عَنْ أَبِي قَتَادَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يُمْسِكَنَّ أَحَدُكُمْ ذَكَرَهُ بِيَمِينِهِ وَهُوَ يَبُولُ، وَلَا يَتَمَسَّحْ مِنَ الْخَلَاءِ بِيَمِينِهِ، وَلَا يَتَنَفَّسْ فِي الْإِنَاءِ».
Kutoka kwa Abuu Katada -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya adabu: Akakataza kwa mwanaume kushika uume wake kwa mkono wa kulia wakati wa kukidhi haja, na kuondoa uchafu katika utupu wa mbele au wa nyuma kwa mkono wa kulia, kwa sababu mkono wa kulia umetayarishwa kwa matendo mema, Kama ambavyo alikataza mtu kupumulia ndani ya chombo anachonywea ndani yake.
Mafunzo
- Hii inaweka wazi namna ambavyo Uislamu umetangulia kuleta ustaarabu katika adabu na usafi kabla ya watu wengine.
- Kuepuka mambo machafu, ikiwa hakuna budi basi afanye kwa mkono wa kushoto.
- Kumebainishwa utukufu wa mkono wa kulia, na ubora wake juu ya mkono wa kushoto.
- Ukamilifu wa sheria ya Uislamu na kuenea mafundisho yake kila nyanja.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 42) (154).
صحيح مسلم (1/ 225) (267).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص41).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 45).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ سَلَمَةَ بْنِ الْأَكْوَعِ رضي الله عنه: أَنَّ رَجُلًا أَكَلَ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِشِمَالِهِ، فَقَالَ: «كُلْ بِيَمِينِكَ»، قَالَ: لَا أَسْتَطِيعُ، قَالَ: «لَا اسْتَطَعْتَ»، مَا مَنَعَهُ إِلَّا الْكِبْرُ، قَالَ: فَمَا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ.
Kutoka kwa Salama bin Al Ak'wa'i -Radhi za Allah ziwe juu yake. Amesimulia kuwa mtu mmoja alikula chakula kwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kwa mkono wake wa kushoto, akasema: "Kula kwa mkono wako wa kulia", Akasema: Siwezi, akasema: "Kamwe, hutoweza!", Hakuna kilichomzuia ila ni kiburi, akasema: hakuweza tena kuunyanyua kwenda kinywani kwake.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alimuona Mtume Rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja akila kwa mkono wake wa kushoto, akamuamrisha ale kwa mkono wake wa kulia, Yule bwana akamjibu kwa kiburi na kwa kuongopa kuwa hawezi! Mtume Rehema na amani ziwe juu yake akamuombea dua mbaya azuiliwe kula kwa mkono wa kulia, Mwenyezi Mungu akajibu dua ya Nabii wake, kwa kupooza mkono wake wa kulia, hakuweza kuunyanyua kwenda kinywani kwake baada ya hapo kwa chakula au kinywaji.
Mafunzo
- Uwajibu wa kula kwa mkono wa kulia, na uharamu wa kula kwa mkono wa kushoto.
- Kiburi katika kutekeleza hukumu za sheria mwenye kufanya hivyo anastahiki adhabu.
- Ukarimu wa Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake Muhammadi Rehema na amani ziwe juu yake kwa kujibu maombi yake.
- Sheria ya kuamrisha mema na kukataza maovu kwa kila hali hata wakati wa chakula.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1599) (2021).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 239).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 183).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 396).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ حُذَيْفَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كُنَّا إِذَا حَضَرْنَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طَعَامًا لَمْ نَضَعْ أَيْدِيَنَا حَتَّى يَبْدَأَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَيَضَعَ يَدَهُ، وَإِنَّا حَضَرْنَا مَعَهُ مَرَّةً طَعَامًا، فَجَاءَتْ جَارِيَةٌ كَأَنَّهَا تُدْفَعُ، فَذَهَبَتْ لِتَضَعَ يَدَهَا فِي الطَّعَامِ، فَأَخَذَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِيَدِهَا، ثُمَّ جَاءَ أَعْرَابِيٌّ كَأَنَّمَا يُدْفَعُ فَأَخَذَ بِيَدِهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ الشَّيْطَانَ يَسْتَحِلُّ الطَّعَامَ أَنْ لَا يُذْكَرَ اسْمُ اللهِ عَلَيْهِ، وَإِنَّهُ جَاءَ بِهَذِهِ الْجَارِيَةِ لِيَسْتَحِلَّ بِهَا فَأَخَذْتُ بِيَدِهَا، فَجَاءَ بِهَذَا الْأَعْرَابِيِّ لِيَسْتَحِلَّ بِهِ فَأَخَذْتُ بِيَدِهِ، وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، إِنَّ يَدَهُ فِي يَدِي مَعَ يَدِهَا».
Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulikuwa tunapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hatuweki mikono yetu mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake basi anaweka mkono wake, na hakika sisi kuna wakati tulihudhuria chakula pamoja naye, akaja kijakazi kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kwa kasi kubwa kana kwamba anasukumwa, akamshika mkono wake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Shetani hukihalalisha chakula kwa kutotajwa jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho, na bila shaka alikuja na kijakazi huyu ili akihalalishe, nikashika mkono wake, akaja tena na Bedui huyu ili akihalalishe nikamshika mkono, namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wake umekamatwa na mkononi wangu pamoja na mkono wake kijakazi".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Hudhaifa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wanapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawaweki mikoni yao katika chakula mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka mkono wake, na hakika sisi tulihudhuria pamoja naye siku moja katika chakula, akaja kijakazi mmoja, kutokana na kasi yake kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kana kwamba anasukubwa, akamshika mkono wake kabla hajagusa chakula, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika Shetani hupata uwezo wa kula chakula, atakapoanza mtu kula chakula pasina kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuja na kijakazi huyu ili ajihalalishie kula, nikamshika mkono wake, kisha akaja na huyu Bedui, ili akihalalishe nikamshika mkono wake, ninamuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wa Shetani ulikuwa mkononi mwangu pamoja na mkono wake, kisha akataja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu na akala.
Mafunzo
- Heshima ya Maswahaba kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na adabu yao kwake.
- Katika adabu za chakula ni mdogo kusubiri mpaka aanze mkubwa na mwenye heshima katika kula.
- Shetani huwasukuma baadhi ya watu wanaojisahau katika matendo ambayo yeye anayapenda; ili aweze kufikia lengo lake, na miongoni mwake ni haya yaliyoko katika hadithi hii.
- Anasema Nawawi: Wanasema Wanachuoni: Na inapendeza mtu kutamka kwa sauti Bismillaah ili mwenzake asikie na amzindue kwa hilo.
- Nikuwa atakapokuja mtu anataka kula na ukawa hujamsikia anasema Bismillaah basi mshike mkono wake mpaka aseme Bismillaah.
- Uwajibu wa kuondoa uovu kwa mwenye kujua, na kuondoa uovu kwa mkono kwa mwenye uwezo.
- Hadithi hii ni alama niongoni mwa alama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kiasi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu alimjulisha kilichotokea katika kisa hiki.
- Shetani hapati uwezo wa kula chakula cha watu wenye imani isipokuwa kama wasipotaja jina la Mwenyezi Mungu katika chakula hicho.
- Inapendeza kuwafundisha watu adabu za kula na kunywa katika Uislamu.
- Inapendeza kutoa kiapo; kwa ajili ya kusisitiza jambo kwa msikilizaji.
- Amesema Nawawi: Bismillaah wakati wa kunywa maji na maziwa na Asali na mchuzi na dawa na vinywaji vinginevyo ni kama Bismillaah wakati wa chakula.
- Amesema Nawawi: Na ikiwa mtu ataacha Bismillaah mwanzo wa chakula kwa makusudi au kwa kusahau au kwa ujinga au kwa kulazimishwa au kwa kushindwa kwa sababu yoyote ile iliyojitokeza, kisha akaweza kufanya hivyo wakati wa kula kwake, basi ni sunna aseme: "Bismillaahi Awwalihi wa Aakhirihi" Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho; kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Akatapokula mmoja wenu basi na ataje jina la Mwenyezi Mungu, na ikiwa atasahau kumtaja Mwenyezi Mungu mwanzo wa chakula, basi na aseme: Bismillaahi Awwalihi Wa Aakhirihi" Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwanzo wake na mwisho wake". Kaipokea Abuu Daudi na Tirmidhi.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1597) (2017).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 51).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 192).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (10/ 202).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 600).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ وَحْشِيِّ بْنِ حَرْبٍ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّهُمْ قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا نَأْكُلُ وَلَا نَشْبَعُ، قَالَ: «فَلَعَلَّكُمْ تَأْكُلُونَ مُتَفَرِّقِينَ؟» قَالُوا: نَعَمْ. قَالَ: «فَاجْتَمِعُوا عَلَى طَعَامِكُمْ، وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ، يُبَارَكْ لَكُمْ فِيهِ».
Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba wao walisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakula lakini hatushibi, akasema: "Huenda nyinyi mnakula kila mtu peke yake?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Baadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.
Mafunzo
- Kukusanyika kwa ajili ya chakula na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula ni sababu ya kupata baraka katika chakula, na kupatikana shibe kwa kukila kwake.
- Utengano wote ni shari, na umoja wote ni heri.
- Himizo la kukusanyika na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa chakula.
- Amesema Assanadi: Kwa sababu ya mkusanyika baraka huteremka katika chakula, na kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Shetani hushindwa kukifikia chakula.
Marejeo
سنن أبي داود (5/ 588) (3764).
سنن ابن ماجه (4/ 418) (3286).
مسند أحمد (25/ 485) (16078).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 217).
نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 607).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 59).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ اللهَ لَيَرْضَى عَنِ الْعَبْدِ أَنْ يَأْكُلَ الْأَكْلَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا، أَوْ يَشْرَبَ الشَّرْبَةَ فَيَحْمَدَهُ عَلَيْهَا».
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Allah humridhia mja anapokula chakula akamshukuru juu ya chakula hicho, au akanywa kinywaji chochote akamshukuru kwa kinywaji hicho".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa shukurani za mja kwa Mola wake Mlezi juu ya fadhila zake na neema zake ni miongoni mwa mambo ambayo huleta radhi za Allah; akala chakula akasema: Al-hamdulillah, na akanywa kinywaji na akasema: Al-hamdulillah.
Mafunzo
- Ukarimu wa Allah Mtukufu, ametoa fadhila zake kwa riziki na kisha akaridhia shukurani.
- Radhi za Allah hupatikana kwa sababu nyepesi, kama kushukuru baada ya kula na kunywa.
- Katika adabu za chakula na kinywaji: Ni kumshukuru Allah Mtukufu baada ya kula na kunywa.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 2095) (2734).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن وغيره (1/ 164).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 215).
شرح رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين، لابن عثيمين (2/ 203).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين.
تطرز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص764).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عُمر بن أبي سلمة رضي الله عنه قال: كُنْتُ غُلَامًا فِي حَجْرِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَتْ يَدِي تَطِيشُ فِي الصَّحْفَةِ، فَقَالَ لِي رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يَا غُلَامُ، سَمِّ اللهَ، وَكُلْ بِيَمِينِكَ، وَكُلْ مِمَّا يَلِيكَ» فَمَا زَالَتْ تِلْكَ طِعْمَتِي بَعْدُ.
Kutoka kwa Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilikuwa kijana mdogo ndani ya nyumba ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na mkono wangu ulikuwa ukizunguka huku na kule katika sahani (ya chakula), akasema kuniambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: " Ewe kijana, mtaje Mwenyezi Mungu, na kula kwa mkono wako wa kulia, na kula kile kinachokuelekea" Ulibakia kuwa ndio ulaji wangu huo hata baada yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-, huyu ni mtoto wa mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ummu Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na alikuwa chini ya malezi yake na usimamizi wake, kwamba yeye alikuwa wakati wa kula akihamisha mkono wake katika pande zote za chombo ili achukue chakula, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamfundisha adabu tatu miongoni mwa adabu za kula.
Adabu ya kwanza: Kusema: "Bismillah" Mwanzo wa kula.
Ya pili: Kula kwa mkono wa kulia.
Ya tatu: Kula upande ulio karibu naye katika chakula.
Mafunzo
- Katika adabu za kula na kunywa ni kusema Bismillahi mwanzo wake.
- Kuwafundisha adabu watoto, hasa hasa wale walio chini ya malezi ya mtu.
- Upole wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, ameuonyesha katika kuwafundisha watoto na kuwaadabisha.
- Katika adabu za chakula ni mtu kula kile kinachomuelekea, isipokuwa chakula kikiwa na aina tofauti tofauti, hapo anaruhusiwa kuchukua.
- Masahaba kushikamana na yale aliyowaadabisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hili tunajifunza kutoka katika kauli ya Omari: Uliendelea kuwa ndio ulaji wangu hata baada yake.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 68) (5376)، (3/ 61) (2092).
صحيح مسلم (3/ 1599) (2022).
شرح النووي على مسلم (13/ 193).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، للبسام (5/ 440).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (4/ 616).
منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 439).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 169).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن ابن عمر رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «إِذَا أَكَلَ أَحَدُكُمْ فَلْيَأْكُلْ بِيَمِينِهِ، وَإِذَا شَرِبَ فَلْيَشْرَبْ بِيَمِينِهِ، فَإِنَّ الشَّيْطَانَ يَأْكُلُ بِشِمَالِهِ، وَيَشْرَبُ بِشِمَالِهِ».
Na imepokewa kutoka kwa bin Omari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake - amesema: "Atakapo kula mmoja wenu basi na ale kwa mkono wake wa kulia, na atakapo kunywa basi na anywe kwa mkono wake wa kulia, kwani Shetani anakula kwa mkono wake wa kushoto, na anakunywa kwa mkono wake wa kushoto".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anamuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu ale na anywe kwa mkono wake wa kulia, na anakataza kula na kunywa kwa mkono wa kushoto; na hii ni kwa sababu Shetani anakula na anakunywa kwa kushoto.
Mafunzo
- Katazo la kujifananisha na Shetani kwa kula au kunywa kwa kushoto.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1598) (2020).
توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، للبسام (5/ 445).
فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 270).
سبل السلام شرح بلوغ المرام، للصنعاني (2/ 625).
عون المعبود شرح سنن أبي داود (10/ 179).
فتاوى اللجنة الدائمة - المجموعة الأولى- (26/ 387).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com