Al-Munaafiqoon 63:9
المنافقونيَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَٰلُكُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُكُمْ عَن ذِكْرِ ٱللَّهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ
Enyi mlioamini! Zisikusahaulisheni mali zenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo, basi hao ndio waliohasiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi mlio amini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio khasiri. [9]
[9] Enyi mlio msadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake! Yasikuhangaisheni mali yenu, na watoto wenu, hata mkaacha kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kutekekeleza aliyo kuamrisheni kuyafanya. Na wenye kushughulishwa na mali zao na watoto wao wakaacha hayo, basi hao ndio watao kuwa wamekhasiri Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! zisiwashughulishe mali zenu wala watoto wenu na kumuabudu Allah Mtukufu na kumtii. Na yoyote atakayeshughulishwa na mali Yake na watoto Wake na hilo la kumuabudu Allah Mtukufu, basi hao ndio waliopunjwa hisa zao za kukurubishwa kwa Allah Mtukufu na kupata rehema zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net