Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Vyenye kuharibu Udhu.

Hadithi 1

Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا وَجَدَ أَحَدُكُمْ فِي بَطْنِهِ شَيْئًا، فَأَشْكَلَ عَلَيْهِ أَخَرَجَ مِنْهُ شَيْءٌ أَمْ لَا، فَلَا يَخْرُجَنَّ مِنَ الْمَسْجِدِ حَتَّى يَسْمَعَ صَوْتًا، أَوْ يَجِدَ رِيحًا».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kitakapotatiza chochote tumboni kwa mwenye kusali, akapata shaka, je kuna chochote kimemtoka au la?, asiondoke katika swala yake na akaikatisha kwa ajili ya kurudia udhu, mpaka apate uhakika wa kutenguka udhu wake; ima kwa kusikia sauti ya upepo, au anuse harufu; kwa sababu mwenye uhakika habatilishi uhakika wake kwa shaka, hali yakuwa ana uhakika na twahara, na hadathi (kutengukwa udhu) kunatiliwa shaka.

Mafunzo
  1. Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, na ni kanuni miongoni mwa kanuni za kisheria, nayo ni; Yakini haiondoki kwa shaka, na asili ni kubaki hali iliyokuwa kama ilivyokuwa, mpaka mtu apate uhakika wa kinyume chake.
  2. Shaka haiathiri katika twahara, na mswaliji ataendelea kubaki katika twahara yake madama hajapata uhakika wa hadathi (kutengukwa udhu).
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 276) (362)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (8/ 374)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 608).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com