Imepokewa kutoka kwa Abuu Aufaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuu anasema: "Sami'allaahu liman hamidah, Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati wamil al Ardhwi wamil amaashi ita min shai in ba'ad".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- anaponyanyua mgongo wake kutoka katika rukuuu ndani ya swala, anasema: " Sami'allaahu liman hamidah", Yaani: Atakayemhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atamjibu, na atakubali himidi zake na atamlipa, kisha atamhimidi kwa kusema: Allaahumma Rabbanaa lakal hamdu, mil as samaawaati, wamil al Adhwi wamil amaa shi ita min shai in baad", himdi zenye kujaza mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, na zinajaza ayatakayo Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Kumebainishwa anayotakiwa kusema mwenye kusali anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu.
Sheria ya kulingana sawa na utulivu baada ya kuinuka kutoka katika rukuu; kwa sababu haiwezekani aseme dhikiri hii ila baada ya kusimama wima na kutulia.
Dhikiri hii ni sheria katika swala zote, sawa sawa ziwe za faradhi au za sunna.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 346) (476)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (11/ 114).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com