani na elimu na matendo mema, na mali nzuri ya halali.
- Sheria ya kuomba dua hii katika kikao kati ya sijida mbili.
- Ubora wa dua hizi kwa kukusanya heri za dunia na akhera.
سنن أبي داود (2/ 138) (850). سنن الترمذي (1/ 317) (284). سنن ابن ماجه (2/ 64) (898). مسند أحمد (5/ 72) (2895). مشكاة المصابيح، للتبريزي (1/ 283). سبل السلام شرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (1/ 274). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 240).