عن تميم الداري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».
Imepokewa Kutoka kwa Tamim Ad-dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema: "Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dini imesimama katika misingi ya kutakasa nia (Ikhlas) na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu, kikamilifu bila uzembe au udanganyifu.
Akaulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nasaha huwa kwa ajili ya nani? Akasema:
Kwanza: Nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha mwingine pamoja naye, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kuzitukuza amri zake, na kulingania watu katika kumuamini.
Pili: Nasaha ni kwa ajili ya kitabu cha Mwenyezi Mungu nacho ni Qur'ani Tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, nakuwa kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza, na tunakisoma ukweli wa kukisoma, na tunazifanyia kazi aya zake za wazi, na tunazikubali zenye kutatiza, na tunapinga upotoshaji wa wenye kupindisha, na tunayazingatia mawaidha yake, na kuieneza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo.
Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Tuitakidi kuwa yeye ni Mtume wa mwisho, na tumsadikishe katika yale aliyokuja nayo, na tutekeleze amri zake, na tuyaepuke makatazo yake, na tusimuabudu Allah isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tuitukuze haki yake, na tumuheshimu, na tuutangaze ujumbe wake, na tuisambaze sheria yake, na tuzikanushe tuhuma dhidi yake.
Nne: Nasaha kwa viongozi wa waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu.
Tano: Nasaha kwa waislamu: Kwa kuwafanyia wema na kuwalingania, na kuzuia maudhi dhidi yao, na kuwapendelea kheri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.
Mafunzo
- Amri ya kunasihiana ni kwa watu wote.
- Ukubwa na utukufu wa nafasi ya nasaha katika dini.
- Dini imekusanya mambo ya itikadi, maneno, na matendo.
- Miongoni mwa nasaha ni kujinasihi mwenyewe kutomfanyia udanganyifu yule mwenye kunasihiwa pamoja na kumtakia kheri.
- Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba anataja jambo kwa ujumla kisha analifafanua.
- Kuanza na lenye umuhimu zaidi kisha linalofuata, kwani alianza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha kitabu chake, kisha Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kisha viongozi wa waislamu, kisha watu wote kwa ujumla.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 74) (55).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص21).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص115).
شرح النووي على مسلم (2/ 37).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ وَائِلٍ الْحَضْرَمِيِّ قَالَ: سَأَلَ سَلَمَةُ بْنُ يَزِيدَ الْجُعْفِيُّ رضي الله عنه رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا نَبِيَّ اللهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ قَامَتْ عَلَيْنَا أُمَرَاءُ يَسْأَلُونَا حَقَّهُمْ وَيَمْنَعُونَا حَقَّنَا، فَمَا تَأْمُرُنَا؟ فَأَعْرَضَ عَنْهُ، ثُمَّ سَأَلَهُ، فَأَعْرَضَ عَنْهُ، ثُمَّ سَأَلَهُ فِي الثَّانِيَةِ أَوْ فِي الثَّالِثَةِ، فَجَذَبَهُ الْأَشْعَثُ بْنُ قَيْسٍ، وَقَالَ: «اسْمَعُوا وَأَطِيعُوا، فَإِنَّمَا عَلَيْهِمْ مَا حُمِّلُوا، وَعَلَيْكُمْ مَا حُمِّلْتُمْ».
Kutoka kwa Wail bin Hadhrami amesema: Salama bin Yazidi Al-Ju'fi radhi za Allah ziwe juu yake alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, hebu tueleze endapo watasimama viongozi wetu wakituomba haki zao, na hali wao wanazuia haki zetu, unatuamrisha nini? Mtume akampuuza, kisha akamuuliza, akampuuza, kisha akamuuliza katika mara ya pili au ya tatu, Ash'athi bin Kaisi akamvuta, na akasema: "Wasikilizeni na muwatii, kwani wao wana yao waliyobebeshwa nanyi mna yenu mliyobebeshwa"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu viongozi wanaotaka haki zao kwa watu ikiwemo kusikilizwa na kutiiwa, na wanazuia haki zilizo juu yao; kama kutenda uadilifu na kuwapa watu ngawira na kurejesha mali za dhulma na kufanya usawa, unatuamrisha tufanye nini tukiwa pamoja nao?.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akampuuza; kana kwamba kalichukia swali hili, lakini muulizaji akarudia mara ya pili na ya tatu, Ash'athi bin Kaisi akamvuta muulizaji ili amnyamazishe.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akajibu na akasema: Sikilizeni kauli zao, na mtii amri zao; kwani wana yao waliyobebeshwa na kulazimishwa kuyafanya ikiwemo uadilifu na raia kuwapa haki zao, na nyinyi mna yenu mliyobebeshwa kama kutii na kutimiza haki na kusubiri juu ya mabalaa.
Mafunzo
- Amri ya kusikia na kutii kwa viongozi kwa kila hali katika yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu, hata wasipotekeleza haki za raia.
- Uzembe wa viongozi katika kutimiza wajibu wao, haupelekei watu wengine kufanya uzembe ili kulipiza kisasi katika wajibu wao; kila mmoja ataulizwa juu ya matendo yake, na atahukumiwa kwa uzembe wake.
- Dini haijajengwa katika misingi ya nipe nikupe, bali katika misingi ya kushikamana na yale ya wajibu hata kama mtu mwingine hatotenda haki kwa yale ya wajibu kwake kwa wakati huo, kama ilivyokuja katika hadithi hii.
Marejeo
صحيح مسلم (3/ 1474) (1846).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 719).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 664).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص432).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 553).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن العِرْباضِ بن ساريةَ رضي الله عنه قال: قام فينا رسول الله صلى الله عليه وسلم ذات يوم، فوَعَظَنا مَوعظةً بليغةً وَجِلتْ منها القلوبُ، وذَرَفتْ منها العيونُ، فقيل: يا رسول الله، وعظتَنَا موعظةَ مُودِّعٍ فاعهد إلينا بعهد. فقال: «عليكم بتقوى الله، والسمع والطاعة، وإن عبدًا حبشيًّا، وسترون من بعدي اختلافًا شديدًا، فعليكم بسنتي وسنة الخلفاء الراشدين المهديين، عَضُّوا عليها بالنواجِذ، وإياكم والأمور المحدثات، فإن كل بدعة ضلالة».
Na kutoka kwa Irbadhi bin Sariya -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Siku moja alisimama kwetu sisi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akatupa mawaidha makali mno, nyoyo zilisisimka kwayo, na macho yalibugujikwa machozi, pakasemwa: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Umetuwaidhi mawaidha ya mwenye kuaga, tuachie usia. Akasema: " Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na usikivu na utii, hata kama (mzungumzaji) atakuwa mtumwa tena muhabeshi (Muethiopia), na mtakuja kuona baada yangu hitilafu nyingi, basi shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za makhalifa (watawala) waongofu, zing'ateni (mzikamatilie) kwa magego, na tahadharini sana na mambo ya kuzushwa, kwani kila uzushi ni upotevu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.
Mafunzo
- Umuhimu wa kushikamana na sunna na kuifuata.
- Kuyatilia umuhimu mawaidha na kulainisha nyoyo.
- Amri ya kuwafuata mahalifa wanne waongofu baada yake, nao ni Abuubakari na Omari, na Othman, na Ally radhi za Allah ziwe juu ya wote.
- Katazo la kuzua katika Dini, nakuwa uzushi wote ni upotofu.
- Usikivu na utii kwa atakayesimamia mambo ya waumini katika yale yasiyokuwa maasi.
- Umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati na hali zote.
- Hitilafu lazima itokee katika umma huu, na wakati wa kutokea kwake ni lazima kurejea katika Sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mahalifa waongofu.
Marejeo
الأربعون النووية (ص: 89) (ح28)، سنن أبي داود (7/ 16) (4607)، سنن الترمذي (4/ 408) (2676)، سنن ابن ماجه (1/ 28) (42)، مسند أحمد (28/ 367) (17142)، تحفة الأحوذي (7/ 366)، عون المعبود وحاشية ابن القيم (12/ 235)، شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 278).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ حُذَيْفَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّهَا سَتَكُونُ أُمَرَاءُ يَكْذِبُونَ وَيَظْلِمُونَ، فَمَنْ صَدَّقَهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَأَعَانَهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَلَيْسَ مِنَّي، وَلَسْتُ مِنْهُ، وَلَا يَرِدُ عَلَيَّ الْحَوْضَ، وَمَنْ لَمْ يُصَدِّقْهُمْ بِكَذِبِهِمْ وَلَمْ يُعِنْهُمْ عَلَى ظُلْمِهِمْ فَهُوَ مِنِّي، وَأَنَا مِنْهُ، وَسَيَرِدُ عَلَيَّ الْحَوْضَ».
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika watakuja viongozi wanaosema uongo na kudhulumu (watu), atakayewasadikisha kwa uongo wao na akawasaidia katika dhulma yao basi huyo si katika mimi, na mi si miongoni mwake, na wala hatokunywa katika Hodhi langu, na ambaye hatowaamini kwa uongo wao na akawa hakuwasaidia katika dhulma yao, basi huyo yuko miongoni mwangu, na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu".
Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba watatawala watu baada ya kifo chake viongozi wanaosema uongo katika mazungumzo yao wanasema wasiyoyatenda, na wanadhulumu katika hukumu, atakayeingia kwao na akawasadikisha kwa uongo wao, au akawasaidia kufanya dhulma au kuitamka, kama kutoa majibu kwa lengo la kujipendekeza kwao na kutaraji mazuri waliyonayo; basi mimi niko mbali naye na yeye si miongoni mwangu, wala hatokuja katika Hodhi la mto Kauthari siku ya Kiyama, na ambaye hatoingia kwao na kuwasadikisha kwa uongo wao na kuwasaidia juu ya dhulma yao basi huyo ni miongoni mwangu na mimi ni miongoni mwake, na atakunywa katika Hodhi langu siku ya Kiyama.
Mafunzo
- Watawala watu wakiingia kwao kwa lengo la kuwaelekeza na kuwapa nasaha na kupunguza shari; jambo hili ndilo linalotakiwa, ama wakiingia kwao kwa lengo la kuwasaidia katika dhulma na kuwasadikisha katika uongo hili ndilo jambo baya.
- Kumebainishwa ahadi ya adhabu kali kwa atakayemsaidia kiongozi katika dhulma yake.
- Ahadi hii katika hadithi inaonyesha uharamu wa kitendo hiki, na kuwa ni katika madhambi makubwa.
- Himizo la kusaidizana katika wema na uchamungu, na kutosaidizana katika madhambi na uadui.
- Kumethibitishwa Hodhi kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba Umma wake utakunywa hapo.
Marejeo
مسند أحمد (38/ 295) (23260).
ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (32/ 334).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي نَجِيحٍ العِرْبَاضِ بْنِ سَارِيَةَ رضي الله عنه قَالَ: وَعَظَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مَوْعِظَةً وَجِلَتْ مِنْهَا القُلُوبُ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا العُيُونُ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ! كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ؛ فَأَوْصِنَا، قَالَ: «أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللَّهِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ، وَإِنْ تَأَمَّرَ عَلَيْكُمْ عَبْدٌ، فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ بَعْدِي فَسَيَرَى اخْتِلَافًا كَثِيرًا، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الخُلَفَاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيينَ، عَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الأُمُورِ؛ فَإِنَّ كُلَّ بِدْعَةٍ ضَلَالَةٌ».
Imesimuliwa kutoka kwa Abuu Najihi Al-'Irbat bin Sariya, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ya kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alituaidhi mawaidha makali sana. Nyoyo zikajaa hofu kwa sababu yake, na macho yakamiminika machozi kwa sababu yake, basi tukasema: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni kama kwamba ni mawaidha ya anayeaga. Basi tuusie." Akasema: "Ninawausia kumcha Mwenyezi Mungu, na kusikia na utii, hata kama atakutawaleni mtumwa. Kwani hakika yeyote kati yenu atakayeishi, ataona tofauti nyingi. Kwa hivyo shikamaneni na Sunna yangu na Sunna ya makhalifa wanyoofu waongofu, zikamateni na kuzing'ata kwa magego. Na jihadharini na mambo ya kuzushwa. Kwani kila jambo jipya (katika dini) ni uzushi, na kila uzushi ni upotofu."
Imepokelewa na Abu Daud na TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliwapa mawaidha Masahaba, mawaidha makali, nyoyo ziliogopa kwa mawaidha hayo, na macho yalibugujikwa machozi, Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kana kwamba mawaidha haya ni ya mwenye kuaga, kwa sababu waliona ni jinsi gani alivyokuwa na umakini mkubwa katika mawaidha, wakaomba usia, ili washikamane nao baada yake, akasema: Nakuusieni kumcha Allah Mtukufu, nako ni kwa kutekeleza wajibu na kuacha maharamisho. Na usikivu na utii, yaani: Kwa wenye mamlaka juu yenu, hata kama kiongozi wenu au aliyekutawaleni ni mtumwa, yaani mtu dhalili akawa kiongozi juu yenu, msilibeze hilo, na mtiini, kwa kuchelea kuamsha fitina, bila shaka atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona hitilafu nyingi, Kisha akawabainishia njia ya kutoka katika hitilafu hii, nayo ni kwa kushikamana na sunna yake na sunna za mahalifa wanne waongofu baada yake, Abuubakari Swiddiq, na Omari bin Khattwab, na Othman bin Affan, na Ally bin Abii Twalib, radhi za Allah ziwe juu yao wote, na kuzing'ata kwa magego, yaani meno ya mwisho: Anakusudia kwa kauli hii yaani kufanya bidii katika kubaki katika sunna na kushikamana nazo, Na akawatahadharisha na mambo ya kuzushwa yaliyobuniwa ndani ya Dini, kwani kila uzushi ni upotevu.
Mafunzo
- Umuhimu wa kushikamana na sunna na kuifuata.
- Kuyatilia umuhimu mawaidha na kulainisha nyoyo.
- Amri ya kuwafuata mahalifa wanne waongofu baada yake, nao ni Abuubakari na Omari, na Othman, na Ally radhi za Allah ziwe juu ya wote.
- Katazo la kuzua katika Dini, nakuwa uzushi wote ni upotofu.
- Usikivu na utii kwa atakayesimamia mambo ya waumini katika yale yasiyokuwa maasi.
- Umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati na hali zote.
- Hitilafu lazima itokee katika umma huu, na wakati wa kutokea kwake ni lazima kurejea katika Sunna za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na mahalifa waongofu.
Marejeo
الأربعون النووية (ص: 89) (ح28).
سنن أبي داود (7/ 16) (4607).
سنن الترمذي (4/ 408) (2676).
سنن ابن ماجه (1/ 28) (42).
مسند أحمد (28/ 367) (17142).
تحفة الأحوذي (7/ 366).
عون المعبود وحاشية ابن القيم (12/ 235).
شرح الأربعين النووية للعثيمين (ص: 278).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com