Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho

عَنْ وَحْشِيِّ بْنِ حَرْبٍ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّهُمْ قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا نَأْكُلُ وَلَا نَشْبَعُ، قَالَ: «فَلَعَلَّكُمْ تَأْكُلُونَ مُتَفَرِّقِينَ؟» قَالُوا: نَعَمْ. قَالَ: «فَاجْتَمِعُوا عَلَى طَعَامِكُمْ، وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ، يُبَارَكْ لَكُمْ فِيهِ».
Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba wao walisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakula lakini hatushibi, akasema: "Huenda nyinyi mnakula kila mtu peke yake?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Baadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.

Mafunzo
  1. Kukusanyika kwa ajili ya chakula na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula ni sababu ya kupata baraka katika chakula, na kupatikana shibe kwa kukila kwake.
  2. Utengano wote ni shari, na umoja wote ni heri.
  3. Himizo la kukusanyika na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa chakula.
  4. Amesema Assanadi: Kwa sababu ya mkusanyika baraka huteremka katika chakula, na kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Shetani hushindwa kukifikia chakula.
Marejeo

سنن أبي داود (5/ 588) (3764). سنن ابن ماجه (4/ 418) (3286). مسند أحمد (25/ 485) (16078). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 217). نزهة المتقين بشرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 607). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 59).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za kula na kunywa.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com

Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho · Hadithi zenye maelezo · Sabīl