عن جابر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لن يدخلَ النارَ رجلٌ شَهِد بدرًا والحُدَيْبِيَة».
Kutoka kwa Jaabir radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hatoingia motoni mtu aliyeshuhudia vita vya Badri na Hudaibia".
Imepokelewa na Ahmad na asili yake ipo katika Sahih MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hatoingia motoni aliyehudhuria vita vya Badri vilivyotokea katika mwaka wa pili wa Hijiria (kalenda ya kiislamu) akipigana pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wala aliyehudhuria suluhu ya Hudaibia, na ndani yake kukiwa na uungaji mkono wa ridhaa (Baiatu ridhiwani) uliotokea katika mwaka wa sita wa Hijiria.
Mafunzo
Hapa kuna fadhila ya watu wa Badri na Hudaibia, na kwamba wao hawatoingia motoni.
Kumebainishwa kwamba Mwenyezi Mungu amechukua dhamana ya dhulma zao, na kuwawezesha kufa katika imani, na kuwaingiza peponi pasina kutanguliwa na adhabu ya moto, hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni mwenye fadhila kubwa.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1942) (2495) .
مسند أحمد (23/ 410) (15262).
المصباح المنير في غريب الشرح الكبير، لأحمد الفيومي (1/ 123).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 302).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي (16/ 57).
عن أنس رضي الله عنه، قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم لأبي بكر وعمر: «هذان سَيِّدا كُهُول أهل الجنة من الأوَّلِين والآخِرين إلا النبيِّين والمرسلين».
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema: Alisema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kumwambia Abubakari na Omari: "Hawa wawili ni mabosi wa watu wazima wa peponi kwanzia watu wa mwanzo na wa mwisho, isipokuwa Manabii na Mitume".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Abubakari Swiddiq na Omari Al-farouq radhi za Allah ziwe juu yao ndio viumbe bora baada ya Manabii, na ndio watu bora katika watu walioingia peponi baada ya Manabii na Mitume.
Mafunzo
Abubakari na Omari radhi za Allah ziwe juu yao ndio watu bora baada ya Mitume na Manabii.
Peponi hakuna mtu wa makamo, bali atakayeingia atakuwa ni kijana wa miaka thelathini na tatu (33), na makusudio yake wao ndio mabosi wa kila mtu aliyekufa katika umri wa makamo duniani, au hilo ni kulingana na jinsi walivyokuwa katika dunia wakati wa kuzungumzwa kwa hadithi hii.
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com