Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa yeye pamoja na mtumishi mwenye kukaribiana naye katika umri wake, wakimfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi anapotoka kwenda kikidhi haja yake, walikuwa wakibeba fimbo yenye meno (mkongojo) mfano wa meno ya mshale ili aifanye kuwa sitara ya kutundukia kitu chenye kusitiri, au sitara kwa ajili ya swala yake, na walikuwa wakibeba pia chombo kidogo cha ngozi kilichojaa maji , anapomaliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukidhi haja yake, basi mmoja wao anampa chombo, basi anastanji kwa maji.
Mafunzo
Muislamu anatakiwa kujiandaa kwa maji (au chochote cha kujisafishia) wakati wa kukidhi haja; ili asijekuhitaji kusimama akajichafua.
Kuhifadhi uchi wakati wa kukidhi haja asijekumtazama yeyote; kwa sababu kutazama katika uchi ni haramu, kwani alikuwa kichomeka fimbo katika Ardhi na akifunga nguo yenye kusitiri.
Kuna haja kubwa ya kuwafundisha watoto adabu za kiislamu na kuwalea katika adabu hizo; ili warithishane.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 42) (152).
صحيح مسلم (1/ 227) (271).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص40).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 43).
الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص84).
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke maji puani mwake kisha ayapenge, na atakayestanji kwa mawe basi afanye yawe witiri, na atakapo amka mmoja wenu toka usingizini basi na aoshe mikono yake kabla ya kuingiza ndani ya chombo chake, kwani mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake". Na lafudhi ya Muslim: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini kwake basi asizamishe mkono wake ndani ya chombo mpaka auoshe mara tatu, kwani hajui ni wapi ulilala mkono wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya hukumu za twahara, miongoni mwake: Ya kwanza: Nikuwa mwenye kutawadha ni lazima aingize maji puani mwake kwa kuyavuta kwa pumzi, kisha ayatoe kwa pumzi pia. Ya pili: Nikuwa atakayetaka kusafisha udhia uliomtoka na kuuondoa pasina kutumia maji kama kwa jiwe na mfano wake, basi kusafisha kwake kuwe kwa idadi ya mamoja (witiri) kwa uchache tatu na kuendelea yatakayoweza kutakatisha kilichotoka na kusafisha mahali. Ya tatu: Kuwa atakayeamka kutoka katika usingizi wa usiku asiingize kiganja chake ndani ya chombo ili atawadhe mpaka akioshe mara tatu nje ya chombo, kwani hajui ni mahali gani ulilala mkono wake, hauwezi kuaminika na kutokuwa na najisi, na huenda shetani aliuchezea na akaubebesha vitu vyenye kumdhuru mwanadamu au vyenye kuharibu maji.
Mafunzo
Ni wajibu kupandisha maji puani wakati wa udhu, nako ni: Kuingiza maji puani kwa njia ya pumzi, na pia ni wajibu kuyapenga, nako ni: Kuyatoa maji puani kwa njia ya pumzi.
Inapendeza kupenga kwa witiri.
Ni sheria kuosha mikono miwili baada ya kutoka usingizini mara tatu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 43) (162).
صحيح مسلم (1/ 233) (278).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص19).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 11).
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: “Mnapoingia chooni, msielekee Kibla, wala msikipe mgongo, bali elekeeni Mashariki au Magharibi.” Abuu Ayub akasema: Basi tukaenda Sham tukakuta vyoo vimejengwa kuelekea Kibla, tukawa tunageuka, na tunaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, mwenye kutaka kukidhi haja kubwa au ndogo kuelekea Kibla na upande wa Al-Kaaba, na asiigeuze kwa kuiweka nyuma ya mgongo wake. Bali ni lazima ageuke akiwa ndani kuelekea Mashariki au Magharibi ikiwa Kibla chake ni kama kibla cha watu wa Madina. Kisha Abuu Ayub (radhi za Allah ziwe juu yake) akaeleza kuwa walipofika Sham walikuta vyoo vilivyotayarishwa kwa ajili ya kujisaidia vimejengwa kuelekea Al-Kaaba, hivyo wakawa wakijigeuza kutoka upande wa Kibla, pamoja na hivyo bado wanamuomba msamaha Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Hekima ya kufanya hilo ni kuitukuza Al-Kaaba tukufu na kuiheshimu.
Kuomba msamaha kwa Allah baada ya kutoka mahali pa kukidhi haja.
Uzuri wa mafundisho ya Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake; Kwa sababu alipoeleza lililokatazwa akaelekeza linalofaa.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 88) (394).
صحيح مسلم (1/ 224) (264).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص37).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 39).
Kutoka kwa Abuu Katada -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya adabu: Akakataza kwa mwanaume kushika uume wake kwa mkono wa kulia wakati wa kukidhi haja, na kuondoa uchafu katika utupu wa mbele au wa nyuma kwa mkono wa kulia, kwa sababu mkono wa kulia umetayarishwa kwa matendo mema, Kama ambavyo alikataza mtu kupumulia ndani ya chombo anachonywea ndani yake.
Mafunzo
Hii inaweka wazi namna ambavyo Uislamu umetangulia kuleta ustaarabu katika adabu na usafi kabla ya watu wengine.
Kuepuka mambo machafu, ikiwa hakuna budi basi afanye kwa mkono wa kushoto.
Kumebainishwa utukufu wa mkono wa kulia, na ubora wake juu ya mkono wa kushoto.
Ukamilifu wa sheria ya Uislamu na kuenea mafundisho yake kila nyanja.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 42) (154).
صحيح مسلم (1/ 225) (267).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص41).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 45).
Imepokewa Kutoka kwa Anas Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msalani anasema: "Allaahumma inniy Auudhubika minal khubuthi wal khabaa ithi" (Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na mashetani wa kike na mashetani wa kiume).
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia mahali ambapo atakidhi haja yake hapo, haja ndogo au kubwa, anaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu, na anajielekeza kwake amkinge na shari za mashetani wa kiume na wa kike, Na limetafsiriwa neno khubuthi na khabaaithi (Mashetani wa kiume na wa kike) kwa maana ya shari na najisi.
Mafunzo
Sunna ya dua hii wakati wa kutaka kuingia msalani.
Viumbe wote ni wahitaji kwa Mola wao Mlezi katika kuzuia yenye kuwaudhi au kuwadhuru katika hali zao zote.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 40) (142).
صحيح مسلم (1/ 283) (375).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 23).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص36).
عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «اسْتَنْزِهوا من البول؛ فإنَّ عامَّة عذاب القبر منه».
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Hadithi Marfu'u: "Jisafisheni vizuri kutokana na mkojo; kwani adhabu nyingi za kaburini zinatokana na hilo".
Imepokelewa na Addaar- AlqutniDarajaSahihi
Maelezo
Anatubainishia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika hadithi hii kuwa moja ya sababu za adhabu za kaburi, ni hii iliyoenea sana, nayo nikutojisafisha vizuri na kujitwaharisha kutokana na mkojo.
Mafunzo
Kuchunga juu ya kujisafisha na kujiweka mbali na mkojo, ili usimpate katika mwili wake wala nguo yake.
Lililo bora ni kufanya haraka kuosha mahala hapo, na kujitwaharisha baada ya kupatwa; ili asiambatane na najisi, ama uwajibu wa kuiondoa unakuwa wakati wa swala.
Nikuwa mkojo ni najisi, ukiupata mwili au nguo au sehemu, unapanajisisha; Hivyo haiswihi swala kwa hilo; kwasababu kujisafisha kutokana na najisi ni moja kati ya sharti zake.
Nikuwa kuacha kujisafisha kutokana na mkojo ni katika madhambi makubwa.
kuthibiti kwa adhabu za kaburini, nazo zimethibiti kwa Qur'ani na sunna na makubaliano ya wanachuoni.
Kuthibitisha malipo Akhera, Hivyo sehemu ya kwanza katika vituo vya akhera ni kaburi: Ima iwe ni kiwanja miongoni mwa viwanja vya pepo, au shimo katika mashimo ya moto.
Marejeo
سنن الدارقطني،أبو الحسن علي بن عمر الدارقطني، تحقيق: شعيب الارنؤوط وآخرون، نشر: مؤسسة الرسالة، بيروت، لبنان، الطبعة: الأولى، 1424هـ، 2004م.
إرواء الغليل في تخريج أحاديث منار السبيل، محمد ناصر الدين الألباني، إشراف: زهير الشاويش، المكتب الإسلامي، بيروت، الطبعة: الثانية 1405هـ، 1985م.
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، عبد الله بن عبد الرحمن البسام، مكتبة الأسدي، مكة المكرّمة، الطبعة: الخامِسَة 1423هـ، 2003م.
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، عبد الله صالح الفوزان، دار ابن الجوزي، الطبعة: الأولى 1428هـ، 1432هـ.
تسهيل الإلمام بفقه الأحاديث من بلوغ المرام، صالح بن فوزان بن عبد الله الفوزان، اعتنى بإخراجه عبدالسلام بن عبد الله السليمان، الرسالة، بيروت، الطبعة: الأولى 1427هـ، 2006م.
فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام للشيخ ابن عثيمين- المكتبة الإسلامية القاهرة- تحقيق صبحي رمضان وأم إسراء بيومي- الطبعة الأولى 1427ه.
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa, na akasema: "Vitu hivyo havisafishi sawa sawa".
Imepokelewa na Addar- AlqutniDarajaSahihi
Maelezo
Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekidhi haja yake sawa iwe haja ndogo au kubwa, kustanji kwa mfupa wa mnyama au kinyesi chake na mabaki yake yaliyokauka; na akasema: Hivyo haviondoshi najisi, na wala havisafishi vizuri.
Mafunzo
Kumebainishwa baadhi ya adabu za kukidhi haja na kustanji.
Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama; kwa sababu: Ima ni najisi, au kwa sababu ni chakula cha wanyama wa Majini.
Katazo la kustanji kwa mfupa; kwa sababu ima ni najisi, au ni chakula cha Majini wenyewe.
Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotoka kukidhi haja anasema: "Ghufraanaka" Msamaha unatoka kwako.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapotoka kukidhi haja yake msalani anasema: " Ninakuomba (Msamaha) Ewe Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
Ni sunna kusema: "Ghufraanaka" baada ya kutoka mahala pa kukidhi haja.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake kumtaka msamaha Mola wake katika hali zake zote.
Inasemekana katika sababu ya kuomba msamaha baada ya kukidhi haja ni kwa sababu ya uzembe wa kushukuru neema nyingi za Mwenyezi Mungu, ikiwemo kurahisishiwa kutoka kile kinachokuudhi, na ninaomba msamaha wako kwa kushughulishwa na kukidhi haja nikaacha kukutaja.
Marejeo
سنن أبي داود (1/ 24) (30).
سنن الترمذي (1/ 57) (7).
سنن ابن ماجه (1/ 200) (300).
مسند أحمد (42/ 124) (25220).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 351).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (1/ 397).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com