عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «إِذَا لَبِسْتُم، وَإِذَا تَوَضَّأتُم، فَابْدَأُوا بَأَيَامِنُكُم».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".
Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Imetilia mkazo hadithi ya Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake swala la kuanza na kulia katika mambo mazuri, ikapokelewa kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtakapo vaa" Yaani mkitaka kuvaa. "Na mtakapo tawadha" Yaani mkitaka kufanya. "Anzeni na kuliani kwenu" ni wingi wa kulia nacho ni kinyume cha kushoto, aingize upande wa kulia wa kanzu, kabla ya kushoto na atangulize kulia katika mikono yake na miguu yake katika udhu, kisha tambua kuwa katika viungo vya udhu vipo ambavyo si sunna kuanza na kulia, navyo ni masikio mawili na viganja viwili na mashavu mawili, bali husafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa litakuwa gumu hilo kama ilivyo kwa aliyekatwa mkono na mfano wake atatanguliza kulia.
Marejeo
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي، ط1، دار ابن الجوزي، الدمام، 1415هـ.
تطريز رياض الصالحين، للشيخ فيصل المبارك، ط1، تحقيق: عبد العزيز بن عبد الله آل حمد، دار العاصمة، الرياض، 1423هـ.
جامع الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر وآخرون، ط2، شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي ، مصر، 1395هـ.
دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين لمحمد علي بن محمد بن علان، ط4، اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة، بيروت، 1425هـ.
رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ.
رياض الصالحين، ط4، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، 1428هـ.
سنن أبي داود ،تحقيق: محمد محيي الدين عبد الحميد، المكتبة العصرية، بيروت.
سنن ابن ماجه، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء الكتب العربية، فيصل عيسى البابي الحلبي.
الشرح الممتع على زاد المستقنع، لمحمد بن صالح بن محمد العثيمين، ط1، دار ابن الجوزي، 1422 - 1428هـ.
كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين برئاسة حمد بن ناصر العمار، ط1، كنوز إشبيليا، الرياض، 1430هـ.
مسند الإمام أحمد بن حنبل، تحقيق: شعيب الأرنؤوط و عادل مرشد، وآخرون، تحت إشراف: د عبد الله بن عبد المحسن التركي، ط1، مؤسسة الرسالة، 1421هـ.
مشكاة المصابيح للتبريزي، تحقيق: محمد ناصر الدين الألباني، ط3، المكتب الإسلامي، بيروت، 1985م.
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي، ط2، دار إحياء التراث العربي - بيروت، 1392هـ.
شرح رياض الصالحين، للشيخ ابن عثيمين، دار الوطن للنشر، الرياض، 1426هـ.
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عائشة رضي الله عنها ، قالت: كُنَّا نُعِدُّ لرسول الله صلى الله عليه وسلم سِوَاكَهُ وَطَهُورَهُ، فَيَبْعَثُهُ الله ما شاء أن يَبْعَثَهُ من الليل، فَيَتَسَوَّكُ، ويتوضَّأ ويُصلي.
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali
Imepokelewa na Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa yeye alikuwa akimuandalia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake, na maji ambayo atayatumia kutawadha usiku, kisha anamuamsha Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka nyakati za usiku, wakati wowote usiku, anapoamka tu anaanza kusugua meno yake kwa mswaki; ili aondoe harufu ya mdomo ambayo hutokea mara nyingi kwasababu ya kulala, kisha anatawadha udhu wake wa swala, kisha anaswali swala za usiku.
Marejeo
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، سليم بن عيد الهلالي، دار ابن الجوزي، الدمام، الطبعة: الأولى 1415هـ.
رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين، أبو زكريا محيي الدين النووي، تحقيق ماهر الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، الطبعة: الأولى 1428هـ.
صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، الطبعة: 1423 هـ.
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين، مؤسسة الرسالة، بيروت، الطبعة: الرابعة عشر 1407هـ.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ لَقِيطِ بْنِ صَبِرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كُنْتُ وَافِدَ بَنِي الْمُنْتَفِقِ -أَوْ فِي وَفْدِ بَنِي الْمُنْتَفِقِ- إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: فَلَمَّا قَدِمْنَا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمْ نُصَادِفْهُ فِي مَنْزِلِهِ، وَصَادَفْنَا عَائِشَةَ أُمَّ الْمُؤْمِنِينَ، قَالَ: فَأَمَرَتْ لَنَا بِخَزِيرَةٍ، فَصُنِعَتْ لَنَا، قَالَ: وَأُتِينَا بِقِنَاعٍ -وَالْقِنَاعُ: الطَّبَقُ فِيهِ تَمْرٌ- ثُمَّ جَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «هَلْ أَصَبْتُمْ شَيْئًا؟ أَوْ أُمِرَ لَكُمْ بِشَيْءٍ؟» قَالَ: قُلْنَا: نَعَمْ، يَا رَسُولَ اللَّهِ، قَالَ: فَبَيْنَا نَحْنُ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جُلُوسٌ، إِذْ دَفَعَ الرَّاعِي غَنَمَهُ إِلَى الْمُرَاحِ، وَمَعَهُ سَخْلَةٌ تَيْعَرُ، فَقَالَ: «مَا وَلَّدْتَ يَا فُلَانُ؟»، قَالَ: بَهْمَةً، قَالَ: «فَاذْبَحْ لَنَا مَكَانَهَا شَاةً»، ثُمَّ قَالَ: «لَا تَحْسِبَنَّ» وَلَمْ يَقُلْ: لَا تَحْسَبَنَّ «أَنَّا مِنْ أَجْلِكَ ذَبَحْنَاهَا، لَنَا غَنَمٌ مِائَةٌ لَا نُرِيدُ أَنْ تَزِيدَ، فَإِذَا وَلَّدَ الرَّاعِي بَهْمَةً، ذَبَحْنَا مَكَانَهَا شَاةً» قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ لِي امْرَأَةً وَإِنَّ فِي لِسَانِهَا شَيْئًا -يَعْنِي الْبَذَاءَ- قَالَ: «فَطَلِّقْهَا إِذن»، قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنَّ لَهَا صُحْبَةً، وَلِي مِنْهَا وَلَدٌ، قَالَ: «فَمُرْهَا» يَقُولُ: عِظْهَا، «فَإِنْ يَكُ فِيهَا خَيْرٌ فَسَتَفْعَلْ، وَلَا تَضْرِبْ ظَعِينَتَكَ كَضَرْبِكَ أُمَيَّتَكَ» فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَخْبِرْنِي عَنِ الْوُضُوءِ، قَالَ: «أَسْبِغِ الْوُضُوءَ، وَخَلِّلْ بَيْنَ الْأَصَابِعِ، وَبَالِغْ فِي الِاسْتِنْشَاقِ إِلَّا أَنْ تَكُونَ صَائِمًا».
Kutoka kwa Lakitwu bin Swabira -radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilikuwa na msafara wa bani Muntafiq -au katika msafara wa bani Muntafiq- kwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, anasema: Tulipofika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hatukumkuta nyumbani kwake, na tukakutana na Aisha Mama wa Waumini, anasema: Akaamrisha tupikiwe mkate, basi tukapikiwa, anasema: Na tukaletewa Kinai -na kinai ni bakuli lenye tende- kisha akaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: "Je, mmepata chochote? Au mmeagiziwa chochote?" Anasema: Tukasema: Ndiyo, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, anasema: Wakati tukiendelea kukaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mara tukaona mchungaji akiwaswaga mbuzi wake kuingia zizini, akiwa na kitoto cha mbuzi kikilia, akasema: "Imezaa kitoto gani ewe fulani?" Akasema: Cha kike, akasema: "Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine" Kisha akasema: "Usidhanie kuwa, sisi tumemchinja mbuzi huyo kwa ajili yako, sisi tuna mbuzi mia moja hatutaki zizidi hapo, akizalisha mchungaji kitoto cha mbuzi basi tunachinja badala yake mbuzi mwingine" Anasema: Nikasema: Ewe Mjume wa Mwenyezi Mungu hakika mimi nina mwanamke katika ulimi wake kuna kitu -yaani ana maneno machafu- akasema: "Basi mpe talaka" Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika ana ujamaa na mimi na nimezaa naye watoto. Akasema: "Muamrishe" Anasema: Mpe nasaha. "Endapo atakuwa na chembe ya kheri basi atatekeleza unachomwambia, na wala usimpige mkeo kama unavyopiga mtumwa wako" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu? Akasema: "Eneza maji ya udhu, na uachanishe kati ya vidole, na pandisha maji yafike puani, isipokuwa utakapokuwa umefunga".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Laqitwu bin Swabira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba yeye alifika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja na watu wengine kutoka katika jamii yake ya Bani Muntafiq, anasema: Hatukumkuta nyumbani kwake, na tukamkuta Mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akaamrisha tuandaliwe mkate wa ngano na samli, na tukaletewa bakuli la tende. Kisha akaja rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Je, mmeletewa chochote katika chakula? Tukasema: Ndiyo, anasema Laqitwu: Wakati tukiwa bado tumekaa naye rehema na amani ziwe juu yake, ghafla akaja mchungaji wa mbuzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwaswaga kwenda katika zizi lake, huku akiwa kabeba kitoto cha mbuzi kikipiga kelele, akasema: Umezalisha nini? Akasema: Jike. Akasema: Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine mkubwa, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Usidhanie kuwa sisi kwa ajili yenu tumejikalifisha na tukamchinja, bali sisi tuna mbuzi idadi yake ni mia moja, na wala hatutaki wazidi katika idadi hii, akizaliwa mbuzi mpya tunachinja badala yake mbuzi mwingine, akasema Laqitwu: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mke wangu ulimi wake ni mrefu na ana maneno machafu, nifanye nini kwake? Akasema: Basi mpe talaka. Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika nimeishi naye muda mrefu sana, na nimezaa naye. Akasema: Basi mpe nasaha, ikiwa ndani ya moyo wake kutakuwa na kheri atazifanyia kazi nasaha zako, na ikiwa hatobadilika, basi mpige kipigo kisichojeruhi, na wala usimpige kama unavyompiga mtumwa wako. Kisha akasema Laqitwu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu. Akasema: Fikisha maji ya Udhu mahala pake, na ukipe kila kiungo haki yake, na wala usiache kitu katika faradhi zake na sunna zake, na achanisha vidole vya mikono yako na miguu yako wakati wa kuviosha, na upitilize katika kuyavuta maji ndani ya pua yako wakati wa udhu na kuyatoa kwake, isipokuwa ikiwa ulitia nia ya swaumu ili maji yasiingie tumboni mwako.
Mafunzo
- Sheria ya kumkirimu mgeni.
- Kufikisha maji kuna aina mbili: 1- Kufikisha kwa wajibu, nako ni kule ambako udhu hautimii bila kufanya hivyo, na makusudio yake ni kuosha mahala stahiki na kupaeneza. 2- Kufikisha kwa sunna, nako ni kule ambako udhu unaweza kutimia bila kuosha, na makusudio yake ni kile kilichozidi katika wajibu, kama kurudia kuosha mara ya pili na ya tatu, hii ni sunna.
- Sunna ya kutawanya vidole vya mikono na miguu miwili wakati wa kuviosha, na kuvitawanya kwake ni kuacha maji yavifikie.
- Amesema Twayibi: Bali hapa alijibu Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya sunna za udhu; kwa sababu muulizaji alikuwa anajua msingi wa udhu.
- Na miongoni mwa mambo yake mazuri Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kujali hisia za watu wengine, na kulinda saikolojia zao.
- Hadithi ni dalili ya uwajibu wa kusukutua katika udhu.
- Hadithi ni dalili ya sunna ya kupita kiasi katika kupandisha maji puani, isipokuwa kwa mfungaji, kwake si sunna; ili kupitiliza huku kusipelekee kuingia maji kooni kupitia puani, yakaharibu swaumu.
- Hapa kuna ushahidi kuwa si wajibu kuhama kwa kila aliyesilimu; kwa sababu Banil-Muntafiq na wengineo hawakuhama, bali walituma misafara yao, na hili liko hivyo, ikiwa mtu yuko katika mazingira ambayo anaweza kudhihirisha ndani yake dini.
Marejeo
سنن أبي داود (1/ 99) (142).
سنن الترمذي (2/ 146) (788).
سنن النسائي (1/ 66) (87).
سنن ابن ماجه (1/ 262) (407).
توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (1/ 217).
سُبل السلام، للصنعاني (1/ 66 ).
فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 183).
منحة العلَّام، لعبد الله الفوزان (1/ 174).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَغْسِلُ، أَوْ كَانَ يَغْتَسِلُ، بِالصَّاعِ إِلَى خَمْسَةِ أَمْدَادٍ، وَيَتَوَضَّأُ بِالْمُدِّ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiosha, au akioga, kwa kibaba kimoja mpaka vibaba vitano, na anatawadha kwa kibaba kimoja.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga janaba kwa kibaba kimoja mpaka vitano, na alikuwa akitawadha kwa kibaba kimoja. Na kibaba ujazo wake ni: mud nne, na mud moja ni: kiasi cha kujaza kiganja cha mtu mwenye mwili wa wastani.
Mafunzo
- Sheria ya kufanya bajeti katika maji ya udhu na kuoga, na kutofanya fujo, hata kama maji yatakuwa mengi na rahisi kupatikana.
- Sunna ya kupunguza maji wakati wa udhu na kuoga, kulingana na uhitaji, nakuwa huu ndio muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Lengo ni kueneza maji katika udhu na kuoga ikiwa ni pamoja na kuchunga sunna na adabu pasina kufanya fujo wala ubahili, na muda uzingatiwe pia na wingi wa maji na uchache wake na mengineyo.
- Janaba huitwa kwa kila aliyeshusha manii au kafanya tendo la ndoa, na limeitwa hivyo kwa sababu ya mwenye janaba kujiweka mbali na swala na ibada zingine mpaka awe msafi.
- Kibaba ni: Kipimo maarufu, na makusudio yake ni kibaba cha Mtume, na kinafikia uzito wake gram (480) za ngano safi, na kwa lita ni lita tatu (3)
- Mud: Ni ni kilo moja kisheria, nayo ni ujazo wa viganja viwili vya mtu mzima atakapovijaza na akanyoosha mikono yake, na Mud ni nusu ya kibaba, kwa itifaki ya wanachuoni wote, na kiwango chake ni mil (750).
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 51) (201).
صحيح مسلم (1/ 258) (325).
توضيح الأحكام، للبسام (1/ 250).
سُبل السلام، للصنعاني (1/ 79 ).
فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (1/ 212).
منحة العلَّام، لعبد الله الفوزان (1/ 186).
منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة قاسم (1/ 272).
تحقيق مقدار المد والصاع النبوي، للدكتور عبدالمحسن القاسم
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضي الله عنه قَالَ: كَانَتْ عَلَيْنَا رِعَايَةُ الْإِبِلِ فَجَاءَتْ نَوْبَتِي فَرَوَّحْتُهَا بِعَشِيٍّ فَأَدْرَكْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمًا يُحَدِّثُ النَّاسَ فَأَدْرَكْتُ مِنْ قَوْلِهِ: «مَا مِنْ مُسْلِمٍ يَتَوَضَّأُ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهُ، ثُمَّ يَقُومُ فَيُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ، مُقْبِلٌ عَلَيْهِمَا بِقَلْبِهِ وَوَجْهِهِ، إِلَّا وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ» قَالَ فَقُلْتُ: مَا أَجْوَدَ هَذِهِ، فَإِذَا قَائِلٌ بَيْنَ يَدَيَّ يَقُولُ: الَّتِي قَبْلَهَا أَجْوَدُ، فَنَظَرْتُ فَإِذَا عُمَرُ قَالَ: إِنِّي قَدْ رَأَيْتُكَ جِئْتَ آنِفًا، قَالَ: «مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ فَيُبْلِغُ - أَوْ فَيُسْبِغُ - الْوَضُوءَ ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ».
Kutoka kwa Uqba bin Amir, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, amesema: “Tulikuwa na zamu ya kuchunga ngamia, basi ikafika zamu yangu nikawapeleka jioni, nikamkuta Mtume rehema na amni ziwe juu yake akiwa amesimama akiwahadithia watu, nikamkuta akiwa katika kauli yake: “Hakuna Muislamu anayetawadha na akautia vizuri udhu wake, kisha akasimama na kuswali rakaa mbili, akielekea kwa moyo wake na uso wake ndani ya rakaa hizo, isipokuwa Pepo itastahiki kwake.” Akasema, nikasema: Ni kheri iliyoje hii, mara ghafla nikasikia msemaji mmoja mbele yangu akisema: Ile ya kabla yake ndio ilikuwa bora, basi nikatazama, mara nikamuona ni Omari, akasema: Nimekuona umekuja hivi karibuni, akasema: “Hakuna yeyote kati yenu atakayetawadha vizuri - au akaukamilisha vizuri- kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Pepo, aingie mlango wowote autakao".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati akiwaeleza watu fadhila mbili kubwa:
Ya kwanza: Mwenye kutawadha vizuri, akaupendezesha vizuri udhu, na akaukamilisha, na akaukamilisha katika namna ilivyoelekezwa, na akakipa kila kiungo haki yake katika maji, kisha akasema: Nashuhudia ya kwamba hakuna mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake; Isipokuwa atafunguliwa milango minane ya Peponi, aingie mlango autakao.
Pili: Mwenye kutawadha udhu huu kamili, kisha akasimama baada ya udhuu huu na kuswali rakaa mbili; Akiwa ameelekea ndani ya swala kwa moyo wake, kwa ikhlaswi na utulivu, na akanyenyekeza uso wake na viungo vyote vya mwili wake kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa Pepo itakuwa ni wajibu kwake.
Mafunzo
- Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kumpa malipo makubwa kwa amali ndogo.
- Sheria ya kueneza maji ya udhu na kutawadha kwa ukamilifu, na kuswali rakaa mbili kwa unyenyekevu baada yake, na malipo makubwa yanayopatikana kwayo.
- Kueneza maji ya udhu, na kuleta dua hii baada yake, ni katika sababu za kuingia peponi.
- Sunna ya kusema dhikiri hii kwa mwenye kuoga pia.
- Maswahaba walikuwa na shauku ya kufanya mema, kama vile kujifunza na kusambaza elimu, na ushirikiano wao katika kufanya hivyo na katika masuala ya riziki zao.
- Dhikri baada ya kutawadha huutakasa moyo na kuusafisha na ushirikina, kama vile udhuu unavyousafisha mwili na kuuondoa uchafu.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 209) (234).
توضيح الأحكام، للبسام (1/ 251).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (3/ 120).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: تَوَضَّأَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَرَّةً مَرَّةً.
Imepokewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alitawadha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mara moja moja.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara moja moja, anaosha uso pamoja kusukutua na kupandisha maji puani, na mikono miwili na miguu miwili mara moja moja, na hiki ndicho kiwango cha wajibu.
Mafunzo
- Kilicho wajibu katika kuosha viungo ni mara moja moja, inayozidi inapendeza kufanya hivyo.
- Sheria ya kutia udhu mara moja moja katika baadhi ya nyakati.
- Sheria katika kufuta kichwa ni mara moja.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 43) (157)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 244).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ زَيْدٍ رضي الله عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ تَوَضَّأَ مَرَّتَيْنِ مَرَّتَيْنِ.
Kutoka kwa Abdallah bin Zubairi -Radhi za Allah ziwe juu yake-: Anasimulia kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alitawadha mara mbili mbili.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika baadhi ya nyakati zake anapotawadha anaosha kila kiungo katika viungo vya udhu mara mbili, anaosha uso ikiwemo kusukutua na kupandisha maji puani na mikono miwili na miguu miwili mara mbili.
Mafunzo
- Kilicho wajibu katika kuosha viungo ni mara moja moja na kinachozidi inapendeza.
- Sheria ya kutia udhu mara mbili mbili katika baadhi ya nyakati.
- Sheria katika kufuta kichwa ni mara moja.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 43) (158)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 244).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ سَفِينَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُغَسِّلُهُ الصَّاعُ مِنَ المَاءِ مِنَ الجَنَابَةِ، وَيُوَضِّئُهُ المُدُّ.
Kutoka kwa Safina radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga kutokana na janaba kwa kiasi cha kibaba, na akitawadha kwa ujazo wa kiganja, na kibaba: Ni ujazo wa viganja vinne, na kiganja: Ni kiasi cha ujazo wa viganja viwili vya mtu wa maumbile ya kati na kati.
Mafunzo
- Sheria ya kubajeti maji ya udhu na ya kuoga, na kutofanya ubadhirifu hata kama maji ni mengi.
- Kupendeza kutumia kidogo katika maji ya udhu na ya kuoga kulingana na haja, na kwamba huu ndio muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- lengo ni kueneza maji katika udhu na kuoga ikiwa ni pamoja na kuzingatia sunna na adabu, pasina kufanya ubadhirifu wala kupunja sana, na azingatie muda na wingi wa maji na uchache wake na mengineyo.
- Huitwa janaba kwa kila aliyeshusha manii au aliyefanya tendo la ndoa, na limeitwa hivyo kwa sababu mtu hujitenga na swala na ibada mbali mbali mpaka asafishike.
- Kibaba: Ni kipimo maarufu, na hukusudiwa kibaba cha Mtume, na kinafikia ujazo wake (480 g) za ujazo wa ngano safi, na kwa lita ni Lita (3).
- Mudd (kiganja): Ni moja kati ya vipimo vya kisheria, nacho ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati atakapovijaza na kunyoosha mkono wake, na kiganga kimoja ni robo kibaba, kwa itifaki ya wanachuoni, na kiasi chake ni (ml 750).
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 258) (326).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (8/ 52).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com