Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Sifa za Kutawadha.

Hadithi 6

Atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili ambazo haizungumzishi ndani yake nafsi yake, basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia

عَنْ ‌حُمْرَانَ مَوْلَى عُثْمَانَ بْنِ عَفَّانَ رضي الله عنه: أَنَّهُ رَأَى عُثْمَانَ بْنَ عَفَّانَ دَعَا بِوَضُوءٍ، فَأَفْرَغَ عَلَى يَدَيْهِ مِنْ إِنَائِهِ، فَغَسَلَهُمَا ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ أَدْخَلَ يَمِينَهُ فِي الْوَضُوءِ، ثُمَّ تَمَضْمَضَ وَاسْتَنْشَقَ وَاسْتَنْثَرَ، ثُمَّ غَسَلَ وَجْهَهُ ثَلَاثًا، وَيَدَيْهِ إِلَى الْمِرْفَقَيْنِ ثَلَاثًا، ثُمَّ مَسَحَ بِرَأْسِهِ، ثُمَّ غَسَلَ كُلَّ رِجْلٍ ثَلَاثًا، ثُمَّ قَالَ: رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَوَضَّأُ نَحْوَ وُضُوئِي هَذَا، وَقَالَ: «مَنْ تَوَضَّأَ نَحْوَ وُضُوئِي هَذَا ثُمَّ صَلَّى رَكْعَتَيْنِ لَا يُحَدِّثُ فِيهِمَا نَفْسَهُ غَفَرَ اللهُ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Humran kijana wa Othman bin Affan alimuona Othman bin Affan akiomba kuletewa chombo cha udhu, akamimina juu ya mikono yake kutoka katika chombo chake, akaiosha mara tatu, kisha akaingiza mkono wake wa kulia katika chombo, kisha akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga(akayatoa), kisha akaosha uso wake mara tatu, na mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara tatu, kisha akafuta kichwa chake, kisha akaosha kila mguu mara tatu, kisha akasema: Nilimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu wangu huu, na akasema: "Atakayetawadha mfano wa udhu wangu huu, kisha akasali rakaa mbili ambazo haizungumzishi ndani yake nafsi yake, basi Allah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Othman -Radhi za Allah ziwe juu yake- alifundisha sifa ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa njia ya vitendo; Ili ueleweka vizuri zaidi, akaomba maji katika chombo, akamimina katika mikono yake mara tatu, na baada ya hapo aliingiza mkono wake wa kulia katika chombo, na akachukua maji akayazungusha kinywani mwake na akayatoa, kisha akavuta kwa pumzi yake kuja ndani ya pua yake, kisha akayatoa na akayapenga, kisha akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake pamoja na viwiko viwili mara tatu, kisha akapitisha mkono wake juu ya kichwa chake ukiwa umeloa kwa maji mara moja, kisha akaosha miguu yake pamoja na fundo mbili mara tatu. Alipomaliza radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimuona Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha mfano wa udhu huu, na akawapa bishara -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetawadha mfano wa udhu wake, na akaswali rakaa mbili, kwa utulivu na kuhudhuriasha moyo mbele ya Mola wake Mtukufu ndani yake, basi Allah atamlipa kwa udhu huu mkamilifu na kwa swala hii iliyotakaswa kwa kumsamehe yaliyotangulia katika madhambi yake.

Mafunzo
  1. Inapendeza kuosha mikono miwili kabla ya kuiingiza katika chombo mwanzo wa udhu, hata kama hajaamka kutoka usingizini, na akiwa kaamka kutoka usingizini basi ni wajibu kuiosha.
  2. Ni lazima mwalimu atumie njia ya karibu na uelewa na kuifanya elimu ikite kwa mwenye kujifunza, na katika hilo ni kufundisha kwa vitendo.
  3. Ni lazima kwa mwenye kuswali kuzuia mawazo yanayohusiana na shughuli za kidunia, utimilifu wa swala na ukamilifu wake ni katika kuhudhuria moyo ndani yake, na kama si hivyo mawazo ni vigumu kusalimika nayo, anatakiwa apambane na nafsi yake na asiruhusu yaendelee.
  4. Sunna ya kuanza na kulia katika udhu.
  5. Sheria ya kupangilia kati ya kusukutua na kupandisha maji puani na kupenga.
  6. Sunna ya kuosha uso na mikono miwili na miguu miwili mara tatu tatu, na wajibu ni mara moja.
  7. Mwenyezi Mungu kuyasamehe yaliyotangulia katika madhambi kunaambatana na mambo mawili: Udhu, na kuswali rakaa mbili, kwa sifa iliyotajwa katika hadithi.
  8. Kila kiungo katika viungo vya udhu kina mpaka: Mpaka wa uso: Kwa urefu ni kuanzia maoteo ya nywele za kichwa ya kawaida, mpaka chini katika ndevu na kidevu, na kwa upana ni sikio kwa sikio. Na mpaka wa mkono: Ni kuanzia ncha za vidole mpaka katika kiwiko nayo ni maungio kati ya muhundi na sehemu ya juu kuelekea begani. Na mpaka wa kichwa: Ni kuanzia maoteo ya kichwa ya kawaida kando kando ya uso mpaka juu ya shingo, na kufuta masikio mawili ni sehemu ya kichwa. Na mpaka wa mguu ni: Mguu wote pamoja na maungio kati yake na muhundi.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 44) (164). صحيح مسلم (1/ 204) (226). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 16). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص26). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 24).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

akatawadha mbele yao udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-

عَنْ يحيى بنِ عُمَارةَ المَازِنِيِّ قَالَ: شَهِدْتُ عَمْرَو بْنَ أَبِي حَسَنٍ سَأَلَ عَبْدَ اللَّهِ بْنَ زَيْدٍ، عَنْ وُضُوءِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَدَعَا بِتَوْرٍ مِنْ مَاءٍ، فَتَوَضَّأَ لَهُمْ وُضُوءَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَكْفَأَ عَلَى يَدِهِ مِنَ التَّوْرِ، فَغَسَلَ يَدَيْهِ ثَلاَثًا، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فِي التَّوْرِ، فَمَضْمَضَ وَاسْتَنْشَقَ وَاسْتَنْثَرَ، ثَلاَثَ غَرَفَاتٍ، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فَغَسَلَ وَجْهَهُ ثَلاَثًا، ثُمَّ غَسَلَ يَدَيْهِ مَرَّتَيْنِ إِلَى المِرْفَقَيْنِ، ثُمَّ أَدْخَلَ يَدَهُ فَمَسَحَ رَأْسَهُ، فَأَقْبَلَ بِهِمَا وَأَدْبَرَ مَرَّةً وَاحِدَةً، ثُمَّ غَسَلَ رِجْلَيْهِ إِلَى الكَعْبَيْنِ.
Imepokelewa kutoka kwa Yahya Bin Umaara Al-Maaziniy amesema: Nilimshuhudia Amri Bin Abii Hasan akimuuliza Abdallah Bin Zaidi, kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha mbele yao udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akamimina katika mikono yake kutoka katika bakuli, akaosha viganja vyake mara tatu, kisha akaingiza mkono wake ndani ya bakuli, akasukutua na akapandisha maji puani na akapenga, kwa michoto mitatu, kisha akaingiza mkono wake akaosha uso wake mara tatu, kisha akaosha mikono yake mara mbili mpaka katika viwiko viwili, kisha akaingiza mkono wake akafuta kichwa chake, akaanza upande wa mbele na akapeleka mpaka nyuma ya kichwa, mara moja, kisha akaosha miguu yake mpaka katika kongo mbili.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Abdallah Bin Zaidi radhi za Allah ziwe juu yake namna ya udhu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kwa vitendo, akaomba chombo kidogo chenye maji, kwanza kabisa akaanza kuosha viganja vyake, kisha akainamisha chombo na akamimina maji akaiosha mara tatu nje ya chombo, Kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo, akachota michoto mitatu, katika kila mchoto anasukutua na anapandisha maji puani na anapenga, Kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha uso wake mara tatu, kisha akachota kutoka ndani ya chombo akaosha mikono yake mpaka katika viwiko viwili mara mbili mbili, kisha akaingiza mikono yake ndani ya chombo akafuta kichwa chake kwa mikono yake akaanza na mbele ya kichwa chake mpaka akafika katika kisogo chake juu ya shingo, kisha akairejesha mpaka akafika mahali alipoanzia, kisha akaosha miguu yake pamoja na kongo mbili.

Mafunzo
  1. Tabia za mwalimu ni njia ya karibu zaidi ya kuleta uelewa na kuifanya elimu isisahaulike, na katika hili ni kufundisha kwa vitendo.
  2. Inafaa kurudia mara tatu katika baadhi ya viungo vya udhu na mara mbili katika baadhi yake, na wajibu ni mara moja.
  3. Uwajibu wa kufuata mpangilio kati ya viungo vya udhu kama ilivyokuja katika hadithi.
  4. Kikomo cha uso ni kuanzia maoteo ya nywele, mpaka ndevu za chini na kidevu, kwa urefu, na kuanzia sikio mpaka sikio jingine, kwa upana.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 48) (186). صحيح مسلم (1/ 210) (235). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 18). الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص72). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص29). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 27). شرح العمدة للسعدي (ص 50).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ مَنَامِهِ فَلْيَسْتَنْثِرْ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَبِيتُ عَلَى خَيَاشِيمِهِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini mwake basi na apenge kwa maji mara tatu, kwani Shetani hulala ndani ya tundu zake za pua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anamuhimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuamka kutoka usingizini mwake kuwa apandishe maji puani na kuyapenga mara tatu; ambako ni kuyatoa maji puani baada ya kuyaingiza, na hii ni kwa sababu Shetani hulala ndani ya tundu za pua - nayo ni pua yote -.

Mafunzo
  1. Anaweka sheria kwa kila mwenye kuamka kutoka usingizini apenge ili kuondoa athari za Shetani puani mwake, na endapo kama atatawadha, hapo amri ya kupenga itakuwa ni lazima.
  2. Kupenga ni katika faida kamili ya kupandisha maji puani; na kupenga kunatoa uchafu huo kupitia maji.
  3. Kufungamanisha na usingizi wa usiku pekee, kwa kuchukua kutoka katika tamko "Kulala" kwani kulala huwa hakuwi ila kwa usingizi wa usiku, kwa sababu ndio usingizi wa kulala muda mrefu na wa fofofo.
  4. Katika hadithi kuna dalili kuwa Shetani humgusa mwanadam pasina yeye kulihisi hilo.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 126) (3295). صحيح مسلم (1/ 212) (238). توضيح الأحكام، للشيخ للبسام (1/ 211). سُبل السلام، للصنعاني (1/ 64). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 179). منحة العلَّام، لعبد الله الفوزان (1/ 166).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja

عَنِ ‌ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: تَوَضَّأَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّةً مَرَّةً.
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja moja, anaosha uso pamoja kusukutua na kupandisha maji puani, na mikono miwili na miguu miwili mara moja moja, na hiki ndicho kiwango cha wajibu.

Mafunzo
  1. Kilicho wajibu katika kuosha viungo ni mara moja moja, inayozidi inapendeza kufanya hivyo.
  2. Sheria ya kutia udhu mara moja moja katika baadhi ya nyakati.
  3. Sheria katika kufuta kichwa ni mara moja.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 43) (157)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 244).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili

عَنْ ‌عَبْدِ اللهِ بْنِ زَيْدٍ رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَوَضَّأَ مَرَّتَيْنِ مَرَّتَيْنِ.
Kutoka kwa Abdallah bin Zubairi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara mbili, anaosha uso ikiwemo kusukutua na kupandisha maji puani na mikono miwili na miguu miwili mara mbili.

Mafunzo
  1. Kilicho wajibu katika kuosha viungo ni mara moja moja na kinachozidi inapendeza.
  2. Sheria ya kutia udhu mara mbili mbili katika baadhi ya nyakati.
  3. Sheria katika kufuta kichwa ni mara moja.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 43) (158)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 244).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرٍو رَضيَ اللهُ عنهما قَالَ: رَجَعْنَا مَعَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ مَكَّةَ إِلَى الْمَدِينَةِ حَتَّى إِذَا كُنَّا بِمَاءٍ بِالطَّرِيقِ تَعَجَّلَ قَوْمٌ عِنْدَ الْعَصْرِ، فَتَوَضَّؤُوا وَهُمْ عِجَالٌ، فَانْتَهَيْنَا إِلَيْهِمْ وَأَعْقَابُهُمْ تَلُوحُ لَمْ يَمَسَّهَا الْمَاءُ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «وَيْلٌ لِلْأَعْقَابِ مِنَ النَّارِ أَسْبِغُوا الْوُضُوءَ».
Kutoka kwa Abdallah bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Tulirejea tukiwa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina mpaka tulipofika katika njia yenye maji, walifanya haraka baadhi ya watu kusali laasiri, wakatia udhu wakiwa na haraka, tukawakuta na hali yakuwa visigino vyao vikiwa vyeupe havijaguswa na maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ole wao (wasiofikisha maji katika) visigino (watakua na adhabu ya) moto, enezeni maji ya udhu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alisafiri Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoka Makka kwenda Madina akiwa pamoja na Masahaba zake, wakiwa njiani walipata maji, wakaenda mbio kutia udhu kwa ajili ya swala ya Alaasiri baadhi ya Masahaba, mpaka ukaonekana weupe mwisho wa miguu yao kwa mtu mwenye kuitazama kwa kukosa maji, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ni adhabu na maangamivu katika moto kwa wenye kufanya uzembe wa kuosha mwisho wa nyayo wakati wa udhu, na akawaamrisha wapitilize katika kuukamilisha udhu.

Mafunzo
  1. Ulazima wa kuosha miguu miwili katika udhu; kwa sababu lau kama ingefaa kufuta asingetoa ahadi ya adhabu ya moto kwa mwenye kuacha kuosha mwisho wa miguu yake.
  2. Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vyenye kuoshwa wakati wa udhu, nakuwa atakayeacha sehemu ndogo ambayo ni ya wajibu kusafishwa kwa makusudi au kwa uzembe, basi swala yake haisihi.
  3. Umuhimu wa kumfundisha asiyejuwa na kumuelekeza.
  4. Msomi anatakiwa kukemea anayoyaona ikiwemo kupoteza wajibu na sunna, lakini kwa usulubu mzuri.
  5. Amesema Muhammad Is-haqa Al-Dahalawi: Kueneza maji kuna aina tatu: Lazima (Faradhi) Nako ni kueneza maji mahali unapoosha kwa mara moja, na sunna: Nayo nikuosha kiungo mara tatu, na inapendeza: kurefusha mahali unapoosha ikiwa ni pamoja na kufanya hivyo mara tatu.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 44) (163). صحيح مسلم (1/ 214) (241). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (6/ 273).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com