Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Masharti ya uongozi mkuu.

Hadithi 2

Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie

عن عائشة رضي الله عنها قالت: سمعتُ من رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول في بيتي هذا: «اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئًا فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ».
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema ndani ya nyumba yangu hii: "Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alimuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila atakayesimamia jambo katika mambo ya waislamu liwe dogo au kubwa, sawa sawa usimamizi huu uwe ni wa umma, au sekta binafsi, na akawaingizia tabu na hakuwahurumia, kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amlipe kutokana na matendo yake, kwa kumtia matatizo na yeye. Nakuwa atakaye wahurumia na wakawafanyia wepesi, na akawarahisishia mambo yao basi Mwenyezi Mungu naye amuhurumie na ampe wepesi katika mambo yake.

Mafunzo
  1. Ni wajibu kwa kila atakayesimamia lolote katika mambo ya waislamu awahurumie kiasi awezavyo.
  2. Malipo huendana na matendo.
  3. Mzani unaozingatiwa katika upole au ukali nikuwa usiende kinyume na Qur'ani na Sunna.
Marejeo

صحيح مسلم (3/ 1458) (1828). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 367). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 224). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 419).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hawatofanikiwa watu waliomkabidhi utawala wao mwanamke

عَنْ أَبِي بَكْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لَنْ يُفْلِحَ قَوْمٌ وَلَّوْا أَمْرَهُمُ امْرَأَةً».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Bakra -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hawatofanikiwa watu waliomkabidhi utawala wao mwanamke".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hawatofanikiwa watu kwa kupata wanayoyataka pindi watakapomtawalisha na kummilikisha mwanamke swala la hukumu au usimamizi wa dola au wizara.

Mafunzo
  1. Wanawake hawasimamii uongozi wala hukumu kwa watu, na mfano wa hayo katika usimamizi wa majukumu makuu, ama mambo maalumu kama usimamizi wa mali za wakfu au mayatima au ukuu wa shule na mfano wa hayo hakuna tatizo.
  2. Kumebainishwa udhaifu mkubwa wa mwanamke, na kwamba hashirikiani na wanaume katika usimamizi mkuu, na kwamba kusimamia kwake mfano wa majukumu hayo ni sababu ya kukosa mafanikio.
  3. Mwenyezi Mungu alimuumba mwanamke, na akamuwekea tabia zinazotofautiana na tabia za mwanaume, kuna mambo hayafai kusimamiwa na mwanamke; kulingana na tabia yake ya kipekee, vile vile kuna mambo hayafai kusimamiwa na mwanaume; kulingana na tabia yake ya kipekee.
  4. Kufanikiwa kulikokanushwa: Ni kufanikiwa kuliko tajwa katika ulimi wa sheria, nako ni kupatikana kwa kheri za dunia na akhera, na haimaanishi ustawi wa ufalme kuwa watu wanampendeza Mwenyezi Mungu, yeyote asiyemtii Mwenyezi Mungu si miongoni mwa waliofanikiwa, hata kama yuko katika hali nzuri zaidi katika kile kinachoonekana miongoni mwa mambo yake ya kidunia.
  5. Hakuna maana yoyote ya kumshusha hadhi mwanamke katika hadithi hii, lakini ni maelekezo ya uwezo wake sahihi unaomfaa kwake.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 8) (4425). عمدة القاري شرح صحيح البخاري، لبدر الدين العيني (14/ 210). أعلام الحديث (شرح صحيح البخاري) لأبي سليمان الخطابي (3/ 1787). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 183). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (2/ 268). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (3/ 441). ذخيرة العقبى في شرح المجتبى، للولوي (1/ 82). كشف المشكل من حديث الصحيحين، لابن الجوزي (2/ 16).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com