Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Nguzo za Udhu.

Hadithi 2

Adhabu kali ya moto itazipata nyayo za miguu

عن أبي هريرة وعبد الله بن عمرو وعائشة رضي الله عنهم عن رسول الله صلى الله عليه وسلم : أنه قال: (ويلٌ للأعْقَاب من النَّار).
Kutoka kwa Abuu Huraira na Abdillahi bin Amri na Aisha- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakwamba yeye amesema: (Adhabu kali ya moto itazipata nyayo za miguu).
Imepokelewa na Imamu Muslim - Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim kwa riwaya zakeDarajaSahihi
Maelezo

Anatahadharisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- juu ya kufanya uzembe katika swala la udhu, na kutotekeleza udhu vilivyo, na anahimiza juu ya kuzingatia kuukamilisha, na kwakuwa mwisho wa miguu mara nyingi ndio huwa hayafiki maji ya udhu, basi mapungufu yanakuwa katika twahara na swala kwasababu hiyo, na akaeleza kuwa adhabu itamiminika juu ya hilo na kwa mfanyaji wake anayefanya uzembe katika twahara yake ya kisheria.

Marejeo

الإلمام بشرح عمدة الأحكام لإسماعيل الأنصاري، ط1، دار الفكر، دمشق، 1381هـ تيسير العلام شرح عمدة الأحكام للبسام، حققه وعلق عليه وخرج أحاديثه وصنع فهارسه: محمد صبحي بن حسن حلاق، ط10، مكتبة الصحابة، الإمارات - مكتبة التابعين، القاهرة، 1426 هـ تنبيه الأفهام شرح عمدة لأحكام لابن عثيمين، ط1، مكتبة الصحابة، الإمارات، 1426هـ عمدة الأحكام من كلام خير الأنام صلى الله عليه وسلم لعبد الغني المقدسي، دراسة وتحقيق: محمود الأرناؤوط، مراجعة وتقديم: عبد القادر الأرناؤوط، ط2، دار الثقافة العربية، دمشق، بيروت، مؤسسة قرطبة، 1408 هـ. صحيح البخاري، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر، ط1، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ. صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، 1423 هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قال: أَخْبَرَنِي عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ: أَنَّ رَجُلًا تَوَضَّأَ فَتَرَكَ مَوْضِعَ ظُفُرٍ عَلَى قَدَمِهِ فَأَبْصَرَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: «ارْجِعْ فَأَحْسِنْ وُضُوءَكَ» فَرَجَعَ، ثُمَّ صَلَّى.
Kutoka kwa Jabiri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amenieleza Omari Bin Khattwab: Yakwamba mtu mmoja alitawadha, akaacha sehemu ndogo saizi ya kucha miguuni kwake, akaiona Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akasema: "Rudi katawadhe vizuri udhu wako" Akarudi, kisha akaswali.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaNi sahihi kwa ushahidi wake mbalimbali
Maelezo

Ameeleza Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuona mtu mmoja kamaliza kutia udhu wake, akaacha kiasi cha kucha moja katika kisigino chake, hakikupatwa na maji ya udhu, akasema kumwambia huku akiashiria sehemu palipo na mapungufu: Rudi katie vizuri udhu wako, na utimize na ukipe kila kiungo haki yake katika maji, yule bwana akarudi akatimiza udhu wake kisha akaswali.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kufanya haraka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kumuelekeza asiyejua na aliyeghafilika, na hasa hasa uovu ukiwa unaambatana na kuharibika kwa ibada yake.
  2. Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vya udhu, nakuwa mwenye kuacha sehemu ya kiungo -hata kama ni kidogo- udhu wake hautasihi, na itamlazimu kurudia ikiwa umepita muda mrefu tangu kumaliza udhu wake.
  3. Sheria ya kupendezesha udhu, na hii ni kwa kuutimiza na kueneza vizuri kwa namna iliyoamrishwa kisheria.
  4. Miguu miwili ni katika viungo vya udhu, na haitoshi kuifuta, bali ni lazima kuiosha.
  5. Ni lazima kufuatanisha baina ya viungo vya udhu, kiasi kwamba aoshe kila kiungo kabla hakijakauka kilicho kabla yake.
  6. Kutojua na kusahau havidondoshi wajibu, bali vinadondosha dhambi, huyu bwana ambaye hakutimiza udhu wake kwa sababu ya kutojua kwake, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakumdondoshea uwajibu, ambao ni udhu, bali alimuamrisha kurudia.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 215) (243). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 247). شرح سنن أبي داود، لعبد المحسن العباد (29/ 13 بترقيم الشاملة آليا).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com