Al-An'aam 6:147
الأنعامفَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَٰسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُۥ عَنِ ٱلْقَوْمِ ٱلْمُجْرِمِينَ
Na wakikukadhibisha, basi wewe sema: Mola wenu Mlezi ni Mwenye rehema kunjufu. Wala haizuiwi adhabu yake kwa kaumu wahalifu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wakikukanusha basi wewe sema: Mola Mlezi wenu ni Mwenye rehema iliyo enea. Wala haizuiliki adhabu yake kwa watu wakhalifu. [147]
[147] Wakanushi wakikukanusha katika haya tuliyo kuletea wahyi, waambie kwa kuwahadharisha: Hakika Mola Mlezi wenu, ambaye anapasa mumuamini Yeye peke yake, na mfuate hukumu zake, ana rehema iliyo enea na kumfikia kila anaye mt'ii, na pia anaye muasi kwa kuwa hafanyi haraka kuwaadhibu. Na lakini haitakikani mghurike na hivyo kuwa rehema yake imeenea kote, kwa sababu adhabu yake haina budi kuwafikia hao wakhalifu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wakikufanya mrongo, ewe Mtume, wanaokwenda kinyume na wewe miongoni mwa washirikina, Mayahudi na wengineo, waambie, «Mola wenu, Aliyetukuka na kuwa juu, ni Mwenye rehema kunjufu. Na wala haiepushwi adhabu Yake kwa watu waliotenda maovu wakapata madhambi na wakajitokeza wazi na ubaya. Katika haya pana onyo kwao, kwa kwenda kwao kinyume na Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net