Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah
عَنْ وَائِل بن حُجرٍ رضي الله عنه قَالَ: صَلَّيْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَكَانَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ: «السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ»، وَعَنْ شِمَالِهِ: «السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ».
Kutoka kwa Waili bin Hujari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Niliswali pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikuwa akitoa salaam kuliani kwake: "Assalaam alaikum warahamatullah wabarakaatuh", na kushotoni kwake: "Assalaam alaikum warahmatullah".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kumaliza swala yake anatoa salaam kuliani kwake na kushotoni kwake kwa kugeuka kwa uso wake upande wa kulia, pamoja na kusema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na anatoa salaam kushotoni kwake, kwa kugeuza uso wake upande wa kushoto, pamoja na kusema: "Assalaam alaiku warahmatullah".
Mafunzo
Sheria ya kutoa salaam mbili ndani ya swala, nakuwa salam hizo ni katika nguzo zake.
Inapendeza kuleta ziada ya kauli "wabarakaatuh", katika baadhi ya nyakati; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwa anadumu nayo.
Kutamka salaam mbili ndani ya swala ni nguzo ya wajibu, na ama kitendo cha kugeuka wakati wa kuzitamka ni sunna.
Inatakiwa iwe kauli ya: "Assalaam alaikum warahmatullaah" wakati wa kitendo cha kugeuka na si kabla yake wala baada yake.
Marejeo
سنن أبي داود (2/ 239) (997).
المجموع شرح المهذب (مع تكملة السبكي والمطيعي) النووي (3/ 479).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، النووي (4/ 153).
توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 291).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com