Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo

عن مَعقِلِ بن يَسار المُزَنِيّ رضي الله عنه قال: إني سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللهُ رَعِيَّةً، يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ، إِلَّا حَرَّمَ اللهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ».
Kutoka kwa Ma'akali bin Yasaari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Hakika mimi nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakuna mja yeyote atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia, akafa siku atakayokufa hali yakuwa aliwafanyia udanganyifu raia wake, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamharamishia pepo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila mtu ambaye Mwenyezi Mungu atamfanya kuwa ni msimamizi au kiongozi kwa watu, sawa sawa uwe ni uongozi wa umma, kama Raisi au usimamizi wa sekta binafsi kama mtu katika nyumba yake na mwanamke katika nyumba yake, akafanya uzembe kutekeleza haki za raia wake, na akawafanyia udanganyifu na wala hakuwanasihi, akapoteza haki zao za kidini na kidunia, huyu atakuwa kastahiki adhabu hii kali.

Mafunzo
  1. Adhabu hii si maalum kwa kiongozi mkuu na wasaidizi wake, bali inajumuisha kila atakayepewa usimamizi na Mwenyezi Mungu kwa raia.
  2. Wajibu kwa kila atakayesimamia lolote katika mambo ya waislamu awanasihi, na ajitahidi kutimiza amana, na atahadhari na hiyana.
  3. Ukubwa wa majukumu kwa kila atakayewasimamia raia kwa umma au binafsi, sawa majukumu yawe madogo au makubwa.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 64) (7150). صحيح مسلم (1/ 125) (142). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 706). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 488). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 543).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Siasa ya Kisheria.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com