Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake

عن عثمان بن عفان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ خَرَجَتْ خَطَايَاهُ مِنْ جَسَدِهِ حَتَّى تَخْرُجَ مِنْ تَحْتِ أَظْفَارِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetawadha kwa kuchunga sunna za udhu na adabu zake, hilo litakuwa katika sababu za kusamehewa makosa na kufuta madhambi, "Mpaka yatoke" madhambi yake kutoka chini ya kucha za mikono yake na miguu yake.

Mafunzo
  1. Himizo la kutilia umuhimu wa kujifunza udhu na sunna zake na adabu zake, na kuzifanyia kazi.
  2. Ubora wa udhu, nakuwa hilo ni kafara ya madhambi madogo, ama makubwa ni lazima kufanya toba.
  3. Sharti za kutoka kwa madhambi ni kuukamilisha udhu na kuuleta bila mapungufu kama alivyobainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  4. Kufutwa kwa madhambi katika hadithi hii kumefungamanishwa na kuyaepuka madhambi makubwa na kuyaombea toba, amesema Mtukufu: "Ikiwa mtayaepuka madhambi makubwa mnayokatazwa tutakusameheni makosa yenu" [An-Nisaa: 31].
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 216) (245). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 9). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 763). بهجة الناظرين، سليم الهلالي (2/ 247).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Fadhila - ubora wa kutawadha.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com