Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُسْتَنْجَى بِرَوْثٍ أَوْ عَظْمٍ، وَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَا تُطَهِّرَانِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa, na akasema: "Vitu hivyo havisafishi sawa sawa".
Imepokelewa na Addar- AlqutniDarajaSahihi
Maelezo

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekidhi haja yake sawa iwe haja ndogo au kubwa, kustanji kwa mfupa wa mnyama au kinyesi chake na mabaki yake yaliyokauka; na akasema: Hivyo haviondoshi najisi, na wala havisafishi vizuri.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa baadhi ya adabu za kukidhi haja na kustanji.
  2. Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama; kwa sababu: Ima ni najisi, au kwa sababu ni chakula cha wanyama wa Majini.
  3. Katazo la kustanji kwa mfupa; kwa sababu ima ni najisi, au ni chakula cha Majini wenyewe.
Marejeo

سنن الدارقطني (1/ 88) (152). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (1/ 355). سبل السلام، للصنعاني (1/ 118). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (1/ 374).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za Kukidhi Haja.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com