Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Siasa ya Kisheria.

Hadithi 19

Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu

عن عُبَادَةَ بن الصَّامتِ رضي الله عنه قال: بَايَعْنَا رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم على السَّمْعِ وَالطَّاعَةِ فِي الْعُسْرِ وَالْيُسْرِ، وَالْمَنْشَطِ وَالْمَكْرَهِ، وعلى أَثَرَةٍ علينا، وعلى أَلَّا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أهلَه، وعلى أَنْ نَقُولَ بِالْحَقِّ أينما كُنَّا، لا نَخَافُ في الله لَوْمَةَ لَائِمٍ.
Kutoka kwa Ubaadah bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu, na tusiwanyang'anye uongozi wanaostahiki, na tusema ukweli mahala popote tuwapo, tusiogope kwa Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alichukua ahadi na mkataba kutoka kwa Masahaba ya utii kwa wenye mamlaka na watawala katika wepesi na ugumu, na katika hali ya utajiri na umasikini, na sawa sawa amri zao ziwe katika yale wanayoyapenda au kuyachukia, hata kama watawala watajipendelea kuliko raia kwa mali ya umma au vyeo au mengineyo, basi ni wajibu kwao kusikiliza na kutii katika wema, na wasitoke dhidi yao, kwa sababu fitina na ufisadi katika kupigana nao ni mambo makubwa na ni mabaya mno kuliko ufisadi unaotokea kwa sababu ya dhulma zao, na katika mambo waliyoyachukulia kiapo ni waseme kweli mahali popote, wakilitakasa hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hawamuogopi mwenye kuwalaumu.

Mafunzo
  1. Matunda ya kusikia na kuwatii viongozi ni kukusanyika kwa nguvu na umoja wa waislamu na kuacha migawanyiko.
  2. Uwajibu wa kusikia na kuwatii wenye mamlaka katika yale yasiyomuasi Mwenyezi Mungu katika hali ya wepesi na uzito, na katika mambo yenye kufurahisha na kuchukiza na kule kujipendelea wanakojipendelea wao.
  3. Uwajibu wa kusema kweli mahala popote tuwapo, bila kuogopa katika jambo la Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulauma.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 47) (7055-7056)، (9/ 77) (7199، 7200). صحيح مسلم (3/ 1470) (1709). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 277). رياض الصالحين، للنووي (ص83) (186). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 419). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 202).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo

عن مَعقِلِ بن يَسار المُزَنِيّ رضي الله عنه قال: إني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ».
Kutoka kwa Ma'akali bin Yasaari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila mtu ambaye Mwenyezi Mungu atamfanya kuwa ni msimamizi au kiongozi kwa watu, sawa sawa uwe ni uongozi wa umma, kama Raisi au usimamizi wa sekta binafsi kama mtu katika nyumba yake na mwanamke katika nyumba yake, akafanya uzembe kutekeleza haki za raia wake, na akawafanyia udanganyifu na wala hakuwanasihi, akapoteza haki zao za kidini na kidunia, huyu atakuwa kastahiki adhabu hii kali.

Mafunzo
  1. Adhabu hii si maalum kwa kiongozi mkuu na wasaidizi wake, bali inajumuisha kila atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia.
  2. Wajibu kwa kila atakayesimamia lolote katika mambo ya waislamu awanasihi, na ajitahidi kutimiza amana, na atahadhari na hiyana.
  3. Ukubwa wa majukumu kwa kila atakayewasimamia raia kwa umma au binafsi, sawa majukumu yawe madogo au makubwa.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 64) (7150). صحيح مسلم (1/ 125) (142). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 706). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 488). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 543).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com