Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Fadhila - ubora wa kutawadha.

Hadithi 5

Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «يَعْقِدُ الشَّيْطَانُ عَلَى قَافِيَةِ رَأْسِ أَحَدِكُمْ إِذَا هُوَ نَامَ ثَلاَثَ عُقَدٍ يَضْرِبُ كُلَّ عُقْدَةٍ عَلَيْكَ لَيْلٌ طَوِيلٌ، فَارْقُدْ، فَإِنِ اسْتَيْقَظَ فَذَكَرَ اللَّهَ، انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ تَوَضَّأَ انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَإِنْ صَلَّى انْحَلَّتْ عُقْدَةٌ، فَأَصْبَحَ نَشِيطًا طَيِّبَ النَّفْسِ، وَإِلَّا أَصْبَحَ خَبِيثَ النَّفْسِ كَسْلاَنَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala, pindi anapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu linafunguka fundo moja, akitawadha, linafunguka fundo jingine, na akiswali, yanafunguka mafundo yake yote, anaamka akiwa na uchangamfu na moyo mkunjufu, na vinginevyo basi anaamka akiwa na nafsi chafu tena mvivu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake hali ya shetani na mapambano yake na mwanadam anayetaka kusimama kwa ajili ya swala ya usiku au Alfajiri. Muumini anapokwenda kulala shetani hufunga katika kisogo chake -yaani mwisho wa kichwa chake- mafundo matatu. Muumini atakapoamka na akamtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na akawa hajatii wasi wasi wa shetani; fundo moja hufunguka. Akitawadha linafunguka fundo jingine. Na ikiwa atasimama akaswali yatafunguka mafundo yote matatu, na atakuwa na uchangamfu wa nafsi; na kufurahi kwake kwa yale aliyoafikishwa na Mwenyezi Mungu katika ibada, akijipa bishara kwa yale aliyoahidiwa na Mwenyezi Mungu katika thawabu na msamaha, ikiwa ni pamoja na hivyo vilivyomuondokea katika mafundo ya shetani na vikwazo vyake, na asipofanya hivyo atakuwa na nafsi chafu, atakuwa na moyo wenye huzuni, mvivu katika mambo ya kheri na mambo mema; kwa sababu atakuwa kafungwa kwa pingu za shetani, na atakuwa kawekwa mbali na kumkaribia Rahmani (Mwingi wa rehema).

Mafunzo
  1. Shetani siku zote anakwenda mbio katika njia zote za mwanadam; ili azuie kati yake na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mja hawezi kusalimika na shetani isipokuwa kwa kutaka msaada kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa kuchukua sababu za kinga na ulinzi.
  2. Kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu kunaleta uchangamfu katika nafsi na kunakunjua kifua, na hufukuza uvivu na kupoa, na huondoa matatizo na hasira; kwa sababu humfukuza shetani, na hili ni katika wasi wasi wake.
  3. Muumini hufurahishwa na taufiki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutekeleza ibada zake, na anasononeka kwa uzembe wake katika kupunguza daraja za fadhila na ukamilifu.
  4. Kujisahahu na kukaa katika maasi ni katika matendo ya shetani na kupambia kwake.
  5. Mambo haya matatu -Kumtaja Mwenyezi Mungu, na udhu, na swala- humfukuza shetani.
  6. Shetani kufunga mwisho wa kichwa pekee; ni kwa sababu ndio kituo cha nguvu, na ndio sehemu ya kutolea maamuzi, akifunga mahali hapo huweza kuitawala roho ya mwanadam, na kumtia usingizi.
  7. Amesema Imam bin Hajari Al-Asqalaani: Umetajwa usiku katika kauli yake: "Tumia usiku huu" Inaonyesha hili ni maalumu kwa usingizi wa usiku.
  8. Amesema bin Hajar Al-Asqalani: Hakuna dhikri makhsusi ambayo haitoshelezi nyingine, bali kila kinachofaa kuitwa dhikri kinatosheleza, na inaingia ndani yake kusoma Qur'ani, kusoma hadithi za Mtume, na kujishughulisha na kusoma elimu ya Kisheria, na jambo bora zaidi lililotajwa ni kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Atakayeshituka usiku kutoka usingizini akasema: "Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, yeye pekee asiye na mshirika, ufalme ni wake na sifa njema ni zake, naye juu ya kila kitu ni muweza, kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu, na ametakasika Mwenyezi Mungu, na hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu Mkubwa, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha akasema: Ewe Mola wangu, nisamehe, au akiomba dua yake itaitikiwa, na akitawadha utakubaliwa udhu wake" Kaipokea Bukhari.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 52) (1142). صحيح مسلم (1/ 538) (776). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 328). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 834). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (15/ 305). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لأحمد العسقلاني (10/ 564). طرح التثريب في شرح التقريب، العراقي (3/ 82).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake

عن عثمان بن عفان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ خَرَجَتْ خَطَايَاهُ مِنْ جَسَدِهِ حَتَّى تَخْرُجَ مِنْ تَحْتِ أَظْفَارِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetawadha kwa kuchunga sunna za udhu na adabu zake, hilo litakuwa katika sababu za kusamehewa makosa na kufuta madhambi, "Mpaka yatoke" madhambi yake kutoka chini ya kucha za mikono yake na miguu yake.

Mafunzo
  1. Himizo la kutilia umuhimu wa kujifunza udhu na sunna zake na adabu zake, na kuzifanyia kazi.
  2. Ubora wa udhu, nakuwa hilo ni kafara ya madhambi madogo, ama makubwa ni lazima kufanya toba.
  3. Sharti za kutoka kwa madhambi ni kuukamilisha udhu na kuuleta bila mapungufu kama alivyobainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  4. Kufutwa kwa madhambi katika hadithi hii kumefungamanishwa na kuyaepuka madhambi makubwa na kuyaombea toba, amesema Mtukufu: "Ikiwa mtayaepuka madhambi makubwa mnayokatazwa tutakusameheni makosa yenu" [An-Nisaa: 31].
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 216) (245). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 9). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 763). بهجة الناظرين، سليم الهلالي (2/ 247).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi

عن أبي مالكٍ الأشعريِّ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَآنِ -أَوْ تَمْلَأُ- مَا بَيْنَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا».
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye kuwa na msimamo na kumtii Mwenyezi Mungu, na akawa ni mwenye kuikomboa nafsi yake kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anafahamisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa twahara na usafi wa nje ambao ni udhu na kuoga ni sharti la usahihi wa swala. Na kuwa neno: "Alhamdulillah hujaza mizani" nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu, na kumsifia kwa sifa za ukamilifu zitakazopimwa siku ya kiyama na kuijaza mizani ya matendo. Na kuwa neno: "Sub-hanallah na Alhamdulillah" na maneno hayo ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifia kwa sifa zilizokamilika na zilizotimia ambazo anastahiki sifa hizo pamoja kumpenda yeye na kumtukuza hujaza sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi. Na kuwa "Swala ni nuru" ya mja katika moyo wake, na katika uso wake na kaburini mwake na siku ya kufufuliwa kwake. Na kuwa "Sadaka ni ushahidi" Na ni dalili ya ukweli wa imani ya muumini, na tofauti yake na mnafiki ambaye huzuia kutoa sadaka kwa kuwa mnafiki haamini malipo ya kutoa sadaka. Na "kuwa subira ni mwangaza" -na subira ni kuizuia nafsi kutoku papatika na kuwa na hasira, subira ni nuru inayokuwa na joto na kuunguza, kama vile mwanga wa Jua; kwa sababu subira ni tabu kubwa inahitaji kuilazimisha nafsi na kuizuia na kile inachokipenda; hivyo haachi kuwa na mng'ao mtu mwenye subira, mwenye kuongoka na mwenye kudumu katika usahihi, nako ni kusubiri katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kutomuasi yeye, na kuwa na subira kwenye matatizo na aina mbalimbali za mambo yenye kuchukiza katika Dunia. Na kuwa "Qur'ani ni hoja kwako wewe" kwa kuisoma na kuifanyia kazi, au yaweza kuwa " Hoja dhidi yako" kwa kuiacha pasina kuifanyia kazi au kuisoma. Kisha akafahamisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa watu wote huenda mbio na hutawanyika na huamka toka usingizini mwao na wanatoka kwenye majumba yao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali miongoni mwao kuna wenyekuwa na msimamo katika kumtii Mwenyezi Mungu, hivyo anakuwa ameikomboa nafsi yake na moto, na miongoni mwao kuna mwenye kwenda kinyume na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu na akaingia katika maasi, hivyo akaiangamiza na kuingia motoni.

Mafunzo
  1. Twahara zipo aina mbili: Twahara ya nje nayo ni udhu na kuoga, na twahara ya ndani inakuwa kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kuwa na imani na matendo mazuri.
  2. umuhimu wa kuzihifadhi swala tano, kwakuwa swala tano ni mwangaza kwa mja hapa Duniani na siku ya Kiyama.
  3. Kutoa sadaka ni dalili ya imani ya kweli.
  4. Umuhimu wa kuifanyia kazi Qur'ani na kuisadikisha ili iwe ni hoja kwako au dhidi yako.
  5. Ikiwa nafsi hutoishughulisha na utiifu itakushughulisha na maasi.
  6. Kila mwanadamu lazima afanye matendo, hivyo ima aikomboe nafsi yake kwa kutii, au aiangamize kwa kufanya maasi.
  7. Na subira inahitaji uvumilivu na kutarajia thawabu, na ndani yake kuna uzito.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 203) (223)، شرح الأربعين لابن دقيق العيد (ص 84)، شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 231)، الرياض الزكية شرح الأربعين النووية للخضير (ص 293)، فتح القوي المتين في شرح الأربعين للعباد (ص 79)

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala

عن عَمْرُو بْنُ عَامِرٍ عَنْ ‌أَنَس بن مالك قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَتَوَضَّأُ عِنْدَ كُلِّ صَلَاةٍ، قُلْتُ: كَيْفَ كُنْتُمْ تَصْنَعُونَ؟ قَالَ: يُجْزِئُ أَحَدَنَا الْوُضُوءُ مَا لَمْ يُحْدِثْ.
Kutoka kwa Amri bin Aamiri kutoka kwa Anasi amesema: Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kila wakati wa swala, nikasema: Nyinyi mlikuwa mnafanya vipi? Akasema: Ulikuwa ukimtosha mmoja wetu udhu mmoja madam hajatengukwa.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitawadha kwa kila swala ya faradhi hata kama hajatengukwa udhu; Na hii ni kwa sababu ya kupata malipo na fadhila. Na inafaa kwa mtu kuswali kwa zaidi ya swala moja kwa udhu mmoja madam bado yuko na udhu wake.

Mafunzo
  1. Mwenendo uliodumu zaidi wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kushika udhu kwa kila swala; ili kutaka ukamilifu zaidi.
  2. Sunna ya kushika udhu kila wakati wa swala.
  3. Inafaa kutekeleza zaidi ya swala moja kwa udhu mmoja.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 53) (214)، شرح ابن بطّال (1/321)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (1/ 285).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi

عَنْ أَبِي مَالِكٍ الحَارِثِ بْنِ عَاصِمٍ الأَشْعَرِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الطُّهُورُ شَطْرُ الْإِيمَانِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَأُ الْمِيزَانَ، وَسُبْحَانَ اللهِ وَالْحَمْدُ لِلهِ تَمْلَآنِ -أَوْ تَمْلَأُ- مَا بَيْنَ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ، وَالصَّلَاةُ نُورٌ، وَالصَّدَقَةُ بُرْهَانٌ، وَالصَّبْرُ ضِيَاءٌ، وَالْقُرْآنُ حُجَّةٌ لَكَ أَوْ عَلَيْكَ، كُلُّ النَّاسِ يَغْدُو، فَبَايِعٌ نَفْسَهُ فَمُعْتِقُهَا أَوْ مُوبِقُهَا»
Imepokelea kutoka kwa Abii Maalik Al-Ash-ariy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi, na Swala ni nuru, na sadaka ni dalili ya imani, na subira ni mwangaza, na Qur'ani ni hoja kwako au hoja dhidi yako, watu wote huamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kutafuta riziki kuna mwenye huiuza nafasi yake yuko anayeikomboa kutoingia motoni, na miongoni mwao kuna mwenye kuangukia kwenye maasi na akaangamia na kuingia motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anafahamisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa twahara na usafi wa nje ambao ni udhu na kuoga ni sharti la usahihi wa swala. Na kuwa neno: "Alhamdulillah hujaza mizani" nako ni kumsifu Mwenyezi Mungu aliyetakasika na machafu, na kumsifia kwa sifa za ukamilifu zitakazopimwa siku ya kiyama na kuijaza mizani ya matendo. Na kuwa neno: "Sub-hanallah na Alhamdulillah" na maneno hayo ni kumtakasa Mwenyezi Mungu na kumsifia kwa sifa zilizokamilika na zilizotimia ambazo anastahiki sifa hizo pamoja kumpenda yeye na kumtukuza hujaza sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi. Na kuwa "Swala ni nuru" ya mja katika moyo wake, na katika uso wake na kaburini mwake na siku ya kufufuliwa kwake. Na kuwa "Sadaka ni ushahidi" Na ni dalili ya ukweli wa imani ya muumini, na tofauti yake na mnafiki ambaye huzuia kutoa sadaka kwa kuwa mnafiki haamini malipo ya kutoa sadaka. Na "kuwa subira ni mwangaza" -na subira ni kuizuia nafsi kutoku papatika na kuwa na hasira, subira ni nuru inayokuwa na joto na kuunguza, kama vile mwanga wa Jua; kwa sababu subira ni tabu kubwa inahitaji kuilazimisha nafsi na kuizuia na kile inachokipenda; hivyo haachi kuwa na mng'ao mtu mwenye subira, mwenye kuongoka na mwenye kudumu katika usahihi, nako ni kusubiri katika kumtii Mwenyezi Mungu, na kutomuasi yeye, na kuwa na subira kwenye matatizo na aina mbalimbali za mambo yenye kuchukiza katika Dunia. Na kuwa "Qur'ani ni hoja kwako wewe" kwa kuisoma na kuifanyia kazi, au yaweza kuwa " Hoja dhidi yako" kwa kuiacha pasina kuifanyia kazi au kuisoma. Kisha akafahamisha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- yakuwa watu wote huenda mbio na hutawanyika na huamka toka usingizini mwao na wanatoka kwenye majumba yao kwa ajili ya kufanya kazi mbalimbali miongoni mwao kuna wenyekuwa na msimamo katika kumtii Mwenyezi Mungu, hivyo anakuwa ameikomboa nafsi yake na moto, na miongoni mwao kuna mwenye kwenda kinyume na kuacha kumtii Mwenyezi Mungu na akaingia katika maasi, hivyo akaiangamiza na kuingia motoni.

Mafunzo
  1. Twahara zipo aina mbili: Twahara ya nje nayo ni udhu na kuoga, na twahara ya ndani inakuwa kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kuwa na imani na matendo mazuri.
  2. umuhimu wa kuzihifadhi swala tano, kwakuwa swala tano ni mwangaza kwa mja hapa Duniani na siku ya Kiyama.
  3. Kutoa sadaka ni dalili ya imani ya kweli.
  4. Umuhimu wa kuifanyia kazi Qur'ani na kuisadikisha ili iwe ni hoja kwako au dhidi yako.
  5. Ikiwa nafsi hutoishughulisha na utiifu itakushughulisha na maasi.
  6. Kila mwanadamu lazima afanye matendo, hivyo ima aikomboe nafsi yake kwa kutii, au aiangamize kwa kufanya maasi.
  7. Na subira inahitaji uvumilivu na kutarajia thawabu, na ndani yake kuna uzito.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 203) (223). شرح الأربعين لابن دقيق العيد (ص 84). شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 231). الرياض الزكية شرح الأربعين النووية للخضير (ص 293). فتح القوي المتين في شرح الأربعين للعباد (ص 79).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com