Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa waislamu watakapokubaliana juu ya kiongozi mmoja, na mshikamano mmoja, kisha akaja anayetaka kumpokonya madaraka, au akataka kuwasambaratisha waislamu kuwafanya kuwa makundi makundi, ni lazima wamzuie na wampige vita, kwa kuzuia shari yake, na kwa kuhifadhi damu za waislamu.
- Ulazima wa kumtii kiongozi anayesimamia mambo ya waislamu, katika mambo yasiyokuwa maasi, na uharamu wa kujitoa dhidi yake.
- Atakayejitoa kwa kiongozi wa waislamu na umoja wao, basi ni wajibu kumpiga vita vyovyote vile itakavyokuwa nafasi yake ya cheo au ukoo.
- Himizo la kuwa wamoja na kutofarakana na kuhitilafiana.
صحيح مسلم (3/ 1480) (1852). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 349). توضيح الأحكام شرح بلوغ المرام، للبسام (6/ 329). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 302). المفاتيح في شرح المصابيح، الحسين المُظْهِري (4/ 295).