Othman Ash Shaham na Farqad As-Sabakhi walimuuliza Muslim mtoto wa Swahaba mtukufu Abuubakra radhi za Allah ziwe juu yake: Je alisikia kutoka kwa baba yake hadithi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika fitina na vita itakayotokea baina ya waislamu? Akasema: Naam, alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba itatokea fitina baada ya kifo chake, na fitina hii aliyekaa na kughafilika nayo ni bora kuliko anayetembea ndani yake, na anaitafuta pasina kujua, na anayetembea ndani yake ni bora kuliko anayekwenda mbio kuiendea na kuitafuta na kushiriki ndani yake. Kisha akaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake itakayeshuka na kufika fitina katika zama zake na kwake kukapatikana upenyo atakaokimbilia; atakayekuwa na ngamia anayechunga basi aifuate ngamia yake, na atakayekuwa na mbuzi anayechunga basi amfuate mbuzi wake, na atakayekuwa na ardhi na shamba basi aende shambani kwake. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hivi wasemaje kwa mtu ambaye hatokuwa na makimbilio kama ngamia wala mbuzi wala shamba? Akasema: Basi aende akachukue silaha yake aipige na ailainishe, kisha akimbie na ajinusuru yeye na mwanaye ikiwa ataweza kuokoka. Kisha akataka ushuhuda rehema na amani ziwe juu yake mara tatu, akasema: Ewe Allah je, nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha? Ewe Allah je nimefikisha?. Bwana mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wasemaje ikiwa nitalazimishwa kushiriki pamoja na safu moja, au moja kati ya makundi mawili, akanipiga mtu kwa panga lake, au mshale ukanilenga ukaniuwa?. Akasema: Atarudi na madhambi yake na madhambi ya aliyemuuwa, na siku ya Kiyama atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.
- Habari ya kutokea fitina na tahadhari dhidi yake, na ili watu wajiandae nayo, wasijiingize ndani yake, na wamuombe Mwenyezi Mungu subira na kuokoka dhidi ya shari zake.
- Amesema Nawawi: Kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Aliyekaa ndani yake ni bora kuliko aliyesimama", mpaka mwisho wake, maana yake ni kubainishwa hatari yake, na himizo la kuiepuka, na kuikimbia, na kwamba shari yake na fitina yake inakuwa kulingana na namna mtu alivyofungamana nayo.
- Amesema Nawawi: Kumeondolewa dhambi kwa aliyelazimishwa atakayehudhuria huko, na ama kuuwa si halali hata kwa kulazimishwa, bali aliyelazimishwa anapata dhambi kwa lile aliloamrishwa kwa makubaliano ya wanachuoni wote.
- Amesema bin Hajari: Na wamesema wengine: Likifanya dhulma kundi likatoka kwa kiongozi likakataa kutekeleza wajibu wake na likaanzisha vita basi ni wajibu kulipiga vita, na vile vile yakipigana makundi mawili ni wajibu kwa kila mwenye kuweza kumzuia mkosefu na kumtetea aliyepigwa, na hii ndio kauli ya jopo la wanachuoni, na wamefafanua wengine, wakasema: Kila mapigano yatakayotokea kati ya makundi mawili ya waislamu kiasi kwamba hakuna kiongozi wa umma, basi hapo mapigano hayo ni marufuku, na zinashuka hadithi zote zilizopo katika mlango huu na nyinginezo.
- Amesema Nawawi: Na wametofautiana wanachuoni katika mapigano ya fitina, kundi miongoni mwao wakasema: Hakuna kupigana katika fitina ya waislamu, hata wakiingia ndani ya nyumba yake, na wakataka kumuuwa, hairuhusiwi kwake kujihami; kwa sababu kamtaka hilo kwa ufahamu potofu, na hii ni kauli ya Abii Bakra Swahaba radhi za Allah ziwe juu yake na wengineo, na amesema bin Omari na Imrani bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yao: Haingii hapa, lakini akikusudia kujihami, kauli zote hizi mbili zimeafikiana juu ya kuacha kuingia katika fitina zote za Uislamu. Na wamesema Maswahaba wengi na wanafunzi wao na wanachuoni wote wa Uislamu: Ni wajibu kumtetea mwenye haki katika fitina, na kusimama naye kwa kupigana na adui jeuri, kama alivyosema Mtukufu: "Basi lipigeni kundi linalodhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu..." mpaka mwisho wa aya, na kauli hii ndiyo sahihi, na hadithi hii inafasiriwa kwa yule ambaye hajabainikiwa na haki, au juu ya makundi mawili dhalimu, na hakuna lolote lililoelewa vibaya aya au hadithi miongoni mwao.
صحيح مسلم (4/ 2212) (2887). النهاية في غريب الحديث والأثر (91). شرح سنن أبي داود للعباد (478/ 3).