Al-An'aam 6:129
الأنعاموَكَذَٰلِكَ نُوَلِّى بَعْضَ ٱلظَّـٰلِمِينَ بَعْضًۢا بِمَا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
Na namna hivi ndivyo tunavyowafanya baadhi ya madhalimu wapendane wao kwa wao kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ndio kama hivi tunawaelekeza madhaalimu wapendane wao kwa wao kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyachuma. [129]
[129] Kama tulivyo wawacha waasi wa kibinaadamu na wa kijini wakistareheshana wao kwa wao, basi amewajaalia madhaalimu wawe ni marafiki wao kwa wao, kwa sababu ya madhambi makubwa wanayo yachuma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kama tulivyowapa uwezo mashetani wa kijini juu ya makafiri wa kibinadamu wakawa ni wategemewa wao, hivyohivyo tunawapa uwezo madhalimu wa kibinadamu juu ya wenyewe kwa wenyewe duniani kwa sababu ya maasia wayafanyayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net