Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea

عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يُمْسِكَنَّ أَحَدُكُمْ ذَكَرَهُ بِيَمِينِهِ وَهُوَ يَبُولُ، وَلَا يَتَمَسَّحْ مِنَ الْخَلَاءِ بِيَمِينِهِ، وَلَا يَتَنَفَّسْ فِي الْإِنَاءِ».
Kutoka kwa Abuu Katada -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya adabu: Akakataza kwa mwanaume kushika uume wake kwa mkono wa kulia wakati wa kukidhi haja, na kuondoa uchafu katika utupu wa mbele au wa nyuma kwa mkono wa kulia, kwa sababu mkono wa kulia umetayarishwa kwa matendo mema, Kama ambavyo alikataza mtu kupumulia ndani ya chombo anachonywea ndani yake.

Mafunzo
  1. Hii inaweka wazi namna ambavyo Uislamu umetangulia kuleta ustaarabu katika adabu na usafi kabla ya watu wengine.
  2. Kuepuka mambo machafu, ikiwa hakuna budi basi afanye kwa mkono wa kushoto.
  3. Kumebainishwa utukufu wa mkono wa kulia, na ubora wake juu ya mkono wa kushoto.
  4. Ukamilifu wa sheria ya Uislamu na kuenea mafundisho yake kila nyanja.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 42) (154). صحيح مسلم (1/ 225) (267). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص41). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 45).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za kula na kunywa.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com