Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu

عَنْ سَلْمَانَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ لَنَا الْمُشْرِكُونَ: إِنِّي أَرَى صَاحِبَكُمْ يُعَلِّمُكُمْ حَتَّى يُعَلِّمَكُمُ الْخِرَاءَةَ، فَقَالَ: أَجَلْ، إِنَّهُ نَهَانَا أَنْ يَسْتَنْجِيَ أَحَدُنَا بِيَمِينِهِ، أَوْ يَسْتَقْبِلَ الْقِبْلَةَ، وَنَهَى عَنِ الرَّوْثِ وَالْعِظَامِ وَقَالَ: «لَا يَسْتَنْجِي أَحَدُكُمْ بِدُونِ ثَلَاثَةِ أَحْجَارٍ».
Kutoka kwa Salman radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Washirikina walisema kutuambia: Hakika mimi ninamuona jamaa yenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni kukidhi haja, akasema: Ndiyo, hakika yeye ametukataza kustanji mmoja wetu kwa mkono wake wa kulia, au kuelekea kibla, na akakataza kinyesi cha wanyama na mifupa, na akasema: "Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amesema Salman Al-Faarisi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Washirikina walisema kwa kutukejeli: Hakika Nabii wenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni namna gani mtakidhi haja zenu kama haja ndogo au kubwa! Akasema Salmaan: Ndiyo, ametufundisha adabu za kukidhi haja; na miongoni mwake ni kwamba alitukataza rehema na amani ziwe juu yake kustanjia baada ya kukidhi haja kwa mkono wa kulia, kwa kuulinda na najisi na kwa kuupa heshima, au kuelekea kibla wakati wa haja ndogo au kubwa, na akakataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama na mabaki yake na mifupa yake, na asitosheke aliyekidhi haja katika kustanji kwa chini ya mawe matatu.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa kuenea na ukamilifu wa sheria ya Uislamu katika kila wanachokihitajia watu.
  2. Kumebainishwa baadhi ya adabu za msalani na kustanji.
  3. Uharamu wa kuelekea kibla wakati wa kukidhi haja ndogo au kubwa; kwa kauli yake: "Alitukataza" Na asili ya katazo ni uharamu.
  4. Katazo la kustanji, au kutumia maji kwa mkono wa kulia; kwa sababu ya kuuheshimu.
  5. Ubora wa mkono wa kulia kwa mkono wa kushoto; kwa sababu mkono wa kushoto hutumika kuondoa najisi na uchafu, na wa kulia ni kinyume na hivyo.
  6. Uwajibu wa kuondoa najisi kwa maji au mawe, sawa sawa najisi iwe kidogo au nyingi.
  7. Katazo la kustanji kwa chini ya mawe matatu; kwa sababu mawe chini ya matutu huwa hayatakatishi mara nyingi.
  8. Kila kinachotimiza lengo la kujisafisha na kujitakatisha, basi kinafaa, bali alitaja mawe rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu ndio hutumika mara nyingi, na kila kitakachokuwa hivyo basi hakina maana.
  9. Mapendekezo ya kuhitimisha kustanji kwa witiri, ikiwa kutakata kutakuwa kwa mawe manne basi itapendeza aongeze la tano, na hivyo hivyo; kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayestanji kwa mawe basi na afanye witiri".
  10. Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama: ima ni kwakuwa ni najisi, au kwakuwa ni malisho ya wanyama wa Majini.
  11. Katazo la kustanji kwa mifupa; kwakuwa ima ni najisi, au ni chakula cha majini wenyewe.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 224) (262). مشارق الأنوار على صحاح الآثار، عياض بن موسى اليحصبي السبتي. معجم اللغة العربية المعاصرة، أحمد مختار عبد الحميد عمر بمساعدة فريق عمل. توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، عبد الله بن عبد الرحمن البسام. تسهيل الإلمام بفقه الأحاديث من بلوغ المرام، صالح بن فوزان بن عبد الله الفوزان. فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، محمد بن صالح العثيمين. منحة العلام في شرح بلوغ المرام، عبد الله صالح الفوزان. شرح سنن أبي داود، عبد المحسن بن حمد بن عبد المحسن العباد.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za Kukidhi Haja.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com