Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 148

Al-An'aam 6:148

الأنعام

سَيَقُولُ ٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ لَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشْرَكْنَا وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمْنَا مِن شَىْءٍ ۚ كَذَٰلِكَ كَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ حَتَّىٰ ذَاقُوا۟ بَأْسَنَا ۗ قُلْ هَلْ عِندَكُم مِّنْ عِلْمٍ فَتُخْرِجُوهُ لَنَآ ۖ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَإِنْ أَنتُمْ إِلَّا تَخْرُصُونَ

Maana

Watasema wale walioshirikisha, "Lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, tusingelishirikisha, wala baba zetu, wala tusingeliharamisha kitu chochote." Hivyo ndivyo walivyokadhibisha wale waliokuwa kabla yao mpaka walipoionja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo elimu yoyote mtutolee hiyo? Nyinyi hamfuati isipokuwa dhana. Wala hamfanyi isipokuwa kukisia tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watasema walio shirikisha: Lau kuwa Mwenyezi Mungu ange taka tusingeli shiriki sisi, wala baba zetu; wala tusingeli harimisha kitu chochote. Vivi hivi walikanusha walio kuwa kabla yao mpaka walipo onja adhabu yetu. Sema: Je, nyinyi mnayo ilimu mtutolee? Nyinyi hamfuati ila dhana. Wala hamsemi ila uwongo tu. [148]

[148] Kwa kutaka kujitolea udhuru kwa ushiriki wao, na kule kuharimisha vyakula alivyo halalisha Mwenyezi Mungu, na kukanusha yaliyo wafikia kuwa Mwenyezi Mungu kaudhika nao kwa vitendo vyao, washirikina watasema: Ushirikina wetu na kuharimisha alicho halalisha Mwenyezi Mungu, ni kwa mujibu wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na kuridhi kwake! Na lau angeli penda Yeye kinyume cha hayo, na angeli chukia tuyatendayo, basi tusingeli mshirikisha sisi wala walio tutangulia, na wala tusingeli harimisha kitu chochote alicho tuhalalishia. Na walio kabla yao waliwakadhibisha Mitume wao, kama hawa wanavyo kukadhibisha wewe. Na waliendelea katika kukanusha kwao mpaka ikawafikia adhabu yetu! Waambie hawa wanao kanusha: Jee mnao ushahidi wa kutegemea ulio sahihi ya kwamba Mwenyezi Mungu amekuridhieni nyinyi mumshirikishe na mhalalishe, mkatutolea? Katika maneno yenu hamfuati ila kudhania tu. Na hiyo haitoshelezi chochote katika Haki. Na nyinyi si chochote, si lolote, ila ni waongo tu katika hayo mnayo dai.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watasema wale walioshirikisha, «Lau Allah Mtukufu angetaka tusishirikishe, sisi na baba zetu, na tusihararamishe kitu chochote kinyume na matakwa Yake, hatungalifanya hilo.» Hapo Allah Mtukufu Aliwarudi kwa kuwaeleza kwamba utata huu ulivumishwa na makafiri kabla yao, wakautumia kuukanusha ulinganizi wa Mitume wao na wakaendelea kufanya hivyo mpaka ikawateremkia adhabu ya Allah Mtukufu. Waambie, ewe Mtume, «Je, mnayo elimu sahihi mtuoneshe, juu ya wanyama howa na makulima mliyoharamisha na juu ya madai yenu kwamba Allah Mtukufu Aliwatakia ukafiri, Akauridhia kwenu na Akaupendelea kwenu? Hamna mnachofuata, katika mambo ya dini, isipokuwa dhana tu; na hamkuwa nyinyi isipokuwa mnasema urongo».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net