عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا تَوَضَّأَ أَحَدُكُمْ فَلْيَجْعَلْ فِي أَنْفِهِ ثُمَّ لِيَنْثُرْ، وَمَنِ اسْتَجْمَرَ فَلْيُوتِرْ، وَإِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلْيَغْسِلْ يَدَهُ قَبْلَ أَنْ يُدْخِلَهَا فِي وَضُوئِهِ، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ لاَ يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدُهُ».
ولفظ مسلم: «إِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلَا يَغْمِسْ يَدَهُ فِي الْإِنَاءِ حَتَّى يَغْسِلَهَا ثَلَاثًا، فَإِنَّهُ لَا يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدُهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke maji puani mwake kisha ayapenge, na atakayestanji kwa mawe basi afanye yawe witiri, na atakapo amka mmoja wenu toka usingizini basi na aoshe mikono yake kabla ya kuingiza ndani ya chombo chake, kwani mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake". Na lafudhi ya Muslim: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini kwake basi asizamishe mkono wake ndani ya chombo mpaka auoshe mara tatu, kwani hajui ni wapi ulilala mkono wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya hukumu za twahara, miongoni mwake: Ya kwanza: Nikuwa mwenye kutawadha ni lazima aingize maji puani mwake kwa kuyavuta kwa pumzi, kisha ayatoe kwa pumzi pia. Ya pili: Nikuwa atakayetaka kusafisha udhia uliomtoka na kuuondoa pasina kutumia maji kama kwa jiwe na mfano wake, basi kusafisha kwake kuwe kwa idadi ya mamoja (witiri) kwa uchache tatu na kuendelea yatakayoweza kutakatisha kilichotoka na kusafisha mahali. Ya tatu: Kuwa atakayeamka kutoka katika usingizi wa usiku asiingize kiganja chake ndani ya chombo ili atawadhe mpaka akioshe mara tatu nje ya chombo, kwani hajui ni mahali gani ulilala mkono wake, hauwezi kuaminika na kutokuwa na najisi, na huenda shetani aliuchezea na akaubebesha vitu vyenye kumdhuru mwanadamu au vyenye kuharibu maji.
Mafunzo
- Ni wajibu kupandisha maji puani wakati wa udhu, nako ni: Kuingiza maji puani kwa njia ya pumzi, na pia ni wajibu kuyapenga, nako ni: Kuyatoa maji puani kwa njia ya pumzi.
- Inapendeza kupenga kwa witiri.
- Ni sheria kuosha mikono miwili baada ya kutoka usingizini mara tatu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 43) (162).
صحيح مسلم (1/ 233) (278).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص19).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 11).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا تَوَضَّأَ الْعَبْدُ الْمُسْلِمُ -أَوِ الْمُؤْمِنُ- فَغَسَلَ وَجْهَهُ خَرَجَ مِنْ وَجْهِهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ نَظَرَ إِلَيْهَا بِعَيْنَيْهِ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ-، فَإِذَا غَسَلَ يَدَيْهِ خَرَجَ مِنْ يَدَيْهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ كَانَ بَطَشَتْهَا يَدَاهُ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ-، فَإِذَا غَسَلَ رِجْلَيْهِ خَرَجَتْ كُلُّ خَطِيئَةٍ مَشَتْهَا رِجْلَاهُ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ- حَتَّى يَخْرُجَ نَقِيًّا مِنَ الذُّنُوبِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakapotawadha muislamu au muumini akaosha uso wake wakati wa udhu, yanatoka katika uso wake makosa yote madogo madogo aliyoyatazama kwa macho yake pamoja na maji ya yanayodondoka baada ya kuosha, au pamoja na tone la mwisho la maji, akiosha mikono yake yanatoka katika mikono yake makosa yote madogo madogo iliyoyachuma mikono yake au pamoja na tone la mwisho la maji, na akiosha miguu yake yanatoka makosa yake yote madogo madogo iliyotembea kuyafuata miguu yake, mpaka atoke akiwa kasafishika na madhambi madogo madogo kwa kumalizika kwa udhu.
Mafunzo
- Fadhila za kuhifadhi udhu, nakuwa unafuta madhambi.
- Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwahimiza watu katika utiifu na ibada, na kutaja malipo na thawabu zake.
- Kila kiungo miogoni mwa viungo vya mwanadamu huingia katika baadhi ya madhambi, na ndio maana madhambi hukifuata kila kiungo kilichoyafanya, na hutoka na kila kiungo kilichotubia kwayo.
- Udhu una usafi wa wazi, na unakuwa pale vinapooshwa viungo vya udhu, na usafi usioonekana; na unakuwa kutokana na madhambi yaliyotokea kupitia viungo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 215) (244).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 108).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 181).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 208).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 157).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «لَا يَقْبَلُ اللهُ صَلَاةَ أَحَدِكُمْ إِذَا أَحْدَثَ حَتَّى يَتَوَضَّأَ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa miongoni mwa sharti za kusihi swala: Ni twahara, ni wajibu kwa atakayetaka kuswali atawadhe ikiwa kimetokea kwake kitenguzi cha udhu; kama haja kubwa au ndogo au usingizi au kinginecho.
Mafunzo
- Swala ya mtu mwenye hadathi (kama janaba, hedhi au nifasi) haikubaliki mpaka ajitwaharishe kwa kuoga kutokana na hadathi kubwa, na kwa kutawadha ikiwa ni hadathi ndogo (kama kwenda haja kubwa au ndogo, au kulala, au kutokwa upepo)
- Udhu ni kuchukua maji na kuyazungusha mdomoni na kuyatoa, kisha kuvuta maji kwa pumzi mpaka ndani ya pua, kisha kuyatoa na kuyapenga, kisha mtu ataosha uso wake mara tatu, kisha ataosha mikono yake pamoja viwiko viwili mara tatu, kisha atafuta kichwa chake mara moja, kisha kuosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 23) (6954).
صحيح مسلم (1/ 204) (225).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص17).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 11).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com