Al-Munaafiqoon 63:10
المنافقونوَأَنفِقُوا۟ مِن مَّا رَزَقْنَـٰكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِىَ أَحَدَكُمُ ٱلْمَوْتُ فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَآ أَخَّرْتَنِىٓ إِلَىٰٓ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن مِّنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na toeni katika tulichokupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: 'Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo, nipate kutoa sadaka sana, na niwe katika watu wema?'
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na niwe katika watu wema? [10]
[10] Enyi Waumini! Toeni katika mali tuliyo kuruzukuni upesi upesi kabla mmoja wenu hayajamfikia mauti akasema kwa majuto: Ewe Mola wangu Mlezi! Hebu hunipi muhula kidogo, nikapata kutoa sadaka, na nikawa miongoni wa watu wema watendao vitendo vyema?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na toeni, (enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake), sehemu ya kile tulichowapa katika njia za kheri, mkilikimbilia hilo kabla ya kifo hakijamjia mmoja wenu na kuziona dalili zake na alama zake, na hapo aseme kwa kujuta, «Mola wangu! Si unipe muda na uahirishe kifo changu kipindi kifupi! Nipate kutoa sadaka sehemu ya mali yangu na niwe miongoni mwa watu wema wachamungu?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net