Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adabu za kutoa salamu na kubisha Hodi.

Hadithi 9

Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا انْتَهَى أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَجْلِسِ فَلْيُسَلِّمْ، فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَقُومَ فَلْيُسَلِّمْ، فَلَيْسَتِ الْأُولَى بِأَحَقَّ مِنَ الْآخِرَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekuja mahali walipokaa watu basi awasalimie, na akitaka kunyanyuka basi awaage jamaa zake pia kwa salamu; kwani salamu ya kwanza wakati wa kuja si bora sana kuliko salamu ya mwisho wakati wa kuondoka.

Mafunzo
  1. Himizo la kusambaza salamu.
  2. Himizo la kuwasalimia jamaa waliokaa wakati wa kukutana nao na wakati wa kuondoka.
  3. Amesema Assanadi: Kauli yake: "Na akitaka kunyanyuka" Yaani: Kutoka katika kikao, "Salamu Ya mwanzo haina haki zaidi" Yaani: Zote mbili ni sunna halisi zinazotakiwa kufanyiwa kazi, hakuna hiyari ya kuiacha ya pili na kuthibitisha ya kwanza.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 500) (5208). سنن الترمذي (4/ 432) (2706). السنن الكبرى للنسائي (9/ 144) (10129). مسند أحمد (12/ 47) (7142). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 360). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 142). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص523). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 672).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا لَقِيَ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ، فَإِنْ حَالَتْ بَيْنَهُمَا شَجَرَةٌ أَوْ جِدَارٌ أَوْ حَجَرٌ ثُمَّ لَقِيَهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ أَيْضًا».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena"
Imepokelewa na Abu DaudDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamhimiza muislamu kumsalimia ndugu yake muislamu kila anapokutana naye, hata kama wakiwa wanatembea pamoja na kikawatenganisha chochote, kama mti au ukuta au jiwe kubwa, kisha akakutana naye baada ya hapo basi amsalimie kwa mara nyingine.

Mafunzo
  1. Ni sunna kusambaza salam, na irudiwerudiwe kila hali inapobadilika.
  2. Pupa yake kubwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kusambaza sunna ya salam na kukithirisha; kwakuwa ndani yake kuna kuleta mapenzi na kuzoeana kati ya waislamu.
  3. Salaam ni kusema: "Assalaam alaikum" Amani iwe nanyi, au "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi na rehema zake na baraka zake", hii ni tofauti na kupeana mkono kunakotokea mara ya kwanza wakati wa kukutana.
  4. Salam ni dua, na waislamu wanahaja kubwa ya kuombeana wao kwa wao hata kama litajirudiarudia hilo.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 494) (5200). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص520). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 138). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 667). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 410).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi

عَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَيْنٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ، فَرَدَّ عَلَيْهِ ثُمَّ جَلَسَ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «عَشْرٌ» ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ: «عِشْرُونَ» ثُمَّ جَاءَ آخَرُ فَقَالَ: السَّلَامُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللَّهِ وَبَرَكَاتُهُ، فَرَدَّ عَلَيْهِ فَجَلَسَ، فَقَالَ: «ثَلَاثُونَ».
Kutoka kwa Imran bin Huswaini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi" Kisha akaja mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaah, akamjibu, akakaa, akasema: "Ishirini" Kisha akaja mtu mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh, akamjibu akakaa, akasema: "Thelathini".
Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy, Ahmad na Ad-DarimiDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Assalaam alaikum" Akamjibu kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ameandikiwa mema kumi, kisha akaja mtu mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullaahi" Akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Amepata thawabu ishirini, kisha akaja mwingine akasema: "Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", akamjibu akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kapata thawabu thelathini; yaani kwa kila tamko ni mema kumi.

Mafunzo
  1. Anayefika awaanze waliokaa kwa salamu.
  2. Malipo kuongezeka kwa kuzidi matamshi ya salamu.
  3. Ukamilifu katika kutoa salamu: "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", na namna nzuri katika kujibu: Ni "Waalaikumus salaam warahmatullaahi wabarakaatuh".
  4. Daraja za kutoa salamu na kujibu zinatofautiana, vile vile malipo yanatofautiana.
  5. Kuwafundisha watu kheri na kuwatanabahisha ili kufanya lililobora zaidi.
  6. Amesema bin Hajari: Ikiwa atazidisha mwenye kuanza "Warahmatullah" basi ni sunna kwake "wabarakaatuh", na ikiwa atazidisha "wabarakaatuh" je ni sheria pia kuzidisha wakati wa kujibu? Na vile vile ikiwa atazidisha mwenye kuanza "wabarakaatuh" je ni sheria kwake kufanya hivyo, ameitoa Maliki katika Muwattwa'a kutoka kwa bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Salamu imeishia katika baraka.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 491) (5195). سنن الترمذي (4/ 420) (2689). مسند أحمد (33/ 170) (19948). كنوز رياض الصالحين ، لمجموعة من الباحثين (11/ 246). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 132). نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (1/ 663). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 399).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya

عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «حَقُّ الْمُسْلِمِ عَلَى الْمُسْلِمِ خَمْسٌ: رَدُّ السَّلَامِ، وَعِيَادَةُ الْمَرِيضِ، وَاتِّبَاعُ الْجَنَائِزِ، وَإِجَابَةُ الدَّعْوَةِ، وَتَشْمِيتُ الْعَاطِسِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya haki za muislamu juu ya ndugu yake muislamu, Haki ya kwanza katika hizi ni kujibu salamu kwa atakayekutolea salamu. Haki ya pili: Kumtembelea mgonjwa na kumzuru. Haki ya tatu: Kulifuata jeneza kutoka nyumbani kwake mpaka mahali pa kuswalia mpaka makaburini mpaka kuzika. Haki ya nne: Kuitika wito anapomuita kuja katika walima wa harusi na mengineyo. Haki ya tano: Kumuombea dua mwenye kupiga chafya, nako ni kumwambia -Yarhamukallaah- (Akuhurumie Mwenyezi Mungu) atakapomhimidi Allah kwa kusema (Al-hamdulillah): kisha mpiga chafya amjibu: -Yahdiikumullaahu wayuslih baalakum- (Akuongozeni Allah na akutengenezeeni mambo yenu).

Mafunzo
  1. Utukufu wa Uislamu katika kuzitilia mkazo haki baina ya waislamu na kuupa nguvu udugu na mapenzi kati yao.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 71) (1240). صحيح مسلم (4/ 1704) (2162). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (4/ 512). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 327). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 253). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 591). بهجة قلوب الأبرار، لابن سعدي (ص81).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi

عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «يُسَلِّمُ الرَّاكِبُ عَلَى المَاشِي، وَالمَاشِي عَلَى القَاعِدِ، وَالقَلِيلُ عَلَى الكَثِيرِ». وَلِلبُخَارِي: «يُسَلِّمُ الصَّغِيرُ عَلَى الكَبِيرِ، وَالمَارُّ عَلَى القَاعِدِ، وَالقَلِيلُ عَلَى الكَثِيرِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi" Na kwa Bukhari: "Mdogo amsalimie mkubwa, na anayepita amsalimie aliyekaa, na wachache kwa wengi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika adabu za kutoleana salamu kati ya waislamu "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh". Mdogo amsalimie mkubwa, na aliyepanda amsalimie anayetembea kwa miguu, na anayetembea kwa mguu amsalimie aliyekaa, na idadi ndogo wawasalimie idadi kubwa.

Mafunzo
  1. Sunna ya kutoa salamu kwa mujibu wa yaliyokuja katika hadithi, mtembea kwa miguu anapomsalimia aliyepanda kipando, na wengineo katika hao waliotajwa, inafaa, lakini ni kwenda kinyume na kilicho bora zaidi.
  2. Kutoa salamu kwa namna iliyokuja katika hadithi ni katika sababu za mapenzi na kujenga umoja.
  3. Wakiwa wanalingana na wako sawa katika hayo yaliyotajwa, basi mbora wao ni yule atakayeanza kwa salamu.
  4. Ukamilifu wa sheria hii katika kubainisha yote anayoyahitaji mwanadam.
  5. Kufundisha adabu za salamu na kumpa kila mwenye haki haki yake.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 52) (6232). صحيح مسلم (4/ 1703) (2160). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 280). بهجة الناظرين، تأليف: سليم الهلالي (2/ 137). نزهة المتقين، مجموعة من الباحثين (1/ 666). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 407). منار القاري، لحمزة قاسم (5/ 257). الأدب النبوي (ص159).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpaka adhikike

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَبْدَؤوا الْيَهُودَ وَلَا النَّصَارَى بِالسَّلَامِ، فَإِذَا لَقِيتُمْ أَحَدَهُمْ فِي طَرِيقٍ فَاضْطَرُّوهُ إِلَى أَضْيَقِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpaka adhikike".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anakataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwaanza Mayahudi na Wakristo kwa salam, hata kama watakuwa wamepewa hifadhi katika nchi za kiislamu, achilia mbali makafiri wengineo, na akabainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tutakapokutana na mmoja wao njiani tumbane mahala pembamba, muumini ndiye atembee katikati ya njia, na anayepisha ni kafiri, na muislamu asiwe dhalili kwa hali yoyote ile.

Mafunzo
  1. Haitakiwi kwa muislamu kumuanza yeyote katika Mayahudi na Wakristo kwa salam, na makafiri wengineo.
  2. Inafaa kujibu salam zao wao watakapoanza kutoa salam kwa kusema: Na kwenu pia.
  3. Haitakiwi kwa muislamu kukusudia kumuudhi kafiri kwa kumbana kwa makusudi pasina sababu; ili amsukumie mahala pafinyu pa njia; lakini njia ikiwa nyembamba au inamsongamano basi muislamu ndiye mwenye haki zaidi, na kafiri ndiye apishe.
  4. Kudhihirisha utukufu wa waislamu na unyonge wa wasiokuwa wao, pasina kuwadhulumu au kuwaambia maneno machafu.
  5. Kuwabana makafiri ni kwa sababu ya ukafiri walionao wa kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, huenda hilo likawa sababu ya kusilimu; akasalimika na moto, ikiwa hilo litawafanya kujua sababu ya kufanyiwa hivyo.
  6. Hakuna ubaya kwa muislamu kumwambia kafiri mwanzo wa mazungumzo, vipi hali yako?, Umeamkaje? Umeshindaje? Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo; kwa sababu katazo hapa linachukuliwa ni katika salam ya kiislamu.
  7. Amesema Attwayibi: Kauli iliyopendekezwa nikuwa mtu wa bida haanzwi kwa salam, na akimsalimia asiyemjua kisha akabaini kuwa si muislamu asema: Nimerudisha salam yangu, kama kumdharau.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1707) (2167). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 141). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 303). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 42). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 670).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu

عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «لَا يَحِلُّ لِرَجُلٍ أَنْ يَهْجُرَ أَخَاهُ فَوْقَ ثَلَاثِ لَيَالٍ، يَلْتَقِيَانِ، فَيُعْرِضُ هَذَا وَيُعْرِضُ هَذَا، وَخَيْرُهُمَا الَّذِي يَبْدَأُ بِالسَّلَامِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu kumhama ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote hamsalimii wala hamsemeshi. Na mbora kati ya hawa wagomvi wawili ni yule anayejaribu kuondoa kuhamana huku, na akaanza kwa salamu, na makusudio ya kuhamana hapa ni sababu ya kujikweza, ama kuhamana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kuwahama waovu na wazushi na marafiki waovu, hili halina muda maalum, bali limeambatana na masilahi katika kuhama, na linamalizika kwa kuondoka maslilahi yake.

Mafunzo
  1. Uhalali wa kumhama mtu ndani ya siku tatu kurudi chini, kwa kulinda maumbile ya kibinadamu, itasamehewa ndani ya siku tatu, ili kiondoke kile kilichojitokeza baina yao.
  2. Ubora wa salamu, nakuwa huondoa yaliyoko ndani ya nafsi, nakuwa ni alama ya kupendana.
  3. Pupa ya Uislamu juu ya udugu na ukaribu baina waislamu.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 21) (6077). صحيح مسلم (4/ 1984) (2560). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 111). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 293). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 339).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الإِسْلاَمِ خَيْرٌ؟ قَالَ: «تُطْعِمُ الطَّعَامَ، وَتَقْرَأُ السَّلاَمَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ».
Kutoka kwa Abdallah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Aliulizwa Mtume rehema na amani zimfikie: Ni jambo lipi katika Uislamu ni bora? Akataja mambo mawili: La kwanza: Kukirithirisha kuwalisha masikini, na inaingia hapa sadaka na zawadi na kuwakirimu wageni na walima (harusi), na inatiliwa mkazo fadhila ya kulisha masikini katika nyakati za njaa na wakati wa bidhaa kupanda bei. La pili: Kumpa salamu kila muislamu, unayemjua na usiyemjua.

Mafunzo
  1. Pupa ya Masahaba katika kuyajua mambo yenye manufaa katika Dunia na Akhera.
  2. Salamu na kulisha chakula ni miongoni mwa amali bora katika Uislamu; kwa sababu ya fadhila zake na uhitaji wa watu juu ya chakula katika wakati wote.
  3. Kwa mambo haya mawili ihisani (wema) unakuwa kwa kauli na vitendo, nao ndio wema uliokamilika zaidi.
  4. Mambo haya ni katika mambo yanayohusu maisha ya waislamu baina yao, na kuna mambo yanahusu mahusiano ya mja na Mola wake.
  5. Kuanza kwa salamu ni maalumu kwa waislamu, haitolewi salamu kwa kumuanza asiyekuwa muislamu.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 12) (12). صحيح مسلم (1/ 65) (39). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 604). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (7/ 2936).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 9
Hadithi 9
  1. Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho
  2. Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena
  3. Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi
  4. Haki za muislamu juu ya muislamu mwenzake ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kufuata jeneza, na kuitika wito, na kumuombea dua mwenye kupiga chafya
  5. Amsalimie aliyepanda anayetembea, na anayetembea aliyekaa, na wachache kwa wengi
  6. Msiwaanze Mayahudi wala wakristo kwa salam, mkikutana na mmoja wao njiani basi mbaneni mpaka adhikike
  7. Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu
  8. Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua
  9. Hakuna waislamu wawili watakaokutana wakapeana mikono isipokuwa watasamehewa kabla hawajaachana

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com