عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «سَتَكُونُ أَثَرَةٌ وَأُمُورٌ تُنْكِرُونَهَا» قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ فَمَا تَأْمُرُنَا؟ قَالَ: «تُؤَدُّونَ الحَقَّ الَّذِي عَلَيْكُمْ، وَتَسْأَلُونَ اللَّهَ الَّذِي لَكُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika utakuja kutokea uchoyo na kujipendelea baada yangu na mambo msiyoyajua (uzushi)" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu unatuamrisha nini? Akasema: "Mtekeleze haki ya wajibu kwenu, na mumuombe Allah haki yenu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa waislamu watatawaliwa na viongozi watakaohodhi na kujipendelea mali za waislamu na mambo mengine mengi yasiyokuwa mali, watazitumia kama watakavyo, na watawanyima waislamu haki yao katika mali hizo. Na watakuwa na mambo ndani ya dini mtakayoyakataa kuwa si katika dini. Masahaba Radhi za Allah ziwe juu yao wakauliza: Ni nini watafanya katika hali kama hiyo? Akawaeleza Rehema na amani ziwe juu yake kuwa kusikuzuieni kule kuhodhi kwao mali na kujipendelea kwao, nanyi mkaacha kufanya wajibu wenu kwao, ikiwemo usikivu na utii, bali kuweni na subira na mtii msiwaletee upinzani katika madaraka, na haki yenu iombeni kutoka kwa Allah, na awarekebishe na azuie shari zao na dhulma zao.
Mafunzo
- Hadithi hii ni katika dalili za utume wake Rehema na amani ziwe juu yake, kiasi ambacho alieleza mambo yatakayotokea ndani ya Umma wake na yakatokea kama alivyoeleza.
- Inafaa kumueleza mtahiniwa yale yatakayomsibu katika mitihani; ili aitulize nafsi yake, mtihani ukimfika atakuwa na subira na atataraji malipo toka kwa Allah.
- Kushikamana na Qur'ani na Sunna ni sababu ya kutoka katika fitina na hitilafu.
- Himizo la kuwa wasikivu na watiifu kwa viongozi katika mema, na kutojitoa katika utiifu, hata kama zitatokea kwao dhulma.
- Kutumia hekima na kufuata mafundisho ya Mtume wakati wa fitina.
- Ni jukumu la kila mtu kutimiza haki ya msingi inayomlazimu hata kama itatokea kadhulumiwa.
- Hadithi inaashiria kanuni ya msingi ambayo ni: Mtu kuchagua moja kati ya shari mbili au madhara yenye nafuu.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 199) (3603).
صحيح مسلم (3/ 1472) (1843).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 720).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص52).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (9/ 402).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 280).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 554).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي حُمَيْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: اسْتَعْمَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا عَلَى صَدَقَاتِ بَنِي سُلَيْمٍ، يُدْعَى ابْنَ اللُّتْبِيَّةِ، فَلَمَّا جَاءَ حَاسَبَهُ، قَالَ: هَذَا مَالُكُمْ وَهَذَا هَدِيَّةٌ. فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَهَلَّا جَلَسْتَ فِي بَيْتِ أَبِيكَ وَأُمِّكَ، حَتَّى تَأْتِيَكَ هَدِيَّتُكَ إِنْ كُنْتَ صَادِقًا» ثُمَّ خَطَبَنَا، فَحَمِدَ اللَّهَ وَأَثْنَى عَلَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: «أَمَّا بَعْدُ، فَإِنِّي أَسْتَعْمِلُ الرَّجُلَ مِنْكُمْ عَلَى العَمَلِ مِمَّا وَلَّانِي اللَّهُ، فَيَأْتِي فَيَقُولُ: هَذَا مَالُكُمْ وَهَذَا هَدِيَّةٌ أُهْدِيَتْ لِي، أَفَلاَ جَلَسَ فِي بَيْتِ أَبِيهِ وَأُمِّهِ حَتَّى تَأْتِيَهُ هَدِيَّتُهُ، وَاللَّهِ لاَ يَأْخُذُ أَحَدٌ مِنْكُمْ شَيْئًا بِغَيْرِ حَقِّهِ إِلَّا لَقِيَ اللَّهَ يَحْمِلُهُ يَوْمَ القِيَامَةِ، فَلَأَعْرِفَنَّ أَحَدًا مِنْكُمْ لَقِيَ اللَّهَ يَحْمِلُ بَعِيرًا لَهُ رُغَاءٌ، أَوْ بَقَرَةً لَهَا خُوَارٌ، أَوْ شَاةً تَيْعَرُ» ثُمَّ رَفَعَ يَدَهُ حَتَّى رُئِيَ بَيَاضُ إِبْطِهِ، يَقُولُ: «اللَّهُمَّ هَلْ بَلَّغْتُ» بَصْرَ عَيْنِي وَسَمْعَ أُذُنِي.
Kutoka kwa Abuu Humaid Assaaidi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja ya kukusanya Zaka kutoka kwa Banii Suleim, akiitwa bin Lutbia, alipokuja akampa mahesabu, akasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako, mpaka zawadi zikujie ikiwa wewe ni mkweli" Kisha akatuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: "Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni mwenu miongoni mwa kazi alizonikabidhi Mwenyezi Mungu, kisha baadaye anakuja anasema: Hii ndio mali yenu na hii ni zawadi yangu niliyopewa, kwa nini asingelikaa nyumbani kwa baba yake na mama yake mpaka zawadi yake imfuate, Wallah hatochukua chochote yeyote miongoni mwenu pasina haki yake, isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa amekibeba alichochukua siku ya Kiyama, na namuapa Mwenyezi Mungu nitakuja kumtambua mmoja wenu aliyekutana na Mwenyezi Mungu akiwa kabeba Ngamia akitoa mlio, au Ng'ombe akitoa mroromo, au Mbuzi akitoa mlio" Kisha akanyanyua mkono wake mpaka ukaonekana weupe wa kwapa lake, huku akisema: "Ewe Mwenyezi Mungu, je, nimefikisha" Limeona jicho langu na limesikia sikio lango.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alimpa kazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake bwana mmoja akiitwa: Bin Lutbia ya kukusanya Zaka kutoka katika kabila la Bani Suleim, aliporejea Madina akampa mahesabu ya mali aliyokusanya na aliyotumia, akasema bin Lutbia: Hii ndio mali yenu niliyoikusanya kutoka katika Zaka, na mali hii nimepewa zawadi mimi. Akasema rehema na amani ziwe juu yake kumwambia: Hivi si ungelikaa nyumbani kwa baba yako na mama yako ili uone je utapewa zawadi ikiwa wewe ni mkweli; kwani hakika haki ulizozifanyia kazi ndio sababu ya kupewa kwako zawadi, na kwamba lau ungekaa nyumbani kwako usingezawadiwa chochote, hupaswi kuihalalisha kwakuwa tu imekufikia kwa njia ya zawadi. Kisha akapanda Mimbari rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili ya kuhutubia huku akiwa na hasira, akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu, kisha akasema: Ama baada ya hayo, hakika mimi ninampa kazi mtu miongoni kama mfanya kazi na muajiriwa katika kile ambacho Mwenyezi Mungu kanipa maamuzi ndani yake miongoni mwa Zaka na Ngawira, kisha anakuja kutoka katika kazi yake na anasema: Hii ni yenu na hii ni zawadi yangu nimezawadiwa! Kwa nini asikae nyumbani kwa baba yake na mama yake ili zawadi yake imfuate, Wallah, namuapa Mwenyezi Mungu, hatochukua yeyote chochote katika vile anavyopewa isipokuwa atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kakibeba siku ya Kiyama juu ya shingo yake, ikiwa alichokichukua ni Ngamia mwenye sauti, au Ng'ombe mwenye sauti ya mroromo, au mbuzi mwenye mlio, basi atapiga kelele. Kisha akanyanyua mikono yake kwa kasi mpaka waliokaa wakaona weupe wa kwapa lake, kisha akasema: Shuhudieni kuwa nimefikisha hukumu ya Mwenyezi Mungu kwenu. Kisha Abuu Humaidi Assaaidi akaeleza radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Kuwa haya ni miongoni mwa mambo ambayo macho yake yaliyashuhudia na masikio yake yakayasikia.
Mafunzo
- Inatakiwa kwa Hakimu kuwabainishia anaofanya nao kazi wajibu wao na yasiyotakiwa katika kazi zao.
- Ahadi kali kwa anayechukua mali za watu kwa dhulma.
- Hakuna atakayedhulumu isipokuwa atakuja na kila alichodhulumu siku ya Kiyama.
- La wajibu kwa muajiriwa katika kazi yoyote miongoni mwa kazi za nchi atimize majukumu aliyopewa, na hatakiwi kuchukua zawadi katika kile kinachohusiana na kazi yake, na akichukua basi akiweke katika benki ya Waislamu, na haifai kuichukua kwa matumizi yake binafsi, kwa sababu hilo ni njia ya kwenda katika shari na kupoteza amana.
- Amesema bin Battwal: Hadithi imeonyesha kuwa zawadi kwa mfanya kazi inakuwa ni shukurani kwa wema wake, au kwa ajili ya kujipendekeza kwake, au kumtaka asitende haki, akaashiria Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa anachozawadiwa yeye katika hivyo yuko sawa na Waislamu wengine, hana ubora kuliko wao katika hicho, na kwamba haifai kujipendelea.
- Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii: Kumebainishwa kuwa zawadi zote za wafanya kazi ni haramu na ni wizi; kwa sababu atakuwa kafanya hiana katika uongozi wake na amana yake, na ndio maana akataja katika hadithi katika adhabu yake na kumbebesha kwake kile alichozawadiwa siku ya Kiyama, kama alivyotaja mfano kwa mwenye kuficha mali, na amebainisha rehema na amani ziwe juu yake katika hadithi hii sababu ya kuharamisha zawadi, ambayo ni uongozi, kinyume na zawadi ya mtu ambaye si mfanya kazi, kwani hiyo inafaa kuchukua.
- Amesema bin Munir: Inachukuliwa katika kauli yake: "kwa nini asingekaa nyumbani kwa baba yake na mama yake" Kuwa inafaa kupokea zawadi kutoka kwa yule aliyekuwa akimpa zawadi kabla ya hapo, amesema bin Hajar: Na haifichikani kuwa mahali pake nikuwa isizidi kiwango cha kawaida.
- Mfumo wa Mtume katika utoaji wa nasaha, ni kuzungumza kwa watu wote, na si kumtangaza mtu.
- Amesema bin Hajari: Hapa inaonyesha kuwa ni sheria kumkagua aliyepewa dhamana.
- Amesema bin Hajari: Na inaonyesha kuwa inafaa kumkemea aliyekosea.
- Inapendeza kunyanyua mikono katika dua.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 28) (6979).
صحيح مسلم (3/ 1463) (1832).
جمهرة اللغة، أبوبكر الأزدي (2/ 1067).
المعجم الوسيط، مجمع اللغة العربية (2/ 1065).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 305).
تطرز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص166).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 234).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ عُمرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «كُلُّكُمْ رَاعٍ فَمَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ، فَالأَمِيرُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ، وَالرَّجُلُ رَاعٍ عَلَى أَهْلِ بَيْتِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُمْ، وَالمَرْأَةُ رَاعِيَةٌ عَلَى بَيْتِ بَعْلِهَا وَوَلَدِهِ وَهِيَ مَسْئُولَةٌ عَنْهُمْ، وَالعَبْدُ رَاعٍ عَلَى مَالِ سَيِّدِهِ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْهُ، أَلاَ فَكُلُّكُمْ رَاعٍ وَكُلُّكُمْ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ».
Kutoka kwa Abdillah Bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao: Yakwamba Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake- amesema: "Kila mmoja miongoni mwenu ni mchunga hivyo ataulizwa kuhusu raia wake, kiongozi anayewaongoza watu ni mchunga naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mwanaume ni mchunga kwa watu wa nyumbani kwake naye ndiye wa kuulizwa kuhusu wao, na mwanamke ni mchunga katika nyumba ya mumewe na watoto wake naye ndiye atakayeulizwa kuhusu wao, na mja ni mchunga juu ya mali ya bosi wake, naye ndiye atakayeulizwa juu ya mali hiyo, tambueni kuwa kila mmoja kati yenu ni mchunga na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume rehema na amani zimfikie kuwa kila muislamu katika jamii anamajukumu anayoyasimamia na anayoyabeba, Imamu na kiongozi ni mchunga katika majukumu aliyopewa na Allah kuyasimamia, anatakiwa kuhifadhi sheria zao, na kuwalinda dhidi ya mwenye kuwafanyia uadui, na kumpiga vita adui yao, na kutopoteza haki zao, Na mwanaume kwa watu wa nyumba yake amelazimishwa kuwasimamia kwa matumizi, na kuishi nao vizuri, na kuwasomesha na kuwaadabisha, Na mwanamke katika nyumba ya mumewe ni mchunga kwa kuipangilia vizuri nyumba yake, na kuwalea watoto wake, naye ataulizwa kuhusu hilo, Na mfanyakazi mmilikiwa na mwajiriwa ataulizwa katika mali ya bosi wake kwa kusimamia kuhifadhi kile kilicho mkononi mwake, na huduma zake, naye ataulizwa kuhusu hilo, kila mmoja ni mchunga katika vile alivyopewa kuvichunga, na kila mmoja ataulizwa kuhusu raia wake.
Mafunzo
- Majukumu katika jamii ya kiislamu ni ya watu wote, na kila mmoja ni kulingana na nafasi yake na uwezo wake na majukumu yake.
- Ukubwa wa majukumu ya mwanamke, na hii ni kwa kusimamia haki za nyumba ya mume wake na majukumu yake kwa watoto wake.
Marejeo
صحيح البخاري (3/ 150) (2554).
صحيح مسلم (3/ 1459) (1829).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 369).
إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، القسطلاني (4/ 326).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي رُقَيَّةَ تَمِيمِ بْنِ أَوْسٍ الدَّارِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ruqaiyya Tamim Ausi Ad-dari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa dini imesimama katika msingi wa utakasifu wa nia na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu kikamilifu pasina mapungufu au udanganyifu. Pakasemwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Zinakuwa kwa nani nasaha? Akasema: Kwanza: Nasaha ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kutukuza amri zake, na kuwaita watu kuja katika kumuamini. Pili: Nasaha kwa ajili ya kitabu chake ambacho ni Qur'ani tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, na kwamba kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza na kukisoma haswa ipasavyo, na tunazifanyia kazi aya zake,zilizo wazi na tunazikubali zenye kutatiza na tunapingana na tafsiri mbaya ya wenye kuzipotosha, na tunachukua mazingatio kwa mawaidha yake, na kuisambaza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo. Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake: Kwa sisi kuitakidi kuwa yeye ni mwisho wa Mitume, na kumuamini kwa yale aliyokuja nayo, na tutekeleza amri yake, na tuepuke makatazo yake, na tusimuabudu Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tunaitukuza na tunaiheshimu, na tunautangaza ujumbe wake, na kuisambaza sheria yake, na kupinga tuhuma zote dhidi yake. Nne: Nasaha kwa viongozi wa Waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika kumtii Mwenyezi Mungu. Tano: Nasaha kwa Waislamu: Kwa kuwatendea wema na kuwalingania, na kuacha kuwaudhi, na kuwapendelea heri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.
Mafunzo
- Amri ya kunasihiana ni kwa watu wote.
- Ukubwa na utukufu wa nafasi ya nasaha katika dini.
- Dini imekusanya mambo ya itikadi, maneno, na matendo.
- Miongoni mwa nasaha ni kujinasihi mwenyewe kutomfanyia udanganyifu yule mwenye kunasihiwa pamoja na kumtakia kheri.
- Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba anataja jambo kwa ujumla kisha analifafanua.
- Kuanza na lenye umuhimu zaidi kisha linalofuata, kwani alianza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha kitabu chake, kisha Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kisha viongozi wa waislamu, kisha watu wote kwa ujumla.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 74) (55).
التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثا النووية (ص21).
شرح الأربعين النووية، لابن عثيمين (ص115).
شرح النووي على مسلم (2/ 37).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com