Al-Munaafiqoon 63:11
المنافقونوَلَن يُؤَخِّرَ ٱللَّهُ نَفْسًا إِذَا جَآءَ أَجَلُهَا ۚ وَٱللَّهُ خَبِيرٌۢ بِمَا تَعْمَلُونَ
Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote unapofika muda wake. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapo fika ajali yake; na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda. [11]
[11] Wala Mwenyezi Mungu hampi muhula mtu yeyote ukisha fika wakati wake wa kufa. Na Mwenyezi Mungu ni Mkamilifu wa kujua yote myatendayo, na Yeye atakulipeni kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wala Allah Mtukufu hataichelewesha nafsi yoyote utakapokuja wakati wa kifo chake na umri wake kukoma. Na Allah Mtukufu, kutakasika na kila sifa ya upungufu ni Kwake, ni mtambuzi wa yale mnayoyatenda: mema na mabaya, na Atawalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net