Al-An'aam 6:150
الأنعامقُلْ هَلُمَّ شُهَدَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا۟ فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا وَٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ
Sema: Waleteni mashahidi wenu ambao wanashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu amewaharamisha hawa. Kwa hivyo, wakishuhudia, basi wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya wale waliozikadhibisha Ishara zetu, na ambao hawaamini katika Akhera, nao wanamlinganisha Mola wao Mlezi na wengine.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Leteni mashahidi wenu watao shuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ameharimisha hawa. Basi wakishuhudia, wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya walio zikanusha Ishara zetu, wala hawaiamini Akhera, na ambao wanamlinganisha Mola Mlezi wao na wengine. [150]
[150] Ewe Nabii! Waambie: Leteni wasaidizi wenu watakao kushuhudieni kwamba kweli Mwenyezi Mungu ameharimisha hivi mnavyo dai kuwa ni haramu. Wakihudhuria na wakashuhudia, basi wewe usiawasadiki, kwa sababu hao ni waongo. Wala usifuate matamanio ya hawa walio kanusha hoja za uumbaji na Qur'ani inayo somwa, na ambao hawaiamini Akhera nao wanamshirikisha Mwenyezi Mungu, wanamfanya Yeye sawa na hao miungu inayo abudiwa kwa uwongo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina, «Waleteni mashahidi wenu ambao watatoa ushahidi kwamba Allah Mtukufu Ndiye Aliyeharamisha vile mlivyoviharamisha vya mazao na wanyama howa.» Wakitoa ushahidi huo, kwa urongo na uzushi, usiwaamini wala usikubaliane na wale waliojitolea uamuzi wenyewe kulingana na mapendeleo ya nafsi zao, wakazikanusha aya za Allah Mtukufu katika yale waliyoyashikilia ya kukiharamisha Alichokihalalisha Allah Mtukufu na kukihalalisha Alichokiharamisha Allah Mtukufu. Wala usiwafuate wale ambao hawayaamini maisha ya Akhera wala wasiotenda vitendo vya kuwafaa huko na wale ambao Mola wao wanamshirikisha wakawa wanamuabudu mwingine pamoja na Yeye.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net