Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuingia mahali ambapo atakidhi haja yake hapo, haja ndogo au kubwa, anaomba kinga kwa Mwenyezi Mungu, na anajielekeza kwake amkinge na shari za mashetani wa kiume na wa kike, Na limetafsiriwa neno khubuthi na khabaaithi (Mashetani wa kiume na wa kike) kwa maana ya shari na najisi.
- Sunna ya dua hii wakati wa kutaka kuingia msalani.
- Viumbe wote ni wahitaji kwa Mola wao Mlezi katika kuzuia yenye kuwaudhi au kuwadhuru katika hali zao zote.
صحيح البخاري (1/ 40) (142). صحيح مسلم (1/ 283) (375). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 23). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص36).