Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا لَقِيَ أَحَدُكُمْ أَخَاهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ، فَإِنْ حَالَتْ بَيْنَهُمَا شَجَرَةٌ أَوْ جِدَارٌ أَوْ حَجَرٌ ثُمَّ لَقِيَهُ فَلْيُسَلِّمْ عَلَيْهِ أَيْضًا».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapokutana mmoja wenu na ndugu yake basi na amsalimie, ukiwatenganisha kati yao mti, au ukuta, au jiwe, kisha akakutana naye tena basi amsalimie tena"
Imepokelewa na Abu DaudDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anamhimiza muislamu kumsalimia ndugu yake muislamu kila anapokutana naye, hata kama wakiwa wanatembea pamoja na kikawatenganisha chochote, kama mti au ukuta au jiwe kubwa, kisha akakutana naye baada ya hapo basi amsalimie kwa mara nyingine.

Mafunzo
  1. Ni sunna kusambaza salam, na irudiwerudiwe kila hali inapobadilika.
  2. Pupa yake kubwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kusambaza sunna ya salam na kukithirisha; kwakuwa ndani yake kuna kuleta mapenzi na kuzoeana kati ya waislamu.
  3. Salaam ni kusema: "Assalaam alaikum" Amani iwe nanyi, au "Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh", Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi na rehema zake na baraka zake", hii ni tofauti na kupeana mkono kunakotokea mara ya kwanza wakati wa kukutana.
  4. Salam ni dua, na waislamu wanahaja kubwa ya kuombeana wao kwa wao hata kama litajirudiarudia hilo.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 494) (5200). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص520). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 138). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 667). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 410).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za kutoa salamu na kubisha Hodi.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com