Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja

عَنْ سَفِينَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُغَسِّلُهُ الصَّاعُ مِنَ المَاءِ مِنَ الجَنَابَةِ، وَيُوَضِّئُهُ المُدُّ.
Kutoka kwa Safina radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kikimuosha kibaba cha maji kutokana na janaba, na ukimtia udhu ujazo wa kiganja.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akioga kutokana na janaba kwa kiasi cha kibaba, na akitawadha kwa ujazo wa kiganja, na kibaba: Ni ujazo wa viganja vinne, na kiganja: Ni kiasi cha ujazo wa viganja viwili vya mtu wa maumbile ya kati na kati.

Mafunzo
  1. Sheria ya kubajeti maji ya udhu na ya kuoga, na kutofanya ubadhirifu hata kama maji ni mengi.
  2. Kupendeza kutumia kidogo katika maji ya udhu na ya kuoga kulingana na haja, na kwamba huu ndio muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. lengo ni kueneza maji katika udhu na kuoga ikiwa ni pamoja na kuzingatia sunna na adabu, pasina kufanya ubadhirifu wala kupunja sana, na azingatie muda na wingi wa maji na uchache wake na mengineyo.
  4. Huitwa janaba kwa kila aliyeshusha manii au aliyefanya tendo la ndoa, na limeitwa hivyo kwa sababu mtu hujitenga na swala na ibada mbali mbali mpaka asafishike.
  5. Kibaba: Ni kipimo maarufu, na hukusudiwa kibaba cha Mtume, na kinafikia ujazo wake (480 g) za ujazo wa ngano safi, na kwa lita ni Lita (3).
  6. Mudd (kiganja): Ni moja kati ya vipimo vya kisheria, nacho ni ujazo wa viganja viwili vya mtu wa kati na kati atakapovijaza na kunyoosha mkono wake, na kiganga kimoja ni robo kibaba, kwa itifaki ya wanachuoni, na kiasi chake ni (ml 750).
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 258) (326). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (8/ 52).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Sunna na Adabu za Kutawadha

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com