Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kutoka kwa ajili ya kumpinga kiongozi.

Hadithi 5

Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu

عن عُبَادَةَ بن الصَّامتِ رضي الله عنه قال: بَايَعْنَا رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم على السَّمْعِ وَالطَّاعَةِ فِي الْعُسْرِ وَالْيُسْرِ، وَالْمَنْشَطِ وَالْمَكْرَهِ، وعلى أَثَرَةٍ علينا، وعلى أَلَّا نُنَازِعَ الْأَمْرَ أهلَه، وعلى أَنْ نَقُولَ بِالْحَقِّ أينما كُنَّا، لا نَخَافُ في الله لَوْمَةَ لَائِمٍ.
Kutoka kwa Ubaadah bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Tulimpa ahadi ya utiifu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kusikia na kutii katika uzito na wepesi, na yenye kufurahisha na kuchukiza, na kumthamini kuliko nafsi zetu, na tusiwanyang'anye uongozi wanaostahiki, na tusema ukweli mahala popote tuwapo, tusiogope kwa Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumu.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alichukua ahadi na mkataba kutoka kwa Masahaba ya utii kwa wenye mamlaka na watawala katika wepesi na ugumu, na katika hali ya utajiri na umasikini, na sawa sawa amri zao ziwe katika yale wanayoyapenda au kuyachukia, hata kama watawala watajipendelea kuliko raia kwa mali ya umma au vyeo au mengineyo, basi ni wajibu kwao kusikiliza na kutii katika wema, na wasitoke dhidi yao, kwa sababu fitina na ufisadi katika kupigana nao ni mambo makubwa na ni mabaya mno kuliko ufisadi unaotokea kwa sababu ya dhulma zao, na katika mambo waliyoyachukulia kiapo ni waseme kweli mahali popote, wakilitakasa hilo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hawamuogopi mwenye kuwalaumu.

Mafunzo
  1. Matunda ya kusikia na kuwatii viongozi ni kukusanyika kwa nguvu na umoja wa waislamu na kuacha migawanyiko.
  2. Uwajibu wa kusikia na kuwatii wenye mamlaka katika yale yasiyomuasi Mwenyezi Mungu katika hali ya wepesi na uzito, na katika mambo yenye kufurahisha na kuchukiza na kule kujipendelea wanakojipendelea wao.
  3. Uwajibu wa kusema kweli mahala popote tuwapo, bila kuogopa katika jambo la Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulauma.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 47) (7055-7056)، (9/ 77) (7199، 7200). صحيح مسلم (3/ 1470) (1709). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 277). رياض الصالحين، للنووي (ص83) (186). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 419). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 202).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Watakuja watawala, mtayajua baadhi ya matendo yao kuwa yanakwenda sawa na sheria, na mengine mtayakemea (kwa kuwa yako nje ya sheria) atakayelijua hilo ataepukana na dhima, na atakayekemea atasalimika, lakini atakayeridhia na akawafuata

عَنْ أُمِّ سَلَمَةَ أُمِّ المُؤمنين رضي الله عنها: أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: «سَتَكُونُ أُمَرَاءُ فَتَعْرِفُونَ وَتُنْكِرُونَ، فَمَنْ عَرَفَ بَرِئَ، وَمَنْ أَنْكَرَ سَلِمَ، وَلَكِنْ مَنْ رَضِيَ وَتَابَعَ» قَالُوا: أَفَلَا نُقَاتِلُهُمْ؟ قَالَ: «لَا، مَا صَلَّوْا».
Kutoka kwa Ummu Salama mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Watakuja watawala, mtayajua baadhi ya matendo yao kuwa yanakwenda sawa na sheria, na mengine mtayakemea (kwa kuwa yako nje ya sheria) atakayelijua hilo ataepukana na dhima, na atakayekemea atasalimika, lakini atakayeridhia na akawafuata" Wakasema: Kwa nini tusiwapige vita? Akasema: "Hapana, (Msifanye hivyo) madam ni waislamu na wanasimamisha swala".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa tutatawaliwa na viongozi ambao tutayajua baadhi ya matendo yao kuwa yako sawa na yale yanayofahamika ndani ya sheria; na tutayakemea baadhi yake kwa kuwa kwake kinyume na sheria, Atakayechukia moyoni mwake na akawa hakuweza kukemea; basi atakuwa kaondoa dhima ya kupata dhambi na unafiki, Na atakayeweza kukemea kwa mkono au ulimi akawakemea kwa hilo basi atakuwa kasalimika na maasi na kushiriki katika maasi, Lakini atakayeridhia matendo yao na akawafuata ataangamia kama walivyoangamia. Kisha wakamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kwa nini tusiwapige vita viongozi ambao wanasifa kama hizi? Akawakataza wasifanye hivyo, na akasema: Hapana, msifanye hivyo madama wanasimamisha swala kwenu nyinyi.

Mafunzo
  1. Katika alama za utume wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kueleza kwake mambo yatakayotokea miongoni mwa ghaibu na yakatokea kama alivyoeleza.
  2. Haifai kuridhia uovu wala kushiriki ndani yake, na ni lazima kuukemea.
  3. Watakapozua viongozi mambo yanayokwenda kinyume na sheria haitakiwi kuwatii katika hilo.
  4. Kutofaa kujitoa chini ya viongozi wa waislamu; kwakuwa hilo linaambatana na madhara na umwagaji damu na amani kutoweka, kuvumilia uovu wa viongozi watenda maasi, na kusubiri juu ya kero zao, haya ni mepesi kuliko kuvunja amani na kumwaga damu.
  5. Swala ina nafasi kubwa, ndio inayotenganisha kati ya ukafiri na Uislamu.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1480) (1854). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (4/ 64). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (32/ 206). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 279). تطريز رياض الصالحين، لفيصل بن عبد العزيز المبارك (ص150). الشرح الممتع على زاد المستقنع، لابن عثيمين (11/ 323). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 435). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 211).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: «مَنْ ‌خَرَجَ ‌مِنَ ‌الطَّاعَةِ، وَفَارَقَ الْجَمَاعَةَ فَمَاتَ، مَاتَ مِيتَةً جَاهِلِيَّةً، وَمَنْ قَاتَلَ تَحْتَ رَايَةٍ عِمِّيَّةٍ، يَغْضَبُ لِعَصَبَةٍ، أَوْ يَدْعُو إِلَى عَصَبَةٍ، أَوْ يَنْصُرُ عَصَبَةً، فَقُتِلَ، فَقِتْلَةٌ جَاهِلِيَّةٌ، وَمَنْ خَرَجَ عَلَى أُمَّتِي، يَضْرِبُ بَرَّهَا وَفَاجِرَهَا، وَلَا يَتَحَاشَى مِنْ مُؤْمِنِهَا، وَلَا يَفِي لِذِي عَهْدٍ عَهْدَهُ، فَلَيْسَ مِنِّي وَلَسْتُ مِنْهُ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayejitoa katika utiifu, na akasambaratisha umoja akafa, atakuwa amekufa kifo cha zama za ujinga, na atakayepigana chini ya bendera kibubusa anachukia kwa sababu ya ndugu zake, au akahamasisha katika (kupendelea kwa sababu ya) udugu, au ana nusuru udugu, akauwawa, basi hicho ni kifo cha zama za ujinga, na atakayejitoa katika umma wangu, akimpiga mwema wake na muovu wake, na wala hajali muumini wake, na wala hamtimizii mwenye ahadi ahadi yake, basi huyo si miongoni mwangu na mimi si miongoni mwake".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetoka katika kuwatii viongozi, na akaeneza fitina na kuusambaratisha umoja wa Uislamu uliokubaliana juu ya kumtii kiongozi, akafa katika hali hiyo ya faraka na kutomtii kiongozi, atakuwa kafa kifo cha watu wa zama za ujinga, ambao walikuwa hawamtii kiongozi yeyote wala hawajiungi katika kundi moja, bali walikuwa makundi makundi na wabaguzi, wakipigana wao kwa wao. Na akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayepigana chini ya bendera ambayo haiko wazi upande wa haki au batili, anachukia kwa sababu ya ubaguzi wa watu wake au kabila lake, na si kwa kuitetea dini na haki, akapigana kwa ubaguzi pasina kuwa na ujuzi na elimu, akiuawa katika hali hiyo, atakuwa ni sawa na aliye uawa katika zama za ujinga. Nakuwa atakayetoka katika Umma wake -Rehema na amani ziwe juu yake- akimpiga mwema wake, na muovu wake, na wala hajali anayoyafanya na wala haogopi adhabu zake kwa kumuuwa muumini, na wala hawatendei uadilifu makafiri waliochukua ahadi au viongozi, bali anatengua ahadi kwao, jambo hili ni katika madhambi makubwa, atakayelifanya atakuwa amestahiki ahadi hii ya adhabu kali.

Mafunzo
  1. Kuwatii viongozi ni wajibu katika mambo yasiyomuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Kuna tahadhari kubwa kwa aliyetoka katika utiifu kwa kiongozi, na akasambaratisha umoja wa waislamu, akifa katika hali hii, atakuwa amekufa katika njia ya watu wajinga.
  3. Katika hadithi kuna katazo la kupigana vita kwa sababu ya ubaguzi.
  4. Ulazima wa kutimiza makubaliano.
  5. Katika utiifu na kushikamana na umoja kuna heri nyingi, na amani na utulivu, na hali kutengamaa.
  6. Katazo la kujifananisha na watu zama za ujinga.
  7. Amri ya kushikamana na umoja wa waislamu.
Marejeo

صحيح مسلم. شرح النووي على مسلم (12/ 238). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (6/ 179). سبل السلام، لمحمد الصنعاني (2/ 374). منحة العلام شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 338). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (6/ 2395).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni

عن عرفجة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ عَلَى رَجُلٍ وَاحِدٍ، يُرِيدُ أَنْ يَشُقَّ عَصَاكُمْ، أَوْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ، فَاقْتُلُوهُ».
Imepokewa kutoka kwa Farja -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa waislamu watakapokubaliana juu ya kiongozi mmoja, na mshikamano mmoja, kisha akaja anayetaka kumpokonya madaraka, au akataka kuwasambaratisha waislamu kuwafanya kuwa makundi makundi, ni lazima wamzuie na wampige vita, kwa kuzuia shari yake, na kwa kuhifadhi damu za waislamu.

Mafunzo
  1. Ulazima wa kumtii kiongozi anayesimamia mambo ya waislamu, katika mambo yasiyokuwa maasi, na uharamu wa kujitoa dhidi yake.
  2. Atakayejitoa kwa kiongozi wa waislamu na umoja wao, basi ni wajibu kumpiga vita vyovyote vile itakavyokuwa nafasi yake ya cheo au ukoo.
  3. Himizo la kuwa wamoja na kutofarakana na kuhitilafiana.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1480) (1852). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 349). توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، للبسام (6/ 329). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 302). المفاتيح في شرح المصابيح، الحسين المُظْهِري (4/ 295).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika zitatokea fitina, kisha tambueni kuwa fitina ya aliyekaa ndani inanafuu kuliko anayetembea, na anayetembea ndani yake inanafuu kuliko anayeikimbilia,

عَنْ عُثْمَانَ الشَّحَّامِ، قَالَ: انْطَلَقْتُ أَنَا وَفَرْقَدٌ السَّبَخِيُّ إِلَى مُسْلِمِ بْنِ أَبِي بَكْرَةَ وَهُوَ فِي أَرْضِهِ، فَدَخَلْنَا عَلَيْهِ فَقُلْنَا: هَلْ سَمِعْتَ أَبَاكَ يُحَدِّثُ فِي الْفِتَنِ حَدِيثًا؟ قَالَ: نَعَمْ، سَمِعْتُ أَبَا بَكْرَةَ رضي الله عنه يُحَدِّثُ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّهَا سَتَكُونُ فِتَنٌ، أَلَا ثُمَّ تَكُونُ فِتْنَةٌ الْقَاعِدُ فِيهَا خَيْرٌ مِنَ الْمَاشِي فِيهَا، وَالْمَاشِي فِيهَا خَيْرٌ مِنَ السَّاعِي إِلَيْهَا، أَلَا فَإِذَا نَزَلَتْ أَوْ وَقَعَتْ فَمَنْ كَانَ لَهُ إِبِلٌ فَلْيَلْحَقْ بِإِبِلِهِ، وَمَنْ كَانَتْ لَهُ غَنَمٌ فَلْيَلْحَقْ بِغَنَمِهِ، وَمَنْ كَانَتْ لَهُ أَرْضٌ فَلْيَلْحَقْ بِأَرْضِهِ»، قَالَ فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ أَرَأَيْتَ مَنْ لَمْ يَكُنْ لَهُ إِبِلٌ وَلَا غَنَمٌ وَلَا أَرْضٌ؟ قَالَ: «يَعْمِدُ إِلَى سَيْفِهِ فَيَدُقُّ عَلَى حَدِّهِ بِحَجَرٍ، ثُمَّ لِيَنْجُ إِنِ اسْتَطَاعَ النَّجَاءَ، اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟ اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟ اللهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ؟»، قَالَ: فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ أَرَأَيْتَ إِنْ أُكْرِهْتُ حَتَّى يُنْطَلَقَ بِي إِلَى أَحَدِ الصَّفَّيْنِ، أَوْ إِحْدَى الْفِئَتَيْنِ، فَضَرَبَنِي رَجُلٌ بِسَيْفِهِ، أَوْ يَجِيءُ سَهْمٌ فَيَقْتُلُنِي؟ قَالَ: «يَبُوءُ بِإِثْمِهِ وَإِثْمِكَ، وَيَكُونُ مِنْ أَصْحَابِ النَّارِ».
Kutoka kwa Othman As Shaham, amesema:Niliondoka mimi pamoja na Farqad As Sabakhi kwenda kwa Muslim bin Abii Bakara naye akiwa katika mji wake, tukaingia kwake na tukasema: Hivi uliwahi kumsikia baba yako akisimulia hadithi yoyote kuhusu fitina? Akasema: Ndiyo, Nilimsikia Abuu Bakra radhi za Allah ziwe juu yake akihadithia, akasema: Alisema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika zitatokea fitina, kisha tambueni kuwa fitina ya aliyekaa ndani inanafuu kuliko anayetembea, na anayetembea ndani yake inanafuu kuliko anayeikimbilia, tambueni itakapoteremka au ikatokea basi atakayekuwa na ngamia basi na amfuate ngamia wake, na atakayekuwa na mbuzi basi na amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi basi na aende katika ardhi yake", anasema, akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa mtu hana ngamia wala mbuzi wala ardhi? Akasema: "Basi achukue panga lake na apige upande wa makali yake katika jiwe, kisha aokoke akiweza kuokoka, ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha? ewe Allah je nimefikisha?" Akasema: Akasema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje endapo nitalazimishwa mpaka nikapelekwa katika moja kati ya safu mbili, au moja kati ya makundi mawili, mtu mmoja akanipiga kwa panga lake, au ukanilenga mshale ukaniua? Akasema: "Yeye ndiye atakayebeba dhambi zake na dhambi zako, na atakuwa miongoni mwa watu wa motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Othman Ash Shaham na Farqad As-Sabakhi walimuuliza Muslim mtoto wa Swahaba mtukufu Abuubakra radhi za Allah ziwe juu yake: Je alisikia kutoka kwa baba yake hadithi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika fitina na vita itakayotokea baina ya waislamu? Akasema: Naam, alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba itatokea fitina baada ya kifo chake, na fitina hii aliyekaa na kughafilika nayo ni bora kuliko anayetembea ndani yake, na anaitafuta pasina kujua, na anayetembea ndani yake ni bora kuliko anayekwenda mbio kuiendea na kuitafuta na kushiriki ndani yake. Kisha akaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake itakayeshuka na kufika fitina katika zama zake na kwake kukapatikana upenyo atakaokimbilia; atakayekuwa na ngamia anayechunga basi aifuate ngamia yake, na atakayekuwa na mbuzi anayechunga basi amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi na shamba basi aende shambani kwake. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hivi wasemaje kwa mtu ambaye hatokuwa na makimbilio kama ngamia wala mbuzi wala shamba? Akasema: Basi aende akachukue silaha yake aipige na ailainishe, kisha akimbie na ajinusuru yeye na mwanaye ikiwa ataweza kuokoka. Kisha akataka ushuhuda rehema na amani ziwe juu yake mara tatu, akasema: Ewe Allah je, nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha?. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa nitalazimishwa kushiriki pamoja na safu moja, au moja kati ya makundi mawili, akanipiga mtu kwa panga lake, au mshale ukanilenga ukaniuwa?. Akasema: Atarudi na madhambi yake na madhambi ya aliyemuuwa, na siku ya Kiyama atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.

Mafunzo
  1. Habari ya kutokea fitina na tahadhari dhidi yake, na ili watu wajiandae nayo, wasijiingize ndani yake, na wamuombe Mwenyezi Mungu subira na kuokoka dhidi ya shari zake.
  2. Amesema Nawawi: Kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Aliyekaa ndani yake ni bora kuliko aliyesimama", mpaka mwisho wake, maana yake ni kubainishwa hatari yake, na himizo la kuiepuka, na kuikimbia, na kwamba shari yake na fitina yake inakuwa kulingana na namna mtu alivyofungamana nayo.
  3. Amesema Nawawi: Kumeondolewa dhambi kwa aliyelazimishwa atakayehudhuria huko, na ama kuuwa si halali hata kwa kulazimishwa, bali aliyelazimishwa anapata dhambi kwa lile aliloamrishwa kwa makubaliano ya wanachuoni wote.
  4. Amesema bin Hajari: Na wamesema wengine: Likifanya dhulma kundi likatoka kwa kiongozi likakataa kutekeleza wajibu wake na likaanzisha vita basi ni wajibu kulipiga vita, na vile vile yakipigana makundi mawili ni wajibu kwa kila mwenye kuweza kumzuia mkosefu na kumtetea aliyepigwa, na hii ndio kauli ya jopo la wanachuoni, na wamefafanua wengine, wakasema: Kila mapigano yatakayotokea kati ya makundi mawili ya waislamu kiasi kwamba hakuna kiongozi wa umma, basi hapo mapigano hayo ni marufuku, na zinashuka hadithi zote zilizopo katika mlango huu na nyinginezo.
  5. Amesema Nawawi: Na wametofautiana wanachuoni katika mapigano ya fitina, kundi miongoni mwao wakasema: Hakuna kupigana katika fitina ya waislamu, hata wakiingia ndani ya nyumba yake, na wakataka kumuuwa, hairuhusiwi kwake kujihami; kwa sababu kamtaka hilo kwa ufahamu potofu, na hii ni kauli ya Abii Bakra Swahaba radhi za Allah ziwe juu yake na wengineo, na amesema bin Omari na Imrani bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yao: Haingii hapa, lakini akikusudia kujihami, kauli zote hizi mbili zimeafikiana juu ya kuacha kuingia katika fitina zote za Uislamu. Na wamesema Maswahaba wengi na wanafunzi wao na wanachuoni wote wa Uislamu: Ni wajibu kumtetea mwenye haki katika fitina, na kusimama naye kwa kupigana na adui jeuri, kama alivyosema Mtukufu: "Basi lipigeni kundi linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." mpaka mwisho wa aya, na kauli hii ndiyo sahihi, na hadithi hii inafasiriwa kwa yule ambaye hajabainikiwa na haki, au juu ya makundi mawili dhalimu, na hakuna lolote lililoelewa vibaya aya au hadithi miongoni mwao.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2212) (2887). النهاية في غريب الحديث والأثر (91). شرح سنن أبي داود للعباد (478/ 3).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com