Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa

عَنْ أَبِي أُمَامَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ قَرَأَ آيَةَ الْكُرْسِيِّ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ مَكْتُوبَةٍ لَمْ يَمْنَعْهُ مِنْ دُخُولِ الْجَنَّةِ إِلَّا أَنْ يَمُوتَ».
Kutoka kwa Abuu Umama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Yeyote atakayesoma Ayatul Kursiy mwisho wa kila swala ya faradhi hakuna kitakachomzuia kuingia peponi isipokuwa kufa".
Imepokelewa na Nasai katika kitabu AlkubraaDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema kuwa mwenye kusoma Ayatul-Kursi baada ya kumalizika kwa swala ya faradhi, hakuna kitakachomzuia kuingia Peponi isipokuwa kifo; nayo iko katika Suratul Baqarah, Mwenyezi Mungu anasema: "Mwenyezi Mungu - hapana mungu isipokuwa Yeye, Aliye hai, Msimamizi wa mambo yote milele. Hashikwi na kusinzia wala kulala. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Ni nani huyo awezaye kufanya uombezi mbele yake isipokuwa kwa idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao, wala wao hawajui vyema chochote katika elimu yake isipokuwa kwa kile akitakacho. Kuti chake cha enzi kimeenea mbingu na dunia, na wala halemewi na kuvilinda vyote viwili. Na Yeye ndiye aliye juu zaidi, Mkuu." [Al-Baqara: 255]

Mafunzo
  1. Fadhila ya Aya hii tukufu; kwa kukusanya kwake majina mazuri, na sifa za hali ya juu.
  2. Sunna ya kusoma Aya hiyo tukufu baada ya swala za faradhi.
  3. Matendo mema ni sababu ya kuingia peponi.
Marejeo

المعجم الكبير، للطبراني السنن الكبرى، للنسائي (9/ 44) (9848). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (2/ 313). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (3/ 197).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adh-kaar - zisomwazo- wakati wa swala.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com