Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekuja mahali walipokaa watu basi awasalimie, na akitaka kunyanyuka basi awaage jamaa zake pia kwa salamu; kwani salamu ya kwanza wakati wa kuja si bora sana kuliko salamu ya mwisho wakati wa kuondoka.
Mafunzo
Himizo la kusambaza salamu.
Himizo la kuwasalimia jamaa waliokaa wakati wa kukutana nao na wakati wa kuondoka.
Amesema Assanadi: Kauli yake: "Na akitaka kunyanyuka" Yaani: Kutoka katika kikao, "Salamu Ya mwanzo haina haki zaidi" Yaani: Zote mbili ni sunna halisi zinazotakiwa kufanyiwa kazi, hakuna hiyari ya kuiacha ya pili na kuthibitisha ya kwanza.
Marejeo
سنن أبي داود (7/ 500) (5208).
سنن الترمذي (4/ 432) (2706).
السنن الكبرى للنسائي (9/ 144) (10129).
مسند أحمد (12/ 47) (7142).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 360).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 142).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص523).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 672).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com