Utakaposujudu basi weka viganja vyako, na unyanyue viwiko vyako
عَنِ الْبَرَاءِ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا سَجَدْتَ، فَضَعْ كَفَّيْكَ وَارْفَعْ مِرْفَقَيْكَ».
Kutoka kwa Suhaib -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Utakaposujudu basi weka viganja vyako, na unyanyue viwiko vyako".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya mikono miwili katika sijida ya swala, nayo ni kwa kuviweka vizuri viganja vyake katika ardhi na aviweke vidole vikiwa vimefungamanishwa kuelekea kibla, na viwe viwiko viwili -maungio ya mkono na muundi wake- viwe vimenyanyuka na viko mbali na kugusa Ardhi, na vimeachanishwa na mbavu.
Mafunzo
Jambo la wajibu kwa mwenye kuswali ni kuweka viganja vyake juu ya Ardhi, na viganja viwili ni viungo katika viungo saba vya kusujudu.
Ni sunna kunyanyua miundi ya mikono isiguse Ardhi, na machukizo ya kuilaza kama anavyolaza mnyama mkali mikono yake.
Sheria ya kuonyesha uchangamfu na nguvu na hamu katika ibada.
Mwenye kusali akiegemea viungo vyake vyote vya kusujudu, kila kiungo kitachukua haki yake katika ibada.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 356) (494).
سبل السلام شرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (1/ 273).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 235).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص162).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com