Al-An'aam 6:149
الأنعامقُلْ فَلِلَّهِ ٱلْحُجَّةُ ٱلْبَـٰلِغَةُ ۖ فَلَوْ شَآءَ لَهَدَىٰكُمْ أَجْمَعِينَ
Sema: Basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hoja ya kukata. Na kama angelitaka, angeliwaongoa nyote.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Basi Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye hoja ya kukata. Na kama angeli penda angeli kuhidini nyote. [149]
[149] Ewe Nabii! Sema: Mwenyezi Mungu ana hoja iliyo wazi kuwa nyinyi ni waongo katika madai yenu kuwa Mwenyezi Mungu ameridhia vitendo vyenu! Wala hamna hoja katika ushirikina wenu, na kuhalalisha kwenu, na kuharimisha kwenu, na mengineyo. Na Mwenyezi Mungu angeli taka mhidike angeli kuhidini nyote mkafuata Njia ya Haki. Lakini hakutaka hayo kwa kuwa nyinyi mmekhiari njia ya upotovu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia wao, «Allah Mtukufu, aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye Mwenye hoja yenye kuzikata dhana zenu. Na lau angalitaka Angaliwaongoza nyote kwenye muelekeo wa sawa».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net