Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدْخُلُ الْخَلَاءَ، فَأَحْمِلُ أَنَا وَغُلَامٌ نَحْوِي إِدَاوَةً مِنْ مَاءٍ وَعَنَزَةً فَيَسْتَنْجِي بِالْمَاءِ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa yeye pamoja na mtumishi mwenye kukaribiana naye katika umri wake, wakimfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi anapotoka kwenda kikidhi haja yake, walikuwa wakibeba fimbo yenye meno (mkongojo) mfano wa meno ya mshale ili aifanye kuwa sitara ya kutundukia kitu chenye kusitiri, au sitara kwa ajili ya swala yake, na walikuwa wakibeba pia chombo kidogo cha ngozi kilichojaa maji , anapomaliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukidhi haja yake, basi mmoja wao anampa chombo, basi anastanji kwa maji.

Mafunzo
  1. Muislamu anatakiwa kujiandaa kwa maji (au chochote cha kujisafishia) wakati wa kukidhi haja; ili asijekuhitaji kusimama akajichafua.
  2. Kuhifadhi uchi wakati wa kukidhi haja asijekumtazama yeyote; kwa sababu kutazama katika uchi ni haramu, kwani alikuwa kichomeka fimbo katika Ardhi na akifunga nguo yenye kusitiri.
  3. Kuna haja kubwa ya kuwafundisha watoto adabu za kiislamu na kuwalea katika adabu hizo; ili warithishane.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 42) (152). صحيح مسلم (1/ 227) (271). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص40). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 43). الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص84).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ubora wa Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com