Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!",

عَنْ سَلَمَةَ بْنِ الْأَكْوَعِ رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا أَكَلَ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِشِمَالِهِ، فَقَالَ: «كُلْ بِيَمِينِكَ»، قَالَ: لَا أَسْتَطِيعُ، قَالَ: «لَا اسْتَطَعْتَ»، مَا مَنَعَهُ إِلَّا الْكِبْرُ، قَالَ: فَمَا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ.
Kutoka kwa Salama bin Al Ak'wa'i -Radhi za Allah ziwe juu yake. Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!", Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi, akasema: hakuweza tena kuunyanyua kwenda kinywani kwake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alimuona Mtume Rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja akila kwa mkono wake wa kushoto, akamuamrisha ale kwa mkono wake wa kulia, Yule bwana akamjibu kwa kiburi na kwa kuongopa kuwa hawezi! Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akamuombea dua mbaya azuiliwe kula kwa mkono wa kulia, Mwenyezi Mungu akajibu dua ya Nabii wake, kwa kupooza mkono wake wa kulia, hakuweza kuunyanyua kwenda kinywani kwake baada ya hapo kwa chakula au kinywaji.

Mafunzo
  1. Uwajibu wa kula kwa mkono wa kulia, na uharamu wa kula kwa mkono wa kushoto.
  2. Kiburi katika kutekeleza hukumu za sheria mwenye kufanya hivyo anastahiki adhabu.
  3. Ukarimu wa Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake kwa kujibu maombi yake.
  4. Sheria ya kuamrisha mema na kukataza maovu kwa kila hali hata wakati wa chakula.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1599) (2021). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 239). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 183). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 396).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za kula na kunywa.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com