Anakataza Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwaanza Mayahudi na Wakristo kwa salam, hata kama watakuwa wamepewa hifadhi katika nchi za kiislamu, achilia mbali makafiri wengineo, na akabainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa tutakapokutana na mmoja wao njiani tumbane mahala pembamba, muumini ndiye atembee katikati ya njia, na anayepisha ni kafiri, na muislamu asiwe dhalili kwa hali yoyote ile.
- Haitakiwi kwa muislamu kumuanza yeyote katika Mayahudi na Wakristo kwa salam, na makafiri wengineo.
- Inafaa kujibu salam zao wao watakapoanza kutoa salam kwa kusema: Na kwenu pia.
- Haitakiwi kwa muislamu kukusudia kumuudhi kafiri kwa kumbana kwa makusudi pasina sababu; ili amsukumie mahala pafinyu pa njia; lakini njia ikiwa nyembamba au inamsongamano basi muislamu ndiye mwenye haki zaidi, na kafiri ndiye apishe.
- Kudhihirisha utukufu wa waislamu na unyonge wa wasiokuwa wao, pasina kuwadhulumu au kuwaambia maneno machafu.
- Kuwabana makafiri ni kwa sababu ya ukafiri walionao wa kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, huenda hilo likawa sababu ya kusilimu; akasalimika na moto, ikiwa hilo litawafanya kujua sababu ya kufanyiwa hivyo.
- Hakuna ubaya kwa muislamu kumwambia kafiri mwanzo wa mazungumzo, vipi hali yako?, Umeamkaje? Umeshindaje? Ikiwa kuna haja ya kufanya hivyo; kwa sababu katazo hapa linachukuliwa ni katika salam ya kiislamu.
- Amesema Attwayibi: Kauli iliyopendekezwa nikuwa mtu wa bida haanzwi kwa salam, na akimsalimia asiyemjua kisha akabaini kuwa si muislamu asema: Nimerudisha salam yangu, kama kumdharau.
صحيح مسلم (4/ 1707) (2167). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 141). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 303). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 42). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 670).