عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدْخُلُ الْخَلَاءَ، فَأَحْمِلُ أَنَا وَغُلَامٌ نَحْوِي إِدَاوَةً مِنْ مَاءٍ وَعَنَزَةً فَيَسْتَنْجِي بِالْمَاءِ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiingia chooni, ninambebea mimi pamoja na kijana wa rika langu, chombo chenye maji na mkongojo, basi anastanji kwa maji.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa yeye pamoja na mtumishi mwenye kukaribiana naye katika umri wake, wakimfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake pindi anapotoka kwenda kikidhi haja yake, walikuwa wakibeba fimbo yenye meno (mkongojo) mfano wa meno ya mshale ili aifanye kuwa sitara ya kutundukia kitu chenye kusitiri, au sitara kwa ajili ya swala yake, na walikuwa wakibeba pia chombo kidogo cha ngozi kilichojaa maji , anapomaliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukidhi haja yake, basi mmoja wao anampa chombo, basi anastanji kwa maji.
Mafunzo
- Muislamu anatakiwa kujiandaa kwa maji (au chochote cha kujisafishia) wakati wa kukidhi haja; ili asijekuhitaji kusimama akajichafua.
- Kuhifadhi uchi wakati wa kukidhi haja asijekumtazama yeyote; kwa sababu kutazama katika uchi ni haramu, kwani alikuwa kichomeka fimbo katika Ardhi na akifunga nguo yenye kusitiri.
- Kuna haja kubwa ya kuwafundisha watoto adabu za kiislamu na kuwalea katika adabu hizo; ili warithishane.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 42) (152).
صحيح مسلم (1/ 227) (271).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص40).
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 43).
الإفهام في شرح عمدة الأحكام، لابن باز (ص84).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ سَهْلُ بْنُ سَعْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ يَوْمَ خَيْبَرَ: «لَأُعْطِيَنَّ هَذِهِ الرَّايَةَ غَدًا رَجُلًا يَفْتَحُ اللَّهُ عَلَى يَدَيْهِ، يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيُحِبُّهُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ»، قَالَ: فَبَاتَ النَّاسُ يَدُوكُونَ لَيْلَتَهُمْ أَيُّهُمْ يُعْطَاهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ النَّاسُ غَدَوْا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كُلُّهُمْ يَرْجُو أَنْ يُعْطَاهَا، فَقَالَ: «أَيْنَ عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ؟» فَقِيلَ: هُوَ يَا رَسُولَ اللَّهِ يَشْتَكِي عَيْنَيْهِ، قَالَ: «فَأَرْسِلُوا إِلَيْهِ»، فَأُتِيَ بِهِ فَبَصَقَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي عَيْنَيْهِ وَدَعَا لَهُ، فَبَرَأَ حَتَّى كَأَنْ لَمْ يَكُنْ بِهِ وَجَعٌ، فَأَعْطَاهُ الرَّايَةَ، فَقَالَ عَلِيٌّ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أُقَاتِلُهُمْ حَتَّى يَكُونُوا مِثْلَنَا؟ فَقَالَ: «انْفُذْ عَلَى رِسْلِكَ حَتَّى تَنْزِلَ بِسَاحَتِهِمْ، ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى الإِسْلاَمِ، وَأَخْبِرْهُمْ بِمَا يَجِبُ عَلَيْهِمْ مِنْ حَقِّ اللَّهِ فِيهِ، فَوَاللَّهِ لَأَنْ يَهْدِيَ اللَّهُ بِكَ رَجُلًا وَاحِدًا، خَيْرٌ لَكَ مِنْ أَنْ يَكُونَ لَكَ حُمْرُ النَّعَمِ».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema siku ya vita vya Khaibari: "Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaeleza Maswahaba kuhusu ushindi wa Waislamu dhidi ya Mayahudi wa Khaibar siku ya kesho, na hilo litakuwa mikononi mwa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera ambayo hutumiwa na jeshi kama nembo yake. Na mtu huyu miongoni mwa sifa zake ni pamoja na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Kwa hiyo Maswahaba walipitisha usiku kucha wakijadiliana na kuzungumza juu ya nani atapewa bendera? Kwa kutamani kuipata heshima hii kubwa, Ilipofika asubuhi walikwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wote wakiwa na matumaini ya kupata heshima hii.
Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuulizia Ally bin Abi Twalib Allah amuwie radhi?
Pakasemwa: Ni mgonjwa na analalamika kuhusu macho yake.
Basi rehema na amani zimshukie, akamtumia watu wakamlete, akamtemea Ally machoni katika mate yake matukufu na akamuombea, akapona ugonjwa wake kana kwamba hakuwa na maradhi, akampa bendera na akamwamuru aende kwa upole mpaka aikaribie ngome ya maadui na awaite katika Uislamu, ikiwa watamjibu; Awaambie ni wajibu gani wanapaswa kufanya.
Kisha rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza Ally ubora wa kumuita mtu kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ikiwa mlinganiaji atakuwa ni sababu ya kuongoka kwa mtu mmoja, hiyo ni bora zaidi kwake kuliko kuwa na ngamia wekundu ambao ndio utajiri wa thamani zaidi kwa Waarabu, azimiliki au azitoe sadaka.
Mafunzo
- Ubora wa Ally bin Abi Twalib – Mwenyezi Mungu amuwie radhi – na ushahidi wa Mtume – Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani – juu yake, wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake juu yake, na mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
- Maswahaba walikuwa na shauku ya kufanya kheri na kulikimbilia kwao hilo.
- Sheria ya adabu wakati wa vita na kuacha kutojali na kelele zenye kuudhi yasiyokuwa ya lazima.
- Miongoni mwa dalili za utume wake, rehema na amani ziwe juu yake, ni kutoa habari ya ushindi dhidi ya Mayahudi, na kumponya kwake macho Ally bin Abi Twalib mikononi mwake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
- Madhumuni makubwa ya Jihadi ni watu kuingia katika Uislamu.
- Nikuwa wito wa kuwaita watu katika Uislamu hutolewa taratibu taratibu, kwanza kafiri ataombwa kusilimu kwa kutamka Shahada mbili, kisha ataamrishwa kutekeleza faradhi za Uislamu baada ya hapo.
- Fadhila za kuwaita watu katika Uislamu na kheri zilizomo kwa mlinganiwaji na mlinganiaji, mlinganiwaji anaweza kuongoka, na mlinganiaji kwa hilo atalipwa malipo makubwa.
Marejeo
صحيح البخاري (5/ 134) (4210).
صحيح مسلم (4/ 1872) (2406).
فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، (ص88).
القول المفيد على كتاب التوحيد، (1/ 134).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، (ص57).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، (ص67).
التمهيد لشرح كتاب التوحيد، (ص59).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن جابر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لن يدخلَ النارَ رجلٌ شَهِد بدرًا والحُدَيْبِيَة».
Kutoka kwa Jaabir radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hatoingia motoni mtu aliyeshuhudia vita vya Badri na Hudaibia".
Imepokelewa na Ahmad na asili yake ipo katika Sahih MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hatoingia motoni aliyehudhuria vita vya Badri vilivyotokea katika mwaka wa pili wa Hijiria (kalenda ya kiislamu) akipigana pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wala aliyehudhuria suluhu ya Hudaibia, na ndani yake kukiwa na uungaji mkono wa ridhaa (Baiatu ridhiwani) uliotokea katika mwaka wa sita wa Hijiria.
Mafunzo
- Hapa kuna fadhila ya watu wa Badri na Hudaibia, na kwamba wao hawatoingia motoni.
- Kumebainishwa kwamba Mwenyezi Mungu amechukua dhamana ya dhulma zao, na kuwawezesha kufa katika imani, na kuwaingiza peponi pasina kutanguliwa na adhabu ya moto, hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1942) (2495) .
مسند أحمد (23/ 410) (15262).
المصباح المنير في غريب الشرح الكبير، لأحمد الفيومي (1/ 123).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 302).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (16/ 57).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن أنس رضي الله عنه، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لأبي بكر وعمر: «هذان سَيِّدا كُهُول أهل الجنة من الأوَّلِين والآخِرين إلا النبيِّين والمرسلين».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abubakari Swiddiq na Omari Al-farouq radhi za Allah ziwe juu yao ndio viumbe bora baada ya Manabii, na ndio watu bora katika watu walioingia peponi baada ya Manabii na Mitume.
Mafunzo
- Abubakari na Omari radhi za Allah ziwe juu yao ndio watu bora baada ya Mitume na Manabii.
- Peponi hakuna mtu wa makamo, bali atakayeingia atakuwa ni kijana wa miaka thelathini na tatu (33), na makusudio yake wao ndio mabosi wa kila mtu aliyekufa katika umri wa makamo duniani, au hilo ni kulingana na jinsi walivyokuwa katika dunia wakati wa kuzungumzwa kwa hadithi hii.
Marejeo
سنن الترمذي (6/ 45) (3664).
تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، لمحمد المباركفوري (10/ 103).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com