Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume

عن أنس رضي الله عنه، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لأبي بكر وعمر: «هذان سَيِّدا كُهُول أهل الجنة من الأوَّلِين والآخِرين إلا النبيِّين والمرسلين».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abubakari Swiddiq na Omari Al-farouq radhi za Allah ziwe juu yao ndio viumbe bora baada ya Manabii, na ndio watu bora katika watu walioingia peponi baada ya Manabii na Mitume.

Mafunzo
  1. Abubakari na Omari radhi za Allah ziwe juu yao ndio watu bora baada ya Mitume na Manabii.
  2. Peponi hakuna mtu wa makamo, bali atakayeingia atakuwa ni kijana wa miaka thelathini na tatu (33), na makusudio yake wao ndio mabosi wa kila mtu aliyekufa katika umri wa makamo duniani, au hilo ni kulingana na jinsi walivyokuwa katika dunia wakati wa kuzungumzwa kwa hadithi hii.
Marejeo

سنن الترمذي (6/ 45) (3664). تحفة الأحوذي بشرح جامع الترمذي، لمحمد المباركفوري (10/ 103).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Vyeo vya Maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com

Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume · Hadithi zenye maelezo · Sabīl