Anaeleza Omari bin Abii Salama -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-, huyu ni mtoto wa mke wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Ummu Salama -Radhi za Allah ziwe juu yake-, na alikuwa chini ya malezi yake na usimamizi wake, kwamba yeye alikuwa wakati wa kula akihamisha mkono wake katika pande zote za chombo ili achukue chakula, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamfundisha adabu tatu miongoni mwa adabu za kula. Adabu ya kwanza: Kusema: "Bismillah" Mwanzo wa kula. Ya pili: Kula kwa mkono wa kulia. Ya tatu: Kula upande ulio karibu naye katika chakula.
- Katika adabu za kula na kunywa ni kusema Bismillahi mwanzo wake.
- Kuwafundisha adabu watoto, hasa hasa wale walio chini ya malezi ya mtu.
- Upole wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, ameuonyesha katika kuwafundisha watoto na kuwaadabisha.
- Katika adabu za chakula ni mtu kula kile kinachomuelekea, isipokuwa chakula kikiwa na aina tofauti tofauti, hapo anaruhusiwa kuchukua.
- Masahaba kushikamana na yale aliyowaadabisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na hili tunajifunza kutoka katika kauli ya Omari: Uliendelea kuwa ndio ulaji wangu hata baada yake.
صحيح البخاري (7/ 68) (5376)، (3/ 61) (2092). صحيح مسلم (3/ 1599) (2022). شرح النووي على مسلم (13/ 193). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، للبسام (5/ 440). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (4/ 616). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 439). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 169).