Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِذَا كَبَّرَ فِي الصَّلَاةِ، سَكَتَ هُنَيَّةً قَبْلَ أَنْ يَقْرَأَ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ بِأَبِي أَنْتَ وَأُمِّي أَرَأَيْتَ سُكُوتَكَ بَيْنَ التَّكْبِيرِ وَالْقِرَاءَةِ، مَا تَقُولُ؟ قَالَ «أَقُولُ: اللهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللهُمَّ اغْسِلْنِي مِنْ خَطَايَايَ بِالثَّلْجِ وَالْمَاءِ وَالْبَرَدِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapotoa takbira katika swala ananyamaza kidogo kabla hajaanza kusoma, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimuweka fidia baba yangu na mama yangu, hebu nieleze kunyamaza kwako kati ya takbira na kisomo: Ni nini unasema: Akasema: Ninasema: Allaahumma baaid bainiy -Ewe Mwenyezi Mungu weka mbali baina yangu- wa baina khatwaayaaya -na baina ya makosa yangu- kamaa baa a'tta bainal mashriqi wal maghribi -kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Allaahumma naqqiniy- Ewe Mwenyezi Mungu nitakase mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- kamaa yunaqqath-thaubul abyadhwa -kama inavyotakaswa nguo nyeupe- minad danasi -kutokana na uchafu. Allaahumma ghsilniy -Ewe Mwenyezi Mungu nioshe mimi- min khatwaayaaya -kutokana na makosa yangu- bil maai wath thalji wal baradi -kwa maji na barafu na baridi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema “Allahu Akbar” kwa ajili ya swala, alikuwa akitulia kidogo kabla ya kusoma Al-Fatiha, ambamo alikuwa akiianza Swala yake kwa baadhi ya dua, miongoni mwa dua hizo zilizoripotiwa ni kauli yake: "Allaahumma baaid bainii wa baina khatwaa yaaya, kamaa baa'atta bainal mashriqi wal maghribi, Allaahu naqinii min khatwaayaaya, kamaa yunaqqah-thaubal abyadhwa minad-danasi, Allaahuma gh-silnii bil maai wath-thalji wal baradai", Hivyo anamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amtenge mbali na madhambi ili asije akaangukia ndani yake, hata kusiwe na kukutana nayo, kama vile hakuna kukutana baina ya Mashariki na Magharibi, na ikitokea katumbukia ndani yake, basi amtakase kutokana na madhambi hayo kama uchafu unavyotolewa kwenye nguo nyeupe, na amuoshe dhambi zake na kuupoza miale na joto lake, kwa vitakatishi hivi baridi; Maji, theluji na baridi.

Mafunzo
  1. Kuificha dua ya ufunguzi wa swala, hata kama swala itakuwa ni ya kusoma kwa sauti.
  2. Pupa ya Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao katika kutaka kujua hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika harakati zake na kutulia kwake.
  3. Zimekuja namna nyingine za dua ya ufunguzi, na kilicho bora kwa mtu afuatilie dua zilizokuja na kuthibiti kutoka kwake rehema na amani ziwe juu yake, ili asome hii wakati mwingine, na hii wakati mwingine.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 149) (744). صحيح مسلم (1/ 419) (598). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 118). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص143). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 186).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adh-kaar - zisomwazo- wakati wa swala.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com