Ameeleza Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimuona mtu mmoja kamaliza kutia udhu wake, akaacha kiasi cha kucha moja katika kisigino chake, hakikupatwa na maji ya udhu, akasema kumwambia huku akiashiria sehemu palipo na mapungufu: Rudi katie vizuri udhu wako, na utimize na ukipe kila kiungo haki yake katika maji, yule bwana akarudi akatimiza udhu wake kisha akaswali.
- Uwajibu wa kufanya haraka kuamrisha mema na kukataza maovu, na kumuelekeza asiyejua na aliyeghafilika, na hasa hasa uovu ukiwa unaambatana na kuharibika kwa ibada yake.
- Ulazima wa kueneza maji katika viungo vyote vya udhu, nakuwa mwenye kuacha sehemu ya kiungo -hata kama ni kidogo- udhu wake hautasihi, na itamlazimu kurudia ikiwa umepita muda mrefu tangu kumaliza udhu wake.
- Sheria ya kupendezesha udhu, na hii ni kwa kuutimiza na kueneza vizuri kwa namna iliyoamrishwa kisheria.
- Miguu miwili ni katika viungo vya udhu, na haitoshi kuifuta, bali ni lazima kuiosha.
- Ni lazima kufuatanisha baina ya viungo vya udhu, kiasi kwamba aoshe kila kiungo kabla hakijakauka kilicho kabla yake.
- Kutojua na kusahau havidondoshi wajibu, bali vinadondosha dhambi, huyu bwana ambaye hakutimiza udhu wake kwa sababu ya kutojua kwake, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- hakumdondoshea uwajibu, ambao ni udhu, bali alimuamrisha kurudia.
صحيح مسلم (1/ 215) (243). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 247). شرح سنن أبي داود، لعبد المحسن العباد (29/ 13 بترقيم الشاملة آليا).