Al-An'aam 6:130
الأنعاميَـٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتِى وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَآءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا۟ شَهِدْنَا عَلَىٰٓ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا وَشَهِدُوا۟ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ كَـٰفِرِينَ
Enyi kundi la majini na watu! Je, hawakuwajia Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakiwabainishia Aya zangu, na wakiwasimulia kukutana na Siku yenu hii? Nao watasema, “Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu.” Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watashuhudia dhidi yao wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri. [130]
[130] Na Mwenyezi Mungu Mtukufu atawaambia Siku ya Kiyama: Enyi watu na majini! Mitume wamekujieni wakikutajieni hoja na dalili zilizo wazi, na wakikusomeeni Aya, na wakikuonyeni na mkutano wa Mwenyezi Mungu katika Siku yenu hii. Basi vipi mnakanusha? Nao watajibu: Tunakubali wenyewe madhambi tuliyo yatenda. Na maisha ya kidunia yaliwakhadaa kwa starehe zake, na wakajikiria nafsi zao kuwa hakika wao walikuwa wapinzani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Enyi majini na binadamu mlio washirikina, kwani hawakuwajia Mitume miongoni mwenu- Maandiko yanaonesha kuwa Mitume wanatoka kwa wanadamu tu.(1)- wanaowapa habari za alama zangu zilizo wazi, zinazokusanya maamrisho na makatazo, zinazofafanua kheri na shari na wanaowaonya kukumbana na adhabu yangu Siku ya Kiyama? Watasema washirikina hawa, majini na binadamu, «Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu kwamba Mitume 1 Hii ndio kauli yenye nguvu ya maimamu wa n aya si dalili wazi ya kuwa kuna Mitume wa kijin kusherehesha aya hii. wako wametufikishia aya zako na wametuonya makutano ya Siku yetu hii, na sisi tukawakanusha.» Na hawa washirikina, liliwadanganya wao pambo la maisha ya dunia. Na walizishuhudilia nafsi zao kwamba wao walikuwa wakiukataa upweke wa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na wakiwafanya warongo Mitume Wake, amani iwashukie.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net