Al-An'aam 6:146
الأنعاموَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا كُلَّ ذِى ظُفُرٍ ۖ وَمِنَ ٱلْبَقَرِ وَٱلْغَنَمِ حَرَّمْنَا عَلَيْهِمْ شُحُومَهُمَآ إِلَّا مَا حَمَلَتْ ظُهُورُهُمَآ أَوِ ٱلْحَوَايَآ أَوْ مَا ٱخْتَلَطَ بِعَظْمٍ ۚ ذَٰلِكَ جَزَيْنَـٰهُم بِبَغْيِهِمْ ۖ وَإِنَّا لَصَـٰدِقُونَ
Na Mayahudi tuliwaharamishia kila mwenye kwato au mguu usio na mgawanyiko. Na katika ng'ombe, na kondoo, na mbuzi tuliwaharamishia shahamu yao, isipokuwa ile iliyobeba migongo yao au matumbo yao, au iliyochanganyika na mifupa. Hayo tuliwalipa kwa sababu ya uasi wao. Nasi bila ya shaka ni wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio fuata dini ya Kiyahudi tumewaharimishia kila mwenye kucha. Na katika ng'ombe na kondoo na mbuzi tumewaharimishia shahamu yao, isipo kuwa ile iliyo beba migongo yao au matumbo yao, au iliyo gandamana na mifupa. Tuliwalipa hivyo kwa sababu ya uasi wao. Na bila ya shaka Sisi ndio wasema kweli. [146]
[146] Basi hivi ndivyo tulivyo kuharimishieni nyinyi. Na Mayahudi tuliwaharimishia nyama na shahamu na kila kitu cha wenye makucha katika wanyama, kama ngamia na wanyama wawindao. Na katika ng'ombe na mbuzi na kondoo tuliwaharimishia shahamu yake tu, ila shahamu ya mgongoni, au iliyoko matumboni, au iliyo changanyika na mafupa. Na kuharimishwa huku kulikuwa kwa ajili ya kuwatesa tu kwa ajili ya dhulma zao, na kuziachisha nafsi zao waweze kujilinda na matamanio. Na hakika Sisi tunasema kweli katika maneno yetu yote, na miongoni ya hayo ni khabari hii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na watajie washirikina hawa, ewe Mtume, wanyama na ndege tuliowaharamishia Mayahudi: nao ni kila ambaye hana pasuko vidoleni mwake, kama ngamia na mbuni, na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo isipokuwa yale mafuta yaliyoshikana na migongo ya wanyama hao na tumbo zao, au yaliyoshikana na mfupa wa mkia na mbavu na mfano wake. Uharamishaji huu uliotajwa juu ya Mayahudi ni adhabu kutoka kwetu kwa sababu ya matendo yao maovu. Na sisi ni wakweli kwa yale tuliyoyaeleza kuhusu wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net